tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,539
- 21,567
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.
Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.
MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.
Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.
Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.