Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Zitto anaonekana kuwa biashara nzuri ya magazeti siku hizi mpaka yale ya udaku
 
Mtei hajakosea ni ukweli mtupu. na zito huo urahisi hapati..wala hatuchagui raisi muislamu..2015 ni mkristo..ndo mpunguze kuchaguana kwa kuangalia vigezo vya dini watu wenyewe hata credentions hawana lakini kwenye tume wapo..kuleana leana tu..ili mradi..sasa zanzibari kaeneo kadogo hivyo watu 15 wote hao wa nini..hata kama ni nchi kamili..muda wa kuanza kulalamikia kuhusu zanzibar umeshapita miaka 50 inabidi kusiwe hata na rais huko zanzibar..tamaa tu ya madaraka...serikali mbili za nini..kuongeza gharama tu kwa walipa kodi..Tanzania inapaswa kuwa nchi MOJA yenye serikali MOJA na sio kutupotezea wakati hapa.. marekani yenyewe taifa kubwa hapa duniani ni muunganiko wa nchi zaidi ya 52 na serikali ni moja iweje sisi maskini tunaotaka maendeleo tunakuwa na muungano wenye serikali mbili..tuwe wakweli tuache porojo..nchi nyingine zinasonga mbele tu sisi tumekalia maneno maneno , wanawake na bia tu..Nchi ya Ajabu sana hii..watu wanakosa maadili..na kuwaza mambo ya maendeleo..uvivu wa kukalia siasa, sijui huyo muislamu..huyu mkristo..viongozi wenyewe wamelewa kwa huo upuuzi..watu wenye tija pekee ndio wanaopaswa kuingia katika hiyo tume..nashangaa watumakini kabisa wameachwa wanachaguliwa watu wa ajabu ajabu tu, kisa kiongozi muislamu, na nyie ndugu zetu waislamu muache kulia lia kila siku na kudai mnaonewa, nendeni shule sio madrasa, mpate elimu ya kutosha na mfanye kazi sio kukaa kucheza bao kila siku na kutegemea maendeleo yatakuja kwa kulia lia.
 
ZITTO, tafadhali acha jazba za kidini, uwe na adabu! Wewe wamwonaje Mtei? Ukweli unakuuma sio? Zanzibar hakuna wakristo? Inakuwaje wajumbe wote 15 wawe waislamu? Wewe inakupendeza hiyo? Tunamheshimu sana mzee Mtei sisi, tumechoka pamoja na unafiki wako sepa, tunakuvumilia kwa mengi, kwa dharau hizi huvumiliki tena! Rais akikosea tushangilie?

Sasa wewe ulitaka rais aanze kutafuta mkristo wa kutoka Zanzibar amuweke kwenye tume huoni huo kama ndio udini wenyewe?

Swala lilikuwa sio kupata watu wa dini fulani , malengo ni kupata watu watakaosaidia kusimamia mchakato wa katiba mpya na rais aliweka wazi watu watume majina, kwanini nyie hamkutafuta majina ya wakristo wa Zanzibar mkampelekea rais? Mbona jina la Mwesiga Baregu mlipeleka?

Sasa hapa kama unavyoona swala la dini halipo na halisaidii.
 
Je alichosema ni cha kweli... Maybe (Mtei shouldn't have said what he said)...

Je should Zitto have said commented on this.....
Absolutely Not (Sometimes Busara na diplomacy inatakiwa) angempuuza tu au angesema points zake bila kuonyesha kwamba kuna any attack..., sometimes ni vema kuangalia the whole war na sio concentrating on winning battles
 
Nioneshe popote niliponukuliwa kusema unavyosema hapa.

