Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

Bilikundi.jpg

Tunachokijua
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

images

Picha: Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.
Sababu ya Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile undugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.

Pamoja na kuwepo muungano lakini Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwenye kila jambo bali kwa baadhi ya mambo tu, hivyo kuwepo kwa mambo yahusuyo Muungano na ambayo hayahusu Muungano hivyo kila upande huyashughulikia bila kuhusisha Muungano.

Je, Mtu wa Tanzania bara anaruhusiwa kuendesha gari Zanzibar kwa kutumia leseni yake aliyopewa na TRA?

JamiiForums Imezungumza na Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'azi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ambaye amekiri kuwa:

"Ni kweli mtu hawezi kutumia leseni yake aliyopewa na mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) kwasababu Mamlaka ya utoaji wa leseni sio jambo la kimuungano hivyo Mamlaka za utoaji wa Leseni kati ya Tanzania bara na Zanzibar zipo tofauti.

Tanzania bara Mamlaka inayotoa leseni ni TRA, baada ya kupata uthibitisho kutoka jeshi la Polisi kuwa mtu huyo amesomea udereva na amepitia mitihani ya polisi au utahini wa polisi na kupewa hati maalum ya kufaulu na kwamba mtu huyo anatakiwa kupatiwa daraja fulani la leseni.

Baada ya TRA kupokea taarifa ya uthibitisho kutoka Polisi hutoa leseni kulingana na maelekezo ya jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani.

Lakini Zanzibar wao wana mamlaka yao ya utoaji leseni ambayo ni tofauti na huku Bara na ndio maana wameweka utaratibu mtu akitoka huku kwenda kule ataomba kibali maalum kwa kuwa mamlaka ya utoaji leseni siyo jambo la kimuungano.

Hivyo
mtu akienda Zanzibar ataomba kibali maalum na vivyo ivyo mtu akitoka Zanzibar kuja bara ataomba kibali maalum ili aweze kuendesha gari".

Pia, JamiiForums imezungumza na Abubakar Nassor Ali Mkuu wa Divisheni ya Upasishaji Madereva, Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani Zanzibar, ambaye amesema kuwa:

"Kimsingi tunapozungumzia suala la usafirishaji, Tanzania tuna sheria 2 tofauti, zikiwa na lengo moja la udhibiti wa usalama barabarani. Huko bara mna sheria ile namba 30, ya mwaka 1973 (Road Traffic Act) lakini Zanzibar tuna sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ivyo ni sheria 2 tofauti ila lengo ni moja la shughuli za usafirishaji.Na hii kutokana na jambo hili kutokuwa la kimuunano.

Kwa maana Zanzibar tuna sheria yetu, sheria hiyo ndio inashughulika na mambo mbalimbali ya leseni, na inamtaka dereva yeyote awe na leseni.

Sheria yetu inatuambia mtu yoyote ambaye atatoka nje ya nchi, inamtaka mwenye leseni ya udereva mbali na ile iliyotolewa na Msimamizi Mkuu wa usafiri barabarani( Mkurugenzi wa mamlaka na usalama Barabarani) kwenda kufanya jaribio au kuangalia afya au kufanya mtihani ili kupima uwezo wake wa uendeshaji chombo cha moto akiwa ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo mtu yoyote ambaye atakuwa na leseni ya nje ya nchi( nje ya nchi hapa ni pamoja na Tanzania bara)
anatakiwa kukata permit, kwa hiyo kwetu mtu yoyote ambaye atakuwa anatokea bara maana yake anatokea nje ya nchi, na anatakiwa kukata Permit (kibali maalum) ambapo kwa sasa gharama yake ni 15,000 ambayo hudumu kwa miezi 3.

