Mkuu wa Wilaya ya Mafia: Watoto 15 wamelawitiwa na Ustadhi wa Madrasa Kisiwani Mafia

Heparin

JF-Expert Member
Sep 24, 2021
216
993
Your browser is not able to display this video.

Licha ya Serikali kupambana kupiga vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini bado Wananchi na wakaadhi wa Kisiwa cha Mafia baadhi yao wameonekana kutia pamba masikio na kupelekea kuongezeka kwa vitendo hivyo hasa kwa watoto wakiume

Akizungumza kwa hisia kali kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Kilindoni, Kitongoji cha Msufini, Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Ally Mangosongo ameleza tangu aanze kuhudumia Taifa kwa mara ya kwanza amekutana na wilaya inayo ongozo kwa vitendo vya ulawiti kwa watoto wakike na wakimue,ubakaji na mimba kwa wanafunzi hali ambayo inatishia usalama kwa watoto.

Aidha, Mangosongo ameeleza tayari wamemkamata Ostadh wa Madrasa amelewiti Watoto 15 na kesi nyengine zinaendelea kuchunguza huku akiwataka wazazi kushirikiana kuwalinda watoto wao.

Upande wake Zaynab Matitu Vullu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Pwani amemuomba Mkuu wa Wilaya Mafia kuangalia vyema ushahidi wa vitendo hivyo na kuwachukulia hatua kali wanaobainika ili kuwa funzo kwa wengine wenye tabia kama hizo.


====

Mafia nimekutana na changamoto ya Ulawiti na Ubakaji. Katika wilaya zote ambazo nimehudumu sijawahi kukutana na changamoto kubwa ya Ulawiti na Ubakaji kama ambavyo ipo Mafia.

Mwalimu mwingine wa Madrasa amelawiti watoto kama sita hivi.

Hapa tu kuna mwalimu wa madrasa amelawiti watoto 15, bora nieleze hapa wazazi mkiwa mnasikia, watoto wa kiume ni wengi kuliko watoto wa kike.

Mkuu wa wilaya ya Mafia Aziza Mangosongo ameyasema haya kwenye mkutano na wananchi wakati wa ziara ya viongozi wa UWT mkoa wa Pwani.

==== =========

Alichoandika Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu, Dk Dorothy Gwajima kuhusu suala hilo:

NAKUPONGEZA SANA MHE. DC MAFIA KWA KUWA MSTARI WA MBELE. PONGEZI KWA WAHE WAKUU WA MIKOA NA WILAYA ZOTE MLIO MSTARI WA MBELE....

Hii ndiyo maana ya madaraka kusogezwa karibu na wananchi kwamba, ofisi ya mkuu wa wilaya ni mamlaka yenye vyombo vyote na wizara zote chini yake. Lakini pia, wananchi wamewakilishwa na Wahe. Madiwani wao kupitia baraza la madiwani la halmashauri husika. Hivyo, ukiona wakuu wa wilaya wanakuwa kazini kama hivi kupambana na mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia na kwa watoto, unaona wazi kuwa, sasa ushindi unaenda kupatikana.

HONGERA SANA MHE... nitakuja kutembelea Mafia nikupe pongezi mubashara.....

ANGALIZO
Tