Morning Trumpet Azam TV 9 December: Mohamed Said na Historia ya Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,900
31,972
MORNING TRUMPET AZAM TV KESHO 9 DECEMBER: MOHAMED SAID NA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA

Kesho In Shaa Allah asubuhi saa moja na nusu nimelikwa kuzungumza kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Picha hiyo ni kipindi changu cha kwanza nilichofanya katika Morning Trumpet mwaka wa 2015.

1670510531115.png
 
Tunakutakia maandalizi mema na Mungu akuonhoze ukalifanikishe hilo! Lakini chondechonde kazungumze yaliyo ya Uhuru wetu tu!! Mambo ya dini waachie wengine!!!
 
Mazaya,
Umaarufu wangu hadi unaona naalikwa kwingi ni kutokana na kitabu nilichoandika: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 - 1968 the Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' (1998).

Katika kitabu hiki kuna historia ya jinsi Waislam walivyoongoza mapambano ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hiyo chondechonde kipi kinakutisha?

Picha hiyo hapo chini nikifanya mazungumzo na mwandishi wa gazeti la serikali Habari Leo Bi. Anna Mwikola.

Tunazungumza kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

View attachment 2440192View attachment 2440193
 
Namsikiliza Yericko Nyerere muda huu Star TV anasema kanisa katoliki lilimlipia Nyerere nauli kwenda UNO na nyumba ya TAA ilitolewa na muingereza kwa kina Abdulwahid Sykes ili waifanye kuwa makao makuu. Ya kweli haya ???? Au kijana kajituma kuja kuondoa ukweli wa historia ya Tanzania.
 
Iika...
Kuhusu historia ya safari ya Mwalimu Nyerere UNO February 1955 fedha zilichangwa na wanachama wa TANU.

Mkusanyaji wa fedha hizi alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) Iddi Faiz Mafongo ambae pia alikuwa Mweka Hazina wa TANU.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza kwa kirefu safari ya UNO ya Julius Nyerere.

Kuhusu ofisi ya African Association ilijengwa kwa kujitolea wanachama kati ya mwaka wa 1929 - 1933 ilipofunguliwa na Gavana Donald Cameron.

Haya pia nimeeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

Picha ya ufunguzi wa jengo hilo ipo katika kitabu cha Abdul Sykes na hiyo picha inatoka katika Maktaba ya Picha ya Sykes.

Hafla ya kumuaga Nyerere kwa safari hii ilifanyika kwenye jengo la Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika Stanley Street na New Street.
 
Mzee hapa Ndio unaharibu sasa, siyo lazima useme pesa zilikusanywa na Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika kulikuwa na haja gani ya kutaja hivyo wakati unafahamu fika huyo bwana alikuwa mweka Hazina wa TANU? Au siku hizi watu hawaruhusiwi kufanya kazi za dini na jamii
 
Labda nikupe historia ya Iddi Faiz Mafungo.

Yeye ni miongoni mwa watu wasiozidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo.

TANU kwa kutambua kuwa alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya wakamuomba awe pia Mweka Hazina wa TANU.

Kadi yake ya TANU ni no.24 na kadi no. 25 ni ya ndugu yake Iddi Tosiri na hawa wote walikuwa wanachama wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hawa ni ndugu na Sheik Mohamed Ramia wa Bagamoyo na ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kumjulisha kwake.

Najua unatabika kwa kuwa hukuwa unaijua historia ya TANU sasa unapoisoma historia hii ya uhuru unapata mshtuko na kujiuliza, ''Mbona historia inayosomeshwa shule na vyuoni ni nyingine?''
 
Mzee Mohamed Said
Allah akupe umri mrefu wenye kheri na wewe uzidi kutuelimisha.
 
Back
Top Bottom