Na kwa yule ambaye atakuwa anataka kuendelea kukaa Zanzibar kwa muda mrefu zaidi au kuweka makazi ya kudumu basi ana uwezo wa kubadilisha leseni yake, yaani atakata leseni ya huku Zanzibar,( hatubatilishi leseni ila atabaki nayo ya bara na atapewa nyingine ya huku baada ya kufuata taratibu za kuchukua leseni huku)

Mtu atakayekiuka sheria hii na kuendesha bila leseni atakuwa ametenda kosa, Kosa la mtu kuendesha bila leseni hapa ni kwa wageni wote ( nchi nyingine pamoja na wa bara) adhabu yake ni faini ya dola zisizopungua 50 ambapo kwa sasa ni sawa 116,500".

bilikundi-jpg.2703699
JamiiForums baada ya kusoma mambo yahusuyo muungano na kujiridhisha kuwa suala la usafirshaji si la kimuungano na kuzungumza na mamlaka za usafirishaji pande zote 2 za muungano ambao wamekiri mtu anayetoka upande 1 kwenda mwingine anatakiwa kukata kibali maalum ivyo imejiridhisha kuwa ni kweli Mtu wa Tanzania bara haruhusiwi kuendesha gari Zanzibar mpaka akate kibali maalum(permit)
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699

Mkuu Chachu

Pole sana mkuu, kweli kisu kikali kwa nguruwe.

Unajuwa sisi wazanzibari tukileta bidhaa za biashara huko tanganyika tunalazimika kulipia ushuru? Tunalipa ushuru kama zile bidhaa zimetoka katika nchi ya kigeni.

Muungani gani unaoutaka weye mkuu?

Tanzania gani tunayoishi hii, mbona mchele wa mbea ukija dar haulipiwi ushuru kwa sbabau umetoka mbea na umeletwa Dar?

Huu muungunano ni kiini macho tu. Tafuteni nchi yenu kwanza kabla kujadili muungano zaidi.
 
Asa ninyi ambao mna Nchi yenu mbona kama mwisho hapo nawe umelalamika kuwa mwalipishwa ushuru wa bidhaa zenu huku bara
 
Afukiri Mwamba Mwabukusi ask maliza la DP World kuokota bandarin zetu, tu muwezeshe aka challenge kero zo Muungano katini. Kipengele kimoja at a time.
 
Asa ninyi ambao mna Nchi yenu mbona kama mwisho hapo nawe umelalamika kuwa mwalipishwa ushuru wa bidhaa zenu huku bara

Mkuu Anyisille

Wazazibari tumo katika muungano na tanganyika kwa kulazimishwa tu. kila miaka mitano watanganyika wanaleta mapaka vifaru ili kuhakikisha muungano bandia unabaki. Hakuna mzanzibari yoyote anayetaka muungano. Nyie ni watu wengine na sie ni watu wengine kabisa. hakuna uhusiano wowote baina yetu zaidi ya kwamba niye ni binadamu na sie ni binadamu.
 
Mkuu Anyisille

Wazanizbari tumo katika muungano na tanganyika kwa kulazimishwa tu. kila miaka mitano watanganyika wanaleta mapaka vifaru ili kuhakikisha muungano bandia unabaki. Hakuna mzanzibari yoyote anayetaka muungano. Nyie ni watu wengine na sie ni watu wengine kabisa. hakuna uhusiano wowote baina yetu zaidi ya kwamba niye ni binadamu na sie ni binadamu.
Yep lakini sasa mwasubiri nini kujitoa wakati mna njia nyepesi???

Sina hakika kama mwalazimishwa au mnashindwa kwa sababu mna maslahi ambayo huwa mnajifanya hamuyaoni.

Samia Mzenji, Mwinyi Mzenji si ndiyo ilikuwa so simple tena na zile nyimbo zenu za tunataka Nchi yetu zingeshamiri uzuri

Wazenji MNA kaunafiki Fulani Fulani hivi.
 
