TANZIA Mtanzania Mansoor Daya Afariki Dunia, alianzisha kiwanda cha kwanza cha Madawa Afrika Mashariki 1962

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,507
8,136
Mansoor Daya.jpeg

Mtanzania Mansoor Daya amefariki dunia jijini Dar es Salaam. Daya alikuwa mtu wa kwanza nchini kufungua kiwanda cha madawa Tanzania na Afrika Mashariki mwaka 1962 akianza kwa kuziuzia nchi jirani na baadae akaanza kuuza kwenye soko la ndani.

Mpaka anafariki dunia alikuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya 'Mansoor Daya Chemicals Limited. Kiwanda chake kimekuwa kinazalisha madawa kwa miaka 60 na sasa kina uwezo wa kuzalisha tembe milioni 3 kwa shift moja.

Wateja wake wakubwa ni MSD, mahospitali na cliniki mbalimbali Tanzania na kinachagiza juhudi za kufikia mpango wa Serikali kuhakikisha Tanzania inaagiza chini ya 50% ya dawa zote zinazotumika nchini kufikia mwaka 2030.
 
Back
Top Bottom