ecolizer baba
Member
- Sep 29, 2010
- 88
- 310
Wadau nawasalimu asubuhi njema kama ya leo.
Jana IEBC ilifanya kikao cha pamoja na vyama vya Jubilee na Muungano wa NASA.
Baada ya kile kikao pande zote tatu zilizungumza kama ifuatavyo:
JUBILEE:
1. Walidai kuwa wanaridhishwa na jinsia maandalizi ya Uchaguzi yanayofanywa na IEBC yanaenda.
2. Hawana Minimum Demands wala Irreducible minimum Demands toka kwa IEBC.
3. Kwa sasa wanaelekeza nguvu zao zote kwenye kampeni kwa siku zilizosalia na hawategemei tena kufika IEBC hadi baada ya Uchaguzi wa tarehe 26.
NASA:
NASA walienda IEBC wakiongozwa na Raila Odinga huku vinara wengine wa muungano huo wakiwa wapo pia pamoja na wanasheria wao.
1. Hakuna jambo lolote kwenye irreducible Minimus lililotimizwa na IEBC.
2. Wataendelea na Maandamano yao ya kudai matakwa yao yatimizwe na IEBC.
3. Bado wataendelea kushinikiza Kampuni ya Safran Morpho na Safaricom kutopewa tenda ya kushughulika na Uchaguzi.
IEBC:
IEBC wakiongozwa na Wafula Chebukati:
1. Matakwa mengi ya NASA yameshatimizwa.
2. Safran Morpho na Safaricom na Alguhair wataendelea kuhusika na Uchaguzi huu.
Sasa baada ya yote hayo the cards are clear now. Ni kwamba kwa hali inavyokwenda kwa sasa ni wazi kuwa Uhuru Kenyatta ana nafasi kubwa ya kushinda. Kwanza wao wameshasema kuwa hawawadai IEBC jambo lolote. Huu ni mwiba mchungu kwa NASA kwa sababu wananchi na jumuiya za kimataifa watajua kuwa mwenye shida sasa ni NASA na wala siyo Jubilee wala IEBC.
Ushauri wangu kwa Raila na NASA wenzake ni kwamba kwa muda huu uliobaki waekekeze nguvu zao kukamilisha kwenye kampeni kuliko kufanya maandamano na press conference kuongelea mambo yale yale ambayo vyovyote iwavyo Uchaguzi upo pale pale.
Asanteni sana.