Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nimemshangaa sana huyu jamaa jinsi anavyowashikia akili waumini wake na kumhusisha Mungu na mambo ya kishetani (CCM). Huu uthubutu kaupata wapi? Analindwa na nani hadi awapotoshe watu hadharani kiasi hiki?Mtanzania yeyote mwenye pesa ukimuona yuko CCM jua kuwa huyo pesa zake ni za haramu.
CCM ndio njia nzuri ya kuzilinda pesa zako za haramu katika nchi hii
Kweli. Baada ya kuona kiboko ya wachawi amefungiwa huduma na CCM, yeye ameamua kula meza .moja na mafisadi wa CCM."Tatizo njaa" - Hashimu Rungwe
"Hauwezi kula bila kuliwa,unataka kula peke yako haiwezekani ,sina maana hiyo" - Jakaya Kikwete
Anasema watu wakeMAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda.
hatari iliyopo, kama leo anaweza kuwaelekeza anaowaita "watu wangu" kupigia ccm, kesho anaweza kuwaelekeza kupigia mtu wake toka kwenye dini yake, na siku ingine toka kwenye kabila lake. ameongea ujinga mkubwa sana.
Kweli. Huyu askofu atakuwa analiwa sio bure. Baada ya kuona kiboko ya wachawi amefungiwa huduma na CCM, yeye ameamua kula meza .moja na mafisadi wa CCM. Mpuuzi sana huyu jamaa.
Ndio hao wanaonua maji na mafutaAnasema watu wake
Yeye ana watu?
Mkuu umemaliza kila kitu. Huyu jamaa amelewa hela za bwerere, hasa baada ya kujenga hoteli ya nyota 5 inayomuingizia mamilioni ya pesa kila siku. Heri kuvimbiwa chakula kuliko kuvimbiwa fedha. Tangu Mwamposa alipovimbiwa pesa, anajiona yeye ndiye kila kitu hapa nchini. Mungu amsamehe bure.Huyu ni mchonganishi sana. soon atatokea shehe naye ataelekeza watu wapigie cuf. atakuja mchungaji ambaye hamkubali mwamposa atataka aongee kumkosoa na kuelekeza watu wampigie fulani, analeta fujo tu, shida ni shule na exposure. ukipata pesa za kitapeli wakati hukutarajia unajiona kama mkuuubwa. yaani yeye ndiye wa kuamulia watanzania hatima zao? hadi wasomi kabisa wanapokea maelekezo toka kwa huyu mnyakyusa tapeli wa dini?
wapentekoste najua wote wanapinga mafundisho ya mwamposa, wakatoliki wanapinga mafundisho yake, walutheran kadhalika. vipi hao nao wakijiunga wakatoa misimamo na maelekezo? yaani yeye kukusanya vile watu anaamini amekusanya watanzania wote? na vipi dini ya kiislam nao wakianza hivyo kuelekeza watu wapigie kuwa yule wanayemtaka? huyu anawaharibia though yeye anafikiri anawasaidia ccm.