Waanze kusajili kile kikundi kinachojiita "chawa wa mama" yaani kuna mambo unafikiria ni vipi watu wazima wenye akili timamu wanaweza kukaa na kujadili ujinga kama huu!
 
Watwambie balaa la UMEME na MAJI Litamalizika lini na mwaka gani haya ndio mambo ya msingi .Hii nchi kuna Mawaziri na wabunge Bumbumbu sana kichwani hamna kitu .Naomba sana niwe Raisi .Waziri nakupa miezi 6 tu kama hudilivery out of the job.
 
Kuna group letu la WhatsApp la kutoana upwiru nalo inabidi tulisajili? Duh hii sasa imezidi
 
Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali pale Wizara ya Mambo ya Ndani mh Kihampa amevitaka vikundi vyote Vya Whatsapp kujisajili kwa mujibu wa sheria

Source: Nipashe
 
yajayo yanafurahisha .... kuelekea uchaguzi mkuu ni marufuku kujadili siasa kwenye makundi ya Whats-app
 
20240403_115209.jpg

Ni kwamba tumekosa vyanzo vipya vya mapato ama lengo ni nini?!!

Makundi ya UVCCM,CCM nchi nzima yatasajiliwa na kulipiwa 200,000?!!

Watu wanafunguaga group la mazishi ambapo huwa kwa siku 2-5 pia yasajiliwe kwanza kwa shs 200,000?!!

Wazazi wengine wana magroup ya shule kwa ajili ya updates za watoto,nayo yasajiliwe kwa shs 200,000?!!

Makundi ya dini yapo lukuki sana kwenye kukumbushana na kuhimizana kutenda mema kwa mujibu wa dini,dini kwa kawaida taasisi zake huwa hazilipi kodi,ila kwenye magroup ya WhatsApp napo walipie usajili?!

Mheshimiwa Rais, upumbavu huu nani kashauri huko serikalini?!!!
 
Back
Top Bottom