Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Friedrich Nietzsche

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
1,237
2,203
Nina kijana wa miaka 17.
Wa kiume ni mpole na mkimya lakini hayuko smart.Tofauti na ilivo kwa watu wengi wa kimya kwa kua na akili nyingi kwa kijana wangu ni tofauti ni mkimya ila sasa akija kuongea unaweza ukajiuliza ameongea wire ukiwa connected kwene switch au Laaah.

Shuleni ni average sana si mkia maksi zake 46,67,37,50,30 kifupi alipata division 3 .
Kinachonitatiza ni uwezo wa kufikiria na kuchanganua mambo mdogo. Maswali ya kawaida ya kutumia common sense hawezi !!
Ukimuelekeza kitu cha kawaida haelewi mara moja had urudie
Ni rahisi kuchanganya vitu na kusahau.
Kifupi anashindwa kujisimamia au kupambanua vitu vya kawaida vya uelewa wa kawaida .

Alafu sometimes anachanganya vitu havihusiani
Ukimuuliza swali anajibu jibu ambalo halina uhusiano na ulichomuuliza!

MIMI MZEE WAKE NIKO VIZURI!Sijui hata karithi kwa nani haya matatizo ,,,, shulen mm nilikua smart siyo sana lakin smart kiasi cha kumlizisha mzazi yyte yule average

Nifanyaje kumsaidia
 
Tuanze na lishe unayompatia nyumbani, je ni mlo kamilii?.

Twende kwenye malezi unayompa hapo nyumbani, je ni malezi ya kumfanya aweze kujitegemeaa?

Tuelekee kwenye lugha ya mawasiliano kati yenu, je huwa unamkaripia/kumgombeza mara kwa mara?

Je, kwa wastani mwili wake upoje, je ni mnene, mkakamavu au lege lege?

Vipi anashiriki michezo yoyote shuleni kwao au hata hapo mtaani?.

Ni mwanao wangapi kuzaliwq kwenye hiyo familia yako?.

Graph yake ya makuzi kadi ya clinic ilikuwaje au ipoje kama bado upo nayo? (Ni muhimu sana kutunza hiyo kadi)

Ukimaliza hayo yote, vipi mwanao huyo ana mpenzi? Kama hana wewe kama baba yake umemsaidiaje hilo swala?. (Usishangae ni jukumu lako mshua)

Ukiona mwanao hawezi kucheka mbele yako inabidi ujitafakari upya kiongozi, kuna kitu kikubwa hakipo sawa kati yenu.

Tafakari hayo machache Mkuu mwenzetu, kila la heri.
 
havihusiani
Ukimuuliza swali anajibu jibu ambalo halina uhusiano na ulichomuuliza

Huyo dogo sio kwamba hana akili , ila akili yake imezidi vile mnavyotaka kumkaririsha , kuna mambo tumejiwekea limits ,mwingne akifikiri njee na hayo mnamwona hana akili ,na apo ndipo tunapofeli .

Ndio maana leo tunajiuliza wale wanafunzi watukutu na wasumbufu mashuleni imekuaje wametoboa kimaisha ,kumbe wao ndio mwenye akili wamegoma kufungiwa kwenye box moja .

Unachotakiwa kufanya ni kuangalia ubora wa dogo upo wap ,ndio utilie mkazo huko , akijua kusoma na kuandika inatosha kabisa .
 
Tuanze na lishe unayompatia nyumbani, je ni mlo kamilii?.

Twende kwenye malezi unayompa hapo nyumbani, je ni malezi ya kumfanya aweze kujitegemeaa?

Tuelekee kwenye lugha ya mawasiliano kati yenu, je huwa unamkaripia/kumgombeza mara kwa mara?

Je, kwa wastani mwili wake upoje, je ni mnene, mkakamavu au lege lege?

Vipi anashiriki michezo yoyote shuleni kwao au hata hapo mtaani?.

Ni mwanao wangapi kuzaliwq kwenye hiyo familia yako?.

Graph yake ya makuzi kadi ya clinic ilikuwaje au ipoje kama bado upo nayo? (Ni muhimu sana kutunza hiyo kadi)

Ukimaliza hayo yote, vipi mwanao huyo ana mpenzi? Kama hana wewe kama baba yake umemsaidiaje hilo swala?. (Usishangae ni jukumu lako mshua)

Ukiona mwanao hawezi kucheka mbele yako inabidi ujitafakari upya kiongozi, kuna kitu kikubwa hakipo sawa kati yenu.

Tafakari hayo machache Mkuu mwenzetu, kila la heri.
ana mpenzi heeeh kijana wangu bado hajaanza hayo mambo mzee
 
hapendi michezo anapenda kulala lala
hawezi cheza mbele yangu
Mi nimkali hasa linapokuja suala la shule
amelelewa na mama ake nimemchukua akiwa darasa la tatu
 
ana mpenzi heeeh kijana wangu bado hajaanza hayo mambo mzee
Ohoo, tatizo lipo na hapa pia, wewe unamchukulia poa huyo kijana wako. Huyo ni kijana mkubwa vyakutosha kuwaza mapenzi na hata kuyafanya. Sasa jukumu ni lako kumsaidia awe timamu.

Usione soo, mfundishe vitu vidogo vidogo kama matumizi ya condoms, na namna ya kuchagua mwanamke bora amfae maishani. Mwanao ataanza kujiamini
 
Back
Top Bottom