Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,689
- 3,268
Huu uwanja ni moja ya sehemu hatari sana kwa maisha ya watanzania. Wakati wa mazishi ya JPM inasemekana watu arobaini walifariki kwa kukanyagana. Hatujui majeruhi walikuwa wangapi. Jana wakati wa mechi ya yanga inadaiwa kafa mmoja na majeruhi thelathini. Bado hapo ambao hupigwa na askari karibu kila tukio, hupigana wao kwa wao na wanaookota nk nk.
Sijui kama zipo, lakini uwanjani hapo zifungwe kamera za usalama na kama kuna mafunxo maalumu ya kulinda mahali penye umati polisi wapewe. Maana polisi nao hamna kitu kabisa, kuna siku uwanja fulani kulitokea kashkashi wao wakapiga mabonu ya machozi. Jambo kama lile lingeweza leta mkanyagano na vifo.
Uwanja wa taifa si sehemu salama. Si vyema kwenda mpaka watakapohakikisha kuna usalama wa kutosha.