round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 668
- 2,277
Kama ningekuwa sijafanana na hawa watoto ningeenda kupima dna, maana ningehisi nimepigwa
Wote ni wavulana, wa kwanza tupo la saba huyu mwengine yupo la sita
Kuna muda mpaka watu wanachanganya wanahisi mdogo ndio mkubwa na mkubwa ndio mdogo.
Pamoja na urafiki wao mkubwa na kulala chumba kimoja bado sielewi
Mtoto wa kwanza sio jasiri, ni rahisi kutishika, hajiamini, mwaka huu amewahi kukimbizwa na jogoo kwa uoga.
Mdogo wake ni jasiri, nishawai kuitwa kesi katoa kichapo kwa mtu aliemzidi madarasa mawili, wazazi wa pande mbili tulibaki kushangaana tu.
Mtoto wa kwanza hajiongezi, ni wa kusubiria kuambiwa fanya hiki au asubirie afanyiwe, huyu wa pili vitu vingi anajiongeza ni rahisi kufundishika.
Mtoto wa kwanza ana uwajibikaji mdogo, mtoto wa pili yupo responsible sana na ni mtunzaji mzuri wa vitu, mfano niliwahi kununua flash zaidi ya mbili nikampa huyo mtoto mkubwa zikapotea, siku hizi hilo jukumu nimempa mdogo wake
Mtoto wa kwanza anapenda kuangalia Tv, kucheza games, kuangalia mziki, mambo ya kidijitali, Huyu wa pili anapenda kucheza mpira, anapenda ku hang out nje na marafiki majirani, shuleni kwao wamenitumia barua kuniomba nimwandae kwajili ya sikukuu ya vipaji
Sehemu ambayo mtoto wa kwanza tupo vizuri labda ni darasani, ni kipanga kitupu, nafasi zake ni 1 au 2, huyu mdogo wake ni nafasi za 10 hadi 15, wanasoma shule moja, madarasa yao huwa na wanafunzi 40 hadi 50