HATUTAKI HUU MUUNGANO hauna faida kwetu
siku tukiamka wanzibar wafurumshwe humu ndiyo siku Muungano utavunjika
tuwatimue humu hakika itakuwa mwisho
hatuwezi kuona tunapitia haya kisa muungano feki usio na lolote kwetu!
Kila mtu arudi kwao
 
Marehemu Karume baada ya kushituka, marehemu Jumbe baada y akushituka, na Maalim Seif walijitahidi sana katika harakati za kuitowa zanzibar katika muungano, unaona watanganyika walivoing'ang'ania zanzibar.

Unafiki mkuu, ni mavazi ya wanasiasa, hata huko tanganyika ufukara wenu unatoka na unafiki mkubwa sana wa wanasiasa wenu.

Sisi tunaloomba kwamba nyie watanganyika mudai utaifa wenu, maana mpaka hivi ninavyondika nyie hamuna utaifa wetu. Tanzania si taifa ni muungano. kilichoungana ni nchi inaiyotwa zanzibar na ina serekali yake na nchi ilikuwa haijuilikani duniani. Narejea tena zanzibar imeungana na nchi isiyokuwepo duniani. nyie watanganyika hamuna nchi, mupo mupo munabutuwa burutwa tu na ccm . tafuteni nchi yenu kwanza.
 
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699
Huu muungano watanganyika tunajipendekeza sana Kwa wazenji
 
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
Umeongea madini matupu
 
Foxhound
Mkuu Mimi umenigusa hapa tu
"Mambo yanayohusu kodi (Zanzibar ni nchi)
Mambo yanayohusu maslahi (Zanzibar si nchi)"
 
HATUTAKI HUU MUUNGANO hauna faida kwetu
siku tukiamka wanzibar wafurumshwe humu ndiyo siku Muungano utavunjika
tuwatimue humu hakika itakuwa mwisho
hatuwezi kuona tunapitia haya kisa muungano feki usio na lolote kwetu!
Kila mtu arudi kwao
Siku huu Muungano utakapo vunjika. Hasara itakua kwa wananchi wa Zanzibar wa level ya kawaida.

Maana hakuna fursa watakamata hapa bara. Na waliopo hapa watatimuliwa.

Ndipo akili zitawakaa kua viongozi wao walikua wanawapotosha.

Ni ujinga kung'angania mipaka ilio wekwa na wakoloni inayo ounguza namna ya kujaminaa na majirani.

Ingekua sawa hata kama tungefungya mipaka yote ya EA kukawa na easy movement of people and goods.
 
Unapaswa ujibu kwanza swali ndipo unauliza swali lako jipya.

Kistaarabu ngoja nikujibu swali lako.

Leseni ya Zanzibar haiwezi kuruhusiwa bara sababu bara sio Zanzibar.

Naomba na wewe unijibu swali langu

Swali langu kwani Zanzibar sio sehemu mojawapo ya Tanzania ?
Pia watuambie leseni ya bara ina title ya Tanganyika au Jamhuri ya muungano wa Tanzania??
 
Nimeenda kwa mara ya kwanza Zanzibar last week, ovyo kabisa. Ni wabaguzi mno, maneno kama "we wa bara" na "waDanganyika" nimeyasikia sana.

Tuko nao kimwili tu ila kiakili na kiroho hawako nasi kabisa, kiufupi HAWATUTAKI. Tunafanana lugha na rangi tu ila sisi sio wamoja hata kidogo. Muungano uvunjwe ili uundwe upya ama uvunjwe mazima, the latter is more preferable.
Sasa kuambiwa we wa bara kumekuumiza nn aisee?
Mbona watu hmna hoja thabiti

Mm nimekaa sana tu bara mbona naona kawaida tu wakiniita mpemba

Mbona uko kwenu mnabaguana kwa makabila!

Unaongea nonsense kabisaaa
 
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699
Nikuulize kwani leseni ya Zanzibar inaruhusiwa bara?

Mda mwingine mlete hoja zenye mantiki sio upumbavu kama huu

Foolish kabisaaa
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom