Mpaka sasa sijaona tofauti ya Kikwete na Magufuli

Utofauti kati ya Magu na Jk upo mkubwa. JK ni kiongozi mzuri sana, alikuwka anajua siasa za ndani na nje, alikuwa aniasikiliza ushauri anauchambua pia mbunifu. Mambo mengi anayofuatilia sasa Magu alianza nayo JK. Tatizo la JK hakuwa mfuatiliaji sana km Magufuli ambaye yuko 'man to man'. Magu ni Msimamizi mzuri anataka jambo analofuatilia alione linafika mwisho kitu ambacho ni kizuri kwa hapa tulipofikia ila sio mbunifu, kilichopangwa na akakiamini hawezi kubadilika, pia siasa za nje hazimudu hivyo zitamtesa kwenye uongozi wake.
 
Mtoa uzi mpaka sasa hujaona tofauti kweli au ni umevurugwa tuu akili, yaani hata tofauti ya majina yao pia umeshindwa kuiona, rangi za miili yao tuu ni tofauti
 
Kuna wana CCM na wapinzani wanachukulia kauli kama hizi zilizoletwa hapo juu kuwa zimeandikwa au zinaletwa na mpinzani. Ila mi naamini kwa asilimia kubwa zaidi huwa zinaandikwa na wana CCM. Sidhani kuwa wana CCM wote wanampenda Magufuli na kufurahia utendaji wake! Na pia maoni yangu kuhusu hilo wazo kuwa sio sahihi kuwafananisha hawa watu wawili. Magufuli yuko tofauti mno tena kwa mbali utendaji wake ni safi, nampa big up, anajitahidi niseme kwa kifupi.
Hivi kuna ccm kindakindaki atathubutu kumpenda Magufuli? Kasababisha jiji limeenda, maslah yao binafsi yanaelekea shimoni, watoto wao mbeleko imekatika, kampuni zao pale bandarini zinakufa kifo kibaya, mirija yao pale TRA inamalizika kukatika, sembe hailipi tena, mitandao ya fitina imekata network, shopping za dubai na amerika nazo zishaelekea qibra, tembo, twiga, nyani na kobe nao wamekosa visa, 10% ni chungu, UDC na URC inakubidi uwe bongo movie hata kama hupendi, STK, STL, SU hazionekan kwenye bar na kumbi za starehe, masomoni Malaysia na kwa obama shida tupu, DAWASCO na TANESCO wameondoa mitambo yao majumbani kwao....
CCM tunaowajua watampendea wapi Magufuli wakat walizoea vya kunyonga?
 
Kuna mambo wako tofauti - kwa mfano kudhibiti utumiaji mbaya wa rasilimali za taifa na ofisi za umma na binafsi, lakini mengine hawana tofauti kama mitizamo yao kwa swala la Zanzibar na Demokrasia kwa ujumla (Ubabe). Tutamfahamu vizuri pale atakaposhika hatamu za Chama!!!
 
toka serikali ya Mwinyi kwa mara ya nyingine nimelitumia bomba langu la mvua kwa maji ya DAWASCO, jambo ambalo hata serikali ya Mkapa halikuwezekana ila ndani ya siku chini ya 100 kwa Dr. Magu limewezekana
 
Blaza kumbe umetuma huku si ulituma kwny grupu ya wasap ukachambwa mbayaa hujakoma tuuu
 
Pole sana mkuu..vipi na nyie mlikuwa hamlipi kodi?? :D:D:D:D:D:D:D
Tulikuwa tunalipa .. Ila kumbe kulikuwa na wafanyakazi waliokuwa wanakosea ku ring zile efd machine.. Badala ya 10,000/= mtu ana bonyeza 1,000,000,000/= afu anatupa risiti.. Tra wakawa wanatudai mabilioni bosi akawa hawElewi.. Wakagoma kukaa chini ku settle wKawa wanataka rushwa ndefu.. Mshua akafunga. Kahamishia biashara zake kenya na south sudan. Bongo sisi si ndio wajanja
 
toka serikali ya Mwinyi kwa mara ya nyingine nimelitumia bomba langu la mvua kwa maji ya DAWASCO, jambo ambalo hata serikali ya Mkapa halikuwezekana ila ndani ya siku chini ya 100 kwa Dr. Magu limewezekana
Ila ujue serikali ya jk ndiyo ilianzisha mkakati wa kuleta maji dsm kwa hisani ya watu wa dsm
Cc faiza foxy
 
Ila ujue serikali ya jk ndiyo ilianzisha mkakati wa kuleta maji dsm kwa hisani ya watu wa dsm
Cc faiza foxy
maji yapi hayo mkuu Saint Ivuga, na sio kwamba labda nimebadilisha pipeline, nah!!! ila nilivyosikia tu kale katangazo kamepita nje kwangu, kale kanakosema...nanukuu "katika kutekeleza agizo la rais wetu Mh. JPM la kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi na salama, DAWASCO inawatangazia wateja wake kufanya marekebisho ya mabomba yao kutoka mfumo wa zamani kwenda mfumo mpya kwa sababu maji yataanza kutoka" mwisho wa kunukuu.....aaaah!! kesho yake tu maji hayo, 24-7 dadadek!!!
 
Kweli mkuu sasa hivi dawaaco ni 24/7... Na mambomba yamepasuka kibao angalia hizo bill zitakazokuja sasa..
 
toka serikali ya Mwinyi kwa mara ya nyingine nimelitumia bomba langu la mvua kwa maji ya DAWASCO, jambo ambalo hata serikali ya Mkapa halikuwezekana ila ndani ya siku chini ya 100 kwa Dr. Magu limewezekana
Unaishi sehem gani mkuu labda tujue sema ukwel maeneo ulipo
 
Ni kweli hakuna tofauti...wote ni viongozi, wote ni watanzania, wote ni wanaume na wote ni wanaccm...
 
Yaani wewe una matatizo sana. Ulitaka alipoingia tu mahakama iwe tayari? Hauoni wanafunz wa vyuo wanavyoprwa mikopo kwa wingi? Elimu bure kwa secondary
 
Back
Top Bottom