Mpenzi wangu ameanza tabia ya kuzima simu usiku

Mabadiliko ya tabia katika mahusiani si kitu cha kupuuzia... Fuatilia nini kinapelekea afanye hivyo...

Ila ata mimi napendelea kuzima simu usiku, sipendi kusumbuliwa nikiwa nimelala... Ila hii tabia sio ya kuanza ghafra... Kuna kitu hapo
 
Mwache tu azime simu yake hiyo mie wangu alianza kuzima simu, wala hata sikupata mshipa wa kuuliza
Naona tena ameacha ila kwa vile ni simu yake no worries :):)
 
Nimeamua kumwambia ukweli afanye maisha yake maisha hayo ya kuzimiwa simu kipindi tunalala wakati mimi sinaga hiyo tabia wakati majuzi ananiambia kila mtu ashike simu yake ikabidi nistuke na haikuwahi kutokea kuniambia hivyo.

Nimeamua aende asinisumbue nishachoka.
kwani ya kwako hataki uzime???
 
wache azime ili mpate kualala maana akiwa anachati usiku nako ni shida ,
jema hakuna chini ya juwa
 
Sasa kwani akizima simu kunakuwa na tatizo gn...mimi naishi peke yangu na usiku nazima simu...sipendagi usumbufu mimi...kuna siku nimelala,mara saa nane usiku inaingia sms(siku hy niliiacha on)..kucheki ni mama lishe anayetuletea msosi,ameandika "hi" nikaichekiii,sikujibu nikaachana nayo..najiuliza ningekuwa nimeoa,mke wangu angeelewaje..saa nane usiku tunauziana chai??? Lkn huyo dada sina mazoea nae yyt mabaya,zaidi ya kumwambia "lete hiki au hiki"...sasa imagine nina mke na ameona vile ingetokea nini.kuzima simu kuna hepusha mengi
....huyo dada kiboko, alikuwa anataka kuweka pre-order ya chai asubuhi
 
Yani ww nyuzi zako zote hazina mantiki laiti hyo bwana wako angelijua kua unakujaga kumkejel uku jf kila kukicha sjui ingelikuaje.
uzi zilizopita zote ni iyo bwana tu malalamiko juu ya malalamiko,ivi unataka kunambia malalamiko yote ya nyuzi zilizopita ni za yuleyule bwana wako mmoja au unabwana wangapi ati dada!!mara sjui mpenzi wangu hataki tuachane,yani unaforce na unamtafutia sababu ndgndg,mara sjui inafaa kumforce mtu anioe,asaiv unasema anakuzimia simu yan hueleweki nduguu.Kaaa,ukiemdelea ivo hutopata mume mmoja wa kutulia nae.
Mana uyo mmoja tu anakushinda maskini ya mungu kila siku unaleta nyuzi mpya kwa kumjudgemhhhmmm.Yeye uko aliko hata ajui.
 
Utakuja kumpata wa kufanana naww kwa tabia nilizoziona kupitia hizo nyuzi zako za zaman na hii ya leo huna lolote umetudhalilisha sana wanawake yaan unamtafutia sababu mwanaume..............
 
Hukuwa na haja ya kuchukua uamuzi huo, dawa ya moto ni moto nawewe ungezima yako
 
Back
Top Bottom