MOTOCHINI
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 27,850
- 30,931
Wacha mambo ya ajabu weweTundaman kafa au? Hii habari mbaya kwa tasnia ya muziki
Unashitua watu bwana
Wacha mambo ya ajabu weweTundaman kafa au? Hii habari mbaya kwa tasnia ya muziki
Da! Pole sanaMwanamziki Tundaman apata ajali mbaya Eneo la Idetelo, katikati ya Nyololo la Makambako, aliyekuwa naye katika gari aina ya Toyota Aaron, apoteza maisha.
Maiti inapelekwa hospitali ya wilaya ya Mufindi....kwa mujibu wa mpashaji aliyepo Nyololo.
=====
UPDATE:
Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki‘
Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.
Pole zake jamani
Yaani ukishapita tu mafinga kama unaelekea mbeya kuna mashimo balaaa,yaani nimepita juzi na mvua zinapiga yaani ni balaaa,mahandaki ya kutosha.Hiyo barabara kuanzia mji mdogo wa mafinga mpaka mbeya ni shida. Wakandarasi waongeze tu bidii ikamilike kwa wakati ili ajali zipungue kama sio kuisha kabisa.
Taarifa hizi nizakweliNgoja nisubirie taarifa kamili
Pamoja na mashimo, ajali hii inaonekana si mashimo ila watu wote akiwemo dereva mwenyewe waliokuwepo kwenye gari hilo walilala usingizi wa pono.Walikuwa wanawahi Dar na hiyo Dar hadi mda huu hawajafika toka saa kumi alfajiri,ni uzembe wa kiwango cha juu sana unaohatarisha uhai wa watumiaji wengine wa barabara.Watu walikuwa kwenye show usiku mzima then mnataka kusafiri bila kupumzika wakati huohuo mnaona mmechoka sana.Yaani ukishapita tu mafinga kama unaelekea mbeya kuna mashimo balaaa,yaani nimepita juzi na mvua zinapiga yaani ni balaaa,mahandaki ya kutosha.
Kuna na ile sehem wanakaa trafic mpkn mwa njombe na mbeya,aisee ni mashimo tu.
aisee hilo eneo halina mashetani?maana naona nyuma ya hilogari kuna Traile nalo limeanguka bondeni.
acha kuishi maisha ya kufikirika kwenye huu ulimwengu wenye technology,Watu wamekesha kwenye show halafu alfajiri wanaunganisha Safari ili wawahi kufika Dar bila hata kulala au kupumzika! Acha mawazo ya kijinga hayo.pole sana bt nahisi FREEMASON AT WORK
Mh Kwani kafarikiREST IN PEACE TUNDAMAN