Mikakati ya Uhuruto na Jubilee itamuacha Raila na historia ambayo haitasahaulika kamwe.

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Wadau kama kawaida yangu nianze kwa kuwasalimu, Assalam Alleikum!!

Bado nazidi kufuatilia siasa za Kenya wakati huu nchi hiyo inapoelekea kwenye Uchaguzi wa marudio.

Niseme tu mapema kuwa Raila Odinga na NASA yake wameshachoka mapema. Na ni dhahiri kuwa ndani ya NASA mtu pekee aliyesalia kuwa resilient and solid ni Raila Odinga. Wengine kuanzia kwa Musyoka, Mudavadi na Wetangula wameshakata tamaa. Kwa hiyo wamebaki kuburuzwa na Odinga. Unaweza kuligundua hili kwa kuangalia facial expression na body language ya vigogo hao wa NASA.

Kwa upande wa pili Uhuruto na Jubilee wameamua kujizatiti vilivyo. The way ambavyo hawa vinara wawili wa jubilee walivyosimama imara bila kutetereka pamoja na kwamba ushindi wao wa awali ulitupiliwa mbali unaonesha namna walivyojiandaa kuibuka washindi kwa mara nyingine.

Mikakati ifuatayo waliyoamua kuutumia kwenye ngwe hii Hakika hatamuacha Raila na NASA yake salama:

1. Kuwavutia viongozi na wanachama wa Upinzani: Alianza Isaack Ruto kule Bomet kisha wakafuatia wengine kama akina Alfred Mutual na waliowahi kwa namna moja ama nyingine kuwa wabunge wa upinzani na hasa ODM. Hii imewafanya Jubilee kuwa na uhai mkubwa kwenye ngome ya upinzani hasa maeneo ya magharibi mwa Kenya.
2. Kuwapa Wabunge waliochaguliwa toka ngome za Wapinzani nafasi ya kuongoza mabunge ya Senate na National Assembly. Moturi wa NA, Lusaka wa Senate na Chief Whip wa NA wote wanatoka ngome ya Raila Odinga. Hii itawafanya wananchi wa maeneo husika ambao hawakumchagua Uhuru Kenyatta last time wampe kura this time around.

3. Kutamka dhahiri kuwa hapana madai yoyote na IEBC: Juzi, William Ruto alipoenda kumwakilisha Kenyatta kule IEBC alitamka wazi kuwa hawana Minimum demands wala irreducible minimum demands toka IEBC na kwa hiyo kuwapongeza IEBC kwa maandalizi waliyokuwa wakiendelea nayo. Kwa upande mwingine Raila amedndelea kushikilia msimamo wake wa kutoka IEBC itimize irreducible Mimimu demands zao vinginevyo hawatashiriki Uchaguzi. Kumbuka hii inakuja baada ya kikao cha juzi ambacho kiliwakutanisha IEBC, Jubilee na NASA ambacho kiliombwa na NASA wenyewe. Lakini baada ya kikao wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutoshiriki Uchaguzi.

4. Uhuruto kukutana na viongozi na/au watu wenye ushawishi toka jamii mbalimbali: Wawakilishi wa jamii mbali mbali wamealikwa na Uhuru Kenyatta kwenda ikulu ili kuwaomba wamuombee kura. Hili limekuwa na mafanikio makubwa kwani jubilee imetumia nafasi hiyo kufika maeneo ambayo haikuwa na nguvu awali.

5. Kuendelea na Kampeni kwa nguvu ile ile na mikakati mipya: Uhuruto wameendelea na kampeni kwa nguvu ile ile kana kwamba hawakufanya kampeni awali. Wameendelea kufanya mikutano mikubwa nchi mzima huku wakitumia kampeni hizo kukutana na viongozi na watu wengine wenye ushawishi kwa maeneo husika ili kuongea nao kwa ajili ya kuwatafutia kura. Kwa upande wa pili Raila Odinga na NASA wamekuwa wakisusua kufanya kampeni pamoja na kuchangisha fedha za kampeni toka kwa mashabiki wao. Raila alipoulizwa kuhusu hili alidai kuwa kampeni zilishakwisha toka kabla ya Uchaguzi wa awali.

Sasa ukichukua hayo mambo matano ni dhahiri shahiri kuwa this time Uhuru Kenyatta atashinda kwa margin kubwa sana hadi Raila na NASA hawataamini. Last time Uhuru Kenyatta alishinda kwa tofauti ya kura takribani 1.5M. This time around inaweza gonga 3 Millions. Na ushindi watakaopata uhuruto hakika utamuachia Raila kovu ambalo hatalisahau kamwe katika maisha yake ya siasa.

Karibuni kwa michango. Naomba kuwasilisha.

Asanteni sana
 
Umesema ukweli kabisa na inadhihirisha unafuatilia siasa za Kenya kwa uzuri na unaelewa. This time Hon Raila hana kitu uwanjani yaani atapata kifo cha mende! Ikumbukwe ni mara ya tano kupigwa chini. Raila kabaki na ngome mbili tu(nasa strongholds) Kibra na Nyanza excluding Nyamira na sehemu kadhaa kule Migori kwani Pwani kwa Hon Joho zinaanza kupungia kwa sababu ya viongozi kadha kama gavana Mrutu amerudi kwa Uhuru,Jubilee.
 
Pia kuna tetesi kwamba kambi ya Raila haina pesa ya kutosha kufanya kampeni kama awali,

Kuna kipindi kalonzo musyoka alienda Uganda akapata usumbufu sana airport Nairobi,inadaiwa alikuwa anafata hela kwa museveni,sijui kama alipata na kama alipata sijui kama ni za kutosha

Nadhani jubilee wamedhibiti funding ya Raila na pia wafanyabiashara wanaompa hela Raila wameshasoma mchezo kwamba wanawekeza kwenye hamna

Pia Raila anatumia muda mwingi kulalamika na jubilee wanamchezeshea hukohuko na kumuondoa kwenye kampeni,muda wote anaimba IEBC wakati wenzie wanachanja mbuga kwenye kampeni

Raila kwisha kazi
 
Na nyongeza kwa hili, Kalonzo Musyoka wanamuita ‘flower girl’ wa Mhe Raila kwa sababu ya kubeba bakuli la kuombea michango kutoka kwa slams za Kibra na wachache wengine. Akamba wanasema mtoto wao kauziwa mbuzi kwenye gunia kwani kama Kalonzo angaliwa na umoja na Jubilee angaliweza kupata nafasi ya Uwaziri Mkuu baada ya kukubaliana na Uhuru kwa ukubwa wao bungeni wangeweza mara moja kubadilisha vitabu vya sheria na kuunda nafasi lakini kwa bahati mbaya sana bado anazidi kurukakura barabarani na Raila na anaweza kuishia ICC kama raia kwenye ngome zao Kisumu na Kibra wataendelea kufa wakati sehemu nyingine zote Kenya ni safi. Kumbuka 2007 ni hivohivo Baba wa vitendawili aliwategea Uhuru na Ruto na wakanaswa na ICC this time Kalonzo, Mudavadi na Raila watanaswa kwani Jubilee hawana masharti yeyote, wao wanakampeni tu.
 
Back
Top Bottom