Ze General
JF-Expert Member
- May 10, 2014
- 1,508
- 1,251
Nasikia bashite ametangulia arusha kwenda kutoa pole....sijui kama watamtangaza akitoa pole
Mungu wangu, mmhh!! Inauma sana.Nasikia ktk huo msiba kuna mama miezi kadhaa nyuma alimpoteza mumewe kwa ajali na hiyo ya jana ikaondoka na wanae wawili,hakuweza kuhimili nae kupata taarifa hizo akaaga dunia...kizazi cha mtu kimepotea,inasikitisha sana.
Serikali haiko na nia njema kumaliza tatizo la ajali sababu makosa ya magari imefanya kama chanzo kikuu cha mapato, hivyo wao hufurahia kuona ubovu wa na makosa mbalimbali ya barabarani yakiongezekafikirieni ndugu zangu kiwango cha faini wanazotupiga barabarani, tena siku hizi imefikia hatua ya kulazimisha makosa au kuvizia kwa madhumuni tu ya kupiga pesa, najiuliza hii pesa tunayotangaziwa inaingia kwa mamilioni inakwenda wapi!??? Tulitegemea ingewekezwa basi kwenye vifaa vya ukaguzi, Kama hilo halitoshi kila mwaka kuna NENDA KWA USALAMA, ambapo tunalipa hela bila ukaguzi wowote kufanyiika, kwa kifupi tunanunua sticker kubandika eti gari imeshakaguliwa!! ilihali hakuna ukaguzi wowote physical and expartly done, leo nashangaa vilio na rambirambi lakini hatujiulizi tumewekeza nini kwenye vyombo vya ukaguzi na usalama Wa vyombo vya barabarani?? Hivyo tusishangae ajali kama hizi zikitokea na haisaidii hata kama tutatawanya ma traffic njia zote, kama vyombo vyenyewe si salama kwa kuwa hakuna perfect road worthiness inspection inayofanyika ni kazi bure, Kama hapa traffic makao makuu hakuna, unategemea nini huko mikoani? Lakini buku 30,000 zinaingia kila uchao. Mungu ibariki Tanzania, walaze wanetu mahala pema peponi.Amen
Napenda kuwapongeza kwa uzalendo wenu wakuahirisha vipindi ili muwe pamoja na familia na watanzania walioondokewa na watoto wao wapendwa, kuna kitu cha kujifunza kutoka kwenu. UTU ni bora kuliko PESA.
Lengo ni kuungana na waombolezaji katika msiba wa wanafunzi 32 wa st, lucky vicent karatu Arusha
Inaumiza sana.Nasikia ktk huo msiba kuna mama miezi kadhaa nyuma alimpoteza mumewe kwa ajali na hiyo ya jana ikaondoka na wanae wawili,hakuweza kuhimili nae kupata taarifa hizo akaaga dunia...kizazi cha mtu kimepotea,inasikitisha sana.
Hivi waziri wa elimu yupo au?
Tusingeweza kuwasifia wakati ule walipokuwa wanategemea mawazo ya ziro brain.Afadhali mmeanza tena kuisifia clouds
Nipe procedure ya ku deleted na mimi ...niitendee hakiHii channel nisha ifuta kwenye king'amuzi changu
Sisi Kama WaTZ tumeridhishwa Na hatua hii ya kufuta vipindi Na kuungana kuomboleza wakati ambapo TV ya Taifa ikidili na mambo mengine,hivyo basi hayo ya matangazo na pesa za Ubani Anzisha ww Kituo chako cha Radio na TV halafu uweke hayo Masharti yakoJe matangazo ya biashara nayo wamezuia? iwapo wamezuia sababu ya maombolezo, nitawaunga mkono, vinginevyo fedha zitakazopatikana kutokana na matangazo basi zikasaidie kununua majaneza,sanda na ubani.