Sijawahi kumjibu Mtei moja kwa moja hata siku moja. Kwenye suala hili msimamo wangu niliuweka wazi hat kabla Mtei Hajasema.
Walioandika wameunganisha tu tweets zangu na kauli ya Mtei ambayo siiungi mkono hata kidogo. Mzee was mistaken.
Tume ya Katiba imeteuliwa kwa mujibu wa sheria. Haina Udini. Ina wajumbe ninaowaheshimu sana. Twende tukatoe maoni. Tuache maneno yasiyo na maana yeyote.
afadhali umeingia tuweze kuchangia sasa.MZEE NI KWELI AMEKOSEA. Hayo majina ya kiarabu(kiislamu) na majina ya kirumi(roma/ulaya) hayana nafasi kabisa katika tume ya katiba. kiuhalisia zanzibar idadi kubwa ya wananchi wake wanaamini katika uislamu lakini sio tija hapa. JE WATEULE HAO HAWAWEZI KAZI? TUNATAKA UWIANO WA DINI AU UMAKINI WA KUTUONGOZA? Ninakuunga mkono, Mzee wetu hakupaswa kusema hilo. Hata wewe hukupaswa kumjibu Baba kupitia magazeti. Ungemtafuta ukamweleza" Baba hapa hapana".
 
Ninyi kaeni mjiridhishe kwa kutetea upuuzi.........
Wenye akili zao ndani ya CDM walikaa kama kamati na kutathimini tamko la huyu Babu na athari zake kwa chama na jamii....
Wakabaini lina mushkeri mkubwa sana usiofuata misingi yetu kama taifa ya kuangalia mambo kwa jicho la kidini na kikanda
Na hatimaye wakaja na tamko hili haraka sana kumnawa asihusishwe na chama kwa aliyoyatamka
JIULIZE..... ni lini umewahi kusikia CDM inatoa tamko kutaka alichotamka kiongozi wake kisihusishwe na chama.....zingatia kwamba Mtei ni muasisi na ana influence kubwa ndani ya chama lakini still viongozi wameona kuna haja ya kuipotezea kwa kutoa tamko rasmi dhidi ya maoni yake?

Mnyika hajakanusha kama mzee Mtei kasema au la. analosema Mnyika ni kuwa mwanachma au hat kiongozi anaweza kusema lake. na kwamba bado wanafanya utafiti lakini si katika udini, maana udini hauna nafasi. Mtei mawazo yake mfilisi na anadhani tunataka kuadiri biblia au kuruan. Wanahitajika watu makini, wenye busara, wazalendo, wanaoipenda nchi yao na hata waikwa wote ni wakristo au waislamu haijarishi ni watu makini. Hata wangekuwa wote ni Wahaya maadamu wan busara na uwezo unahitaji nini, makanjanja mradi uwiani. Mzee hiyo akili imechoka na i-RIP
 
Hivi bado kuna watu huwa mnashangaa kauli za hili jamaa bishi( zitto)? Jamaa halishauriki na siku zote limekuwa likiropoka 2 kwa kudhani ni sifa, mzee mtei kasema kweli kabisa kwamba hawa watu wa makka ni wengi kwenye tume, sema 2 wakristo nyie huwa ni waoga sana kuongea ukweli pale ambapo haki inaonekana haitendeki, hivi ni matamko mangapi ya Bakwata ambayo huwa wanayatoa tena yenye udini na hata pale moro mjini huwa kuna maredio fm ya kiislamu na usiku kucha huwa yanahubiri ubaguzi wa kidini lakini Zitto kakaa kimya. Msimuonee mzee wa watu bure kwani kasema ukweli lakini watu wameyakuza mambo. KUBISHANA NA ZITTO NI SAWA NA KUJARIBU KUHAMISHA MLIMA KILIMANJARO TOKA MOSHI MPAKA DAR KAWANI JAMAA HUYU NI MUHA SO HUWA HAKUBALI KUSHINDWA KITU.
 
maneno ya Mtei yana ukweli mkubwa sana. sioni sababu ya kuwaweka waislam wengi kiasi kile, kwan zanzibar hakuna wakristo? au wakristo walioko kule wanababuliwa kwenye uongozi hadi kuwa vile? palitakiwa pawe na balance, nchi hii ya kwetu sote, ukilewa watu wa upande mmoja katiba italalia zaidi upande wao, hasa ikizingatia rais mwenyewe ni muislam, unafikiri watu watamueleweje? au ndo shukrani yake kwasababu anaona hii ndo term yake ya mwisho?
 
