Mpambe wa Rais Magufuli abadilishwe

Kuna uzi moja ulianzishwa kipindi cha nyuma ukimuongelea huyu mpambe. Nilimtetea kwa kiasi kikubwa kwa kuzingatia kwamba Rais Magufuli ni Rais ambaye yupo tofauti kabisa na marais waliomtangulia. Yeye hana utulivu, lolote wakati wowote anapoana anapenda kulifanya anafanya. Mfano, amewaona wanakwaya, huyoo anaenda kuimba nao, mfano amewaona wapiga ngoma, huyoo anaenda kupiga ngoma.

Huyu mpambe wake kwa muda wote ambao amekuwa na Rais ameshidwa kuendana naye, ana uzubaifu kwa kiasi fulani, au pengine Rais yupo phisical fit zaidi yake yeye. Pengine anachoka na speed ya Rais ya kazi kazi. Dom-Arusha-eco bank- uganda.

Mfano wa picha hii, huyu mlinzi wa uganda amechukua position yake ambayo kimsingi kama ana jambo baya lolote, hapo ni shida.

View attachment 346675

=====================
Kijana unaelekea hujui kazi za mpambe wa Rais,cheo alichonacho na protokali
Huwezi kuwa kanali ukawa legelege
Nafasi hiyo hawapewi tu watu kujuana lazima upimwe utimilifu
Kuhusu huyo mpambe wa kiganda kumfunika rais wetu na mwamvuli hivyo ndio protokali inataka
 
Mkuu kwamtoro itoshe tu kusema kwamba suala la ulinzi wa rais ni zaidi ya macho yako yanavoweza kuona wakati wa tukio lolote liwalo.
 
Dah haya ni matusi ,huyo jamaa Magufuli yuko physical fit kuliko yeye ? ,kwani mpaka anafikia level ya kuwa ADC vigezo alivyo pitia ni kuvunja biskuti kwa kuloweka kwenye chai ??
Huyo anachokizungumza hakukifikiria!
 
Back
Top Bottom