Mnada: Njia mpya ya Utapeli, tujiepushe!

Unataka kusema,wale hawashtakiwi ukiwafkisha kwenye vyombo vya sheria.
Masharti ya mnada ni "kifaa kinauzwa kama kilivyo"wewe ukinunua bila ya kutest,ukienda kukuta hakifanyi kazi ni kosa lako kwa sababu umenunua kama kilivyo!
 
Habarini za muda huu ndugu zangu wanajamvi wa JF.

Ninapenda kuwapongeza wote mliofanikiwa kupewa pumzi na utambuzi kifikra mpaka leo,Ashukuriwe MwenyeEnzi Mungu

Napenda kuwa tahadharisha kuwa sasa kuna utapeli kupitia minada ya vitu mbalimbali ambayo mara nyingi hufanyika maeneo ya masoko.
Wezi hao huuza vitu mbalimbali km Electronic devices n.k,huku wakitangaza vitu hivyo ni Mali za waliotaifishwa au kufirisiwa kutokana na kushindindwa kurejesha mikopo yao,Hii si kweli!!!!Mtaibiwa!

Watu hao huuza vitu vibovu na ambavyo vimechoka kabisa ambavyo huwa vimefungwa vizuri kama vile ni vibya!Mfano;Personal computer (PC) huuzwa bila Charger(adapter) zake ili isiwe rahisi wewe mnunuaji kutaka kujaribu na kugundua mapema.!Pia wanakupatia mpka receipt japo Ina jina la uongo na TIN za uongo za Auction Mart fulani ili kukuaminisha, "Msikubari"!!

Mimi binafsi nilitapeliwa laki moja na nusu(150K) km bei ya manunuzi ya PC aina ya ACER.

Cha kushangaza nilienda kutaarifu kituo cha polisi ili wakawakate na kuwachukulia hatua lakini wakaonekana kutokujari huku wakinikejeri na kunibeza kuwa napenda vya being Rahisi ndio maana nimetapeliwa,Iliniuma sana na kutamani kuwaTusi!!!

Nawaonya ndugu zangu msikubari kununua vitu ktk minada hiyo,Mtaibiwa!!!!!

Nawasilisha!!!!!!!!!
cc Mh. Mwigulu Nchemba
 
Bado watu wataibiwa tu, unadhani ni rahisi hiyo elimu iwafikie watu wote nchi nzima?
miaka karibu minne iliyopita niliibiwa na hao hao kwa mtindo huo huo, wakaniuzia digital camera ya dizaini fulani amazing, kwa 60,000/- ile kamera, ilikuwa kama mdoli wa kuchezea watoto, japo ilikuwa kamera halisi, ila ilikuwa na uwezo mdodo kiasi kwamba hta memory card ya one Gb ilikuwa haiomi kwa maana ni kubwa kuliko divise husika!
nawalaani sana polisi kwa kukumbatia hawa majambazi wa aina yake!
Pole mkuu!yaani nilikwazika sana kutokana na majibu ya polisi.
Ila wengi wanaibiwa sana,sababu ni kukosa maarifa juu ya wizi huo

Sent from my TECNO M3 using JamiiForums mobile app
 
pole mkuu ila usipende mteremko...always ununue kitu kwa bei inayoendana na thamani yake...thamani ya kitu na bei yake vikiachana sana weka walakini...
 
Wanekuja mitaani wanauza flash Na makorokocho mengine,flash gb 64 elfu kumi brand sum sung duuuh nkawastukia.
 
Kuna wengine hua nawaona pale ilala boma wanauza simu,aina mbalimbali bei kuanzia 10,000 kuendelea lakn cm mbovu zote cha kushangaza raia wananunua
 
pole mkuu ila usipende mteremko...always ununue kitu kwa bei inayoendana na thamani yake...thamani ya kitu na bei yake vikiachana sana weka walakini...
unaweza kuweka walakini, lakini kwani hakuna vitu vya thamani vinavyouzwa bei ndogo?
mtu anaposema ni mnada, na yupo kati kati ya mji, anatangaza mji mzima, utaaminije kama anauza vitu bibovu kabla kujaibiwa au kusikia aliyeibiwa kama hivi?

hivi unaweza kusema wote wanaoibiwa kwa mtindo huo hawajitoshelezi kufikiri?

sema tu kwamba "mzigo wa mwenzio ni kanda la ukufi"

lakini hakuna sababu ya kumbeza mtu juu ya kitu kama hicho.
siku moja hudhulia pale uone kinachofanyika, ila uende kwa tahadhari, maana ninavyojua mimi mbinu za wizi wa wale jamaa pamoja na kuyajua haya usipokuwa makini utaibiwa na wewe!
 
mkuu kwa experience yangu vitu vya mteremko vingi ni vibovu au utapeli, halafu kitu kikiwa kizuri kweli na kina ubora na ni cha bei rahisi wanauziana wao kwa wao coz hata wao wanahitaji vitu kama hivyo usifikiri wao ndo hawana shida...ukiona vimefikia steji ya kuuzwa hadharani kwa bei rahisi asee pay maximum attention

mkuu kuna mdau alikuja kulalamika huku eti kupatana ni mtandao wa kitapeli katapeliwa hela, eti kaona tangazo limeandikwa LG home theata na tv yake inch 40 vyote kwa laki mbili jamaa akatuma hela ha ha haaa, sasa huyo alijitosheleza kufikiri kweli???
 
Benki huwa wanauza nyumba mbovu?

huwa hawauzi kwa mnada?

huwa wanauziana wao kwa wao?

huwa hawauzi vitu vingine zaid; ya nyumba?

jibu hayo [HASHTAG]#francoo1[/HASHTAG]:
 
Back
Top Bottom