Zito anaweza akawa amesema ukweli kwa maoni ya watu wengi, lakini si kila ukweli unapaswa kusemwa kwa namna hii na kuwekwa hadharani. Huku ni kukosa adabu kwa hali ya juu kabisa. Ili unielewe, fikiria kwamba kuna ukweli juu ya baba au mama yako ambao watu wanaufahamu lakini ambao wewe hutapenda wauseme hadharani, japo ni ukweli.
Ukweli wa baba na mama vyumbani usiletwe hapa. Baba na mama yako (x) hawamhusu Y au z. Lakini kwa kiongozi wa jamii ya Mzee Mtei (kumbuka nimemwita Mzee nimempa hesihma yake) kuuzungumzia udini kwa maana ya uwiano wa kiuwakilishi unaleta maswali mengi. mzee amekosea. Kama alikengeuka Mzee Mkapa tukamwambia hapa mkuu umekosea na Vicent Nyerer hakuonekana mkosefu wa adabu tatizo liko wapi kwa Mtei.? Kesho atasema mbona hakuna wachaga kuna wazaramo tu nk nk. Tupitie umakini wa wateuliwa bila kujali imani zao za dini. wengine wana majina ya kiarabu lakini si waislamu, wanakunywa pombe, wanacheza kamari, wanasengenya na mwisho wanatafuna kitimoto.(samahani).
 
Tufikie mahali tupingane ki-staarabu..Sina tatizo la CDM kuona kwamba mawazo ya Mzee Muasisi wa CDM hayana nafasi kwenye chama na taifa kwa wakati huu tulionao....lakini natatizika iwapo mtu mzima anaambiwa "Kafilisika Kimawazo" - inawezekana ni uzeee au ugonjwa au uchakavu wa mawazo kutokana na akili kuzeeka- but to slap it on face sio desturi yetu ... Ndo maana wenzetu walio kwenye demokrasia zilizokomaa wana sema .. "it was a wrong choice of Words" au ' Kila Mtu ana uhuru kutoa mawazo yake kama alivyosema mzee Mtei" lakini sera za chama kwa nyakati hizi ni ....na kadhalika!!! Je Zitto hana wazazi au wazee ambao wakati mwingine wanamshauri mambo ambayo anayaona kabisa hayafai.. Na Je anawajibu. kama alivyo mjibu huyu mzee??? Tuwe na staha jamani... ndo maana wahenga walipomwona mfalme kakaa uchi aliambiawa 'Mfalme wangu kuna mdudu ana kunyemelea ebu sogea huku ili mradi ajikusanye na kukaa vizuri kujistiri!!!!
 
wala mzee Mtei hajafilisika kimawazo bali ametoa maoni yake jinsi aonavyo. hata mimi namuunga mkono kwanini waisalmu wawe wengi kuliko wakristo? je wanataka kutuletea mahakama ya kadhi iamue masuala yao kwa kutumia kodi zetu

Tume yenyewe kwa ujumla haiaminiki kwa sehemu kubwa, mm nikianza kuchambua watu mtachoka kwani wengi wao ni royal to the government

napisha wengine
 
Nadhani Mtei kakisema tu kile kilicho kwenye mioyo ya wana-CDM wengi. Kwa kweli waislamu hatuwaamini kabisa kwenye CHADEMA, hivyo tunahofu hawatasimamia masilahi yetu!
 
Zitto hana ubavu wowote wa kumwita Mzee MFILISI wa kimawazo. He hasn't reached even half way the Mzee has gone. Kakakurupuka vibaya katika hili.
 
Zitto hana ubavu wowote wa kumwita Mzee MFILISI wa kimawazo. He hasn't reached even half way the Mzee has gone. Kakakurupuka vibaya katika hili.

Sasa mtei naye anabusara gani zaidi ya UKABILA na UDINI ..nyama...fu zake
 
Zitto anaivuruga CDM, au chadema inamvuruga zitto?? Zitto anapanbana na maadui zake ndani ya chadema wasiotaka kuona chama kinatoka minoni mwa wenye malengo maalum!! Mtoeni zitto ili chama chenu kife ili tanzania iendelee kuwa na amani

Unaota ndoto za alinacha mwambie hata leo aondoke uone chama kinakufa, chadema ni movement sio mtu stupid
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom