ZITTO, tafadhali acha jazba za kidini, uwe na adabu! Wewe wamwonaje Mtei? Ukweli unakuuma sio? Zanzibar hakuna wakristo? Inakuwaje wajumbe wote 15 wawe waislamu? Wewe inakupendeza hiyo? Tunamheshimu sana mzee Mtei sisi, tumechoka pamoja na unafiki wako sepa, tunakuvumilia kwa mengi, kwa dharau hizi huvumiliki tena! Rais akikosea tushangilie?
afadhali umeingia tuweze kuchangia sasa.MZEE NI KWELI AMEKOSEA. Hayo majina ya kiarabu(kiislamu) na majina ya kirumi(roma/ulaya) hayana nafasi kabisa katika tume ya katiba. kiuhalisia zanzibar idadi kubwa ya wananchi wake wanaamini katika uislamu lakini sio tija hapa. JE WATEULE HAO HAWAWEZI KAZI? TUNATAKA UWIANO WA DINI AU UMAKINI WA KUTUONGOZA? Ninakuunga mkono, Mzee wetu hakupaswa kusema hilo. Hata wewe hukupaswa kumjibu Baba kupitia magazeti. Ungemtafuta ukamweleza" Baba hapa hapana".Nioneshe popote niliponukuliwa kusema unavyosema hapa.
Sijawahi kumjibu Mtei moja kwa moja hata siku moja. Kwenye suala hili msimamo wangu niliuweka wazi hat kabla Mtei Hajasema.
Walioandika wameunganisha tu tweets zangu na kauli ya Mtei ambayo siiungi mkono hata kidogo. Mzee was mistaken.
Tume ya Katiba imeteuliwa kwa mujibu wa sheria. Haina Udini. Ina wajumbe ninaowaheshimu sana. Twende tukatoe maoni. Tuache maneno yasiyo na maana yeyote.
Ninyi kaeni mjiridhishe kwa kutetea upuuzi.........
Wenye akili zao ndani ya CDM walikaa kama kamati na kutathimini tamko la huyu Babu na athari zake kwa chama na jamii....
Wakabaini lina mushkeri mkubwa sana usiofuata misingi yetu kama taifa ya kuangalia mambo kwa jicho la kidini na kikanda
Na hatimaye wakaja na tamko hili haraka sana kumnawa asihusishwe na chama kwa aliyoyatamka
JIULIZE..... ni lini umewahi kusikia CDM inatoa tamko kutaka alichotamka kiongozi wake kisihusishwe na chama.....zingatia kwamba Mtei ni muasisi na ana influence kubwa ndani ya chama lakini still viongozi wameona kuna haja ya kuipotezea kwa kutoa tamko rasmi dhidi ya maoni yake?
He !!!! Makubwa jamani muacheni Zitto apumzike!!.
Ukweli wa baba na mama vyumbani usiletwe hapa. Baba na mama yako (x) hawamhusu Y au z. Lakini kwa kiongozi wa jamii ya Mzee Mtei (kumbuka nimemwita Mzee nimempa hesihma yake) kuuzungumzia udini kwa maana ya uwiano wa kiuwakilishi unaleta maswali mengi. mzee amekosea. Kama alikengeuka Mzee Mkapa tukamwambia hapa mkuu umekosea na Vicent Nyerer hakuonekana mkosefu wa adabu tatizo liko wapi kwa Mtei.? Kesho atasema mbona hakuna wachaga kuna wazaramo tu nk nk. Tupitie umakini wa wateuliwa bila kujali imani zao za dini. wengine wana majina ya kiarabu lakini si waislamu, wanakunywa pombe, wanacheza kamari, wanasengenya na mwisho wanatafuna kitimoto.(samahani).Zito anaweza akawa amesema ukweli kwa maoni ya watu wengi, lakini si kila ukweli unapaswa kusemwa kwa namna hii na kuwekwa hadharani. Huku ni kukosa adabu kwa hali ya juu kabisa. Ili unielewe, fikiria kwamba kuna ukweli juu ya baba au mama yako ambao watu wanaufahamu lakini ambao wewe hutapenda wauseme hadharani, japo ni ukweli.
Zitto hana ubavu wowote wa kumwita Mzee MFILISI wa kimawazo. He hasn't reached even half way the Mzee has gone. Kakakurupuka vibaya katika hili.
Zitto anaivuruga CDM, au chadema inamvuruga zitto?? Zitto anapanbana na maadui zake ndani ya chadema wasiotaka kuona chama kinatoka minoni mwa wenye malengo maalum!! Mtoeni zitto ili chama chenu kife ili tanzania iendelee kuwa na amani