MOROGORO: Polisi inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za ubakaji na udhalilishaji wa mwanamke

anko Magu leta viwanda fasta...awa vijana wangekuwa na ajira zao viwandani huko wasingeweza kushawishika kushiriki ubedui kama huu.
 
sijali ninachojali ni kuwa nimesema ukweli

Ila hata ukweli nao unaweza ukawa ni uongo. Maana hata muongo anaposema uongo yy anafaham kbsa kuwa n uongo ila kwako inabaki imani inayokuaminisha kile ulchokisikia ni kweli.

Chunga sana unachokilisha akili yako. Akili ni kama ardhi ukipanda mahindi huwezi kuvuna mapapai.
Ukiiliasha akili yako ujinga na upumbavu utakuwa mjinga na mpumbavu na ukiilisha werevu utakuwa mwerevu

Chaguo ni lako
 
Mkuu acheni kuleta masuala ya dini kwenye sehemu ambayo ni uovu wa mtu binafsi mbona askofu juzi alipata kashfa ya kudate na wake za watu hakuna aliyesema dini ile inahalalisha vitendo viovu kama hivyo kupitia kwa viongoz wao wakiroho?sio ishu
 
Nilivyosikia msichana alikuwa hajaolewa, alikuwa anatoka na mume wa mtu..dem akawa ana jamaa mwingine behind mume wa mtu. So huyo mume wa mtu ndio ameplan yote hayo.
Ni vizuri ukashauri watu wote waache michepuko. Michepuko haina jinsia. Huyo mume ndio alitakiwa akitulize kwa mke wake.
Tunakuwaga wepesi sana wa kufanya maamuzi pasi kufikiri. Sasa ona huyu so called Mume wa mtu fedheha aliyomuachia mkewe na familia yake kwa ujumla. Utakuta jamaa lilikuwa linajidai lina wivu na mkewe, ukali kwa kwenda mbele kumbe liko busy na mchepuko!
 
Umeongea vyema il kajifunza kutofautisha "R na L" na "A na H" i.e. Sheria sio shelia, msamaha sio msamaa, hamjamfikiria sio amjamfikilia na mengine mengi, inatia uvivu kusoma
Nashukuru wewe ukuona uvivu kusoma ukagundua tofauti ya uandishi
 
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu kumi na mmoja kwa tuhuma za kumdhalilisha mwanamke mwenye umri wa miaka 21 kwa kumtishia kwa kisu,kumbaka na kusambaza picha za kudhalilisha za tukio hilo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao 11, ni pamoja na mmoja Idd Adam (32) mkazi wa Makambako mkoani Iringa,aliyehusika kumtishia kwa kisu ili abakwe na kumrekodi video binti huyo,na mtuhumiwa Zuberi Thabit (30) mkazi wa mbarali mkoa ni Mbeya aliyembaka binti huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Kamanda Mateo amesema watuhumiwa wengine tisa wakiwemo wanaume saba na wanawake wawili,wakazi wa dakawa mkoani Morogoro wanashikiliwa kwa tuhuma za kusambaza kwenye mitandao ya kijamii picha za utupu za tukio hilo la ukatili na udhalilishaji dhidi ya mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa ni mjamzito.

Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamepokea kwa hisia tofauti tukio hilo la ubakaji na udhalilishaji wakitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa,huku wengine wakishauri ndugu jamaa na marafiki kuwa karibu na binti huyo ili kumfariji na kumshauri awe mvumilivu katika wakati huu mgumu kwake .
Watuhumiwa wanyongwe ili liwe fundisho kwa wengine.
 
Back
Top Bottom