Msaada: Nataka kufungua mgahawa kwa ajili ya mabasi ya mkoani njia ya Mbeya - Dar

Habari,

Naomba ushauri, Nataka kufungua mgahawa wa kulisha mabasi kwa njia ya Dar - Mbeya, Nimeona kuna changamoto ya vyakula vibaya katika njia hii. Mtaji ninao 120milion, Nina migahawa ya kawaida (restaurant Arusha, Mwanza, Dar Es Salaam inayojulikana kwa jina la ifood hivyo nina uzoefu na biashara ya chakula)

Kuna mambo kadhaa nimesikia ningependa kujua/kusikia kutokakwenu kama ni ya kweli kabla sija invest pesa na muda

1. Je, kuna ukweli kwamba ukiwa unalisha mabasi ya mikoani basi faini zote za mabasi YANAYOKULA KWENYE HOTELI YAKO utazilipia wewe unayeletewa abiria mgahawani? Yani makubaliano ya wamiliki wa mabasi/madereva na wenye mighahawa ni hayo/

2. Je, natakiwa kuwalipa madereva kiasi cha shilingi elfu 20 kila wanapo niletea abiria?

Tafadhari tushauriane hapa,

Natanguliza shukrani.
...Mkuu, una migahawa dar, Arusha na Mwanza lakini unaomba Ushauri wa kufungua mgahawa njia ya Mbeya ??
Hio mingine uliifungisje??
Yote uliomba Ushauri kwanza ??

Ushauri Mkubwa Kwako utakuwa wa kukushauri usiombe Sana Ushauri Kwa Watu.
Usipende kutoa wazo lako Hadharani. Jitahidi kuchamngamka Mwenyewe. Wapo Watu wamelala tayari tayari kuchukua wazo la Mtu na kulifanyia Kazi haraka, Mengine yote watajua huko huko mbele ya safari !
Mpaka wewe Inakuja kulifanyia Kazi wazo lako, Unakuta Migahawa Kibao imeichalichangamkia wazo lako fasta !

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
....Hivi inatoka Dar kwenda Tanga au Dodoma au Iringa au Mtwara na Lindi kweli ni Lazima ule Njiani ?? Inatoka Kwako umekuls vyema Bado Unataka Kila gari linaposimama ule ? Masaa SITA au Saba TU huwezi kuvumilia , huku una pakiti zako mbili tatu za Karanga za kukaanga ama biskuti na Chupa ya Maji ?...

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Shukran sana mkuu, Hivi eneo kama confort kitonga si lishakufa? Panakodishwa pale au ndo bado mmiliki anakomaa nako?
Mita mia Tano kutoka comfort mbona unapata eneo zuri tuu...hope kile kitongoji chote kina maeneo na bei siyo kubwa....nunua eneo laki maana Wa-TZ wenye maeneo ni vigeugeu sana.....utashangaa unaletewa fitna
 
Habari,

Naomba ushauri, Nataka kufungua mgahawa wa kulisha mabasi kwa njia ya Dar - Mbeya, Nimeona kuna changamoto ya vyakula vibaya katika njia hii. Mtaji ninao 120milion, Nina migahawa ya kawaida (restaurant Arusha, Mwanza, Dar Es Salaam inayojulikana kwa jina la ifood hivyo nina uzoefu na biashara ya chakula)

Kuna mambo kadhaa nimesikia ningependa kujua/kusikia kutokakwenu kama ni ya kweli kabla sija invest pesa na muda

1. Je, kuna ukweli kwamba ukiwa unalisha mabasi ya mikoani basi faini zote za mabasi YANAYOKULA KWENYE HOTELI YAKO utazilipia wewe unayeletewa abiria mgahawani? Yani makubaliano ya wamiliki wa mabasi/madereva na wenye mighahawa ni hayo/

2. Je, natakiwa kuwalipa madereva kiasi cha shilingi elfu 20 kila wanapo niletea abiria?

Tafadhari tushauriane hapa,

Natanguliza shukrani.
Mi naomba kujua hiyo migahawa unaiendesha vipi ilhali ipo mikoa tofauti?

Maana ninavyowajua wabongo ufungue mgahawa mwanza wakati wewe unaishi dar watakuibia mpaka uombe poo!!

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom