simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,418
- 9,209
Taarifa ya zamani (2007). Lengo lako nini hasa?
Taarifa ya zamani (2007). Lengo lako nini hasa?
Yaani ktk njia za mashindano ya magari watembea kwa miguu wanakatisha barabara?Yes, ajali imetokea na imethibitishwa na Daktari wa mashindano hayo DK. Karrim Zam.
Imetokea katika Kijiji cha Dongwe Mkoa wa Kusini Unguja wakati akiwa kasi Khalid alijaribu kupunguza mwendo kwa kuwakwepa watoto waliokuwa njiani na kujikuta akipinduka. na alipasuka kichwa na kusababishwa na kutoka damu nyingi, wanasema imetokea saa 3:45 asubuhi wakati Yussuf akijaribu kunusuru maisha ya watoto waliokuwa wakikata njia kwa kupunguza mwendo lakini kwa bahati mbaya gari lake likapinduka.
marehemu tayari alikuwa ameshatumia kilomita 26 tangu kuanza kwa kituo cha kwanza katika hoteli ya Zamani Kempiski iliyopo Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Msaidizi wake Raia wa Uganda Moses Matovu, hajapata madhara makubwa lakini alionekana kuchanganyikiwa kutokana na ajali hiyo.
Hili ni tukio la pili la madereva wa mbio za magari kupoteza maisha tangu yalipoanza Kisiwani hapa ambapo Nassir Khan alifariki dunia mwaka jana wakati wa mashindano kama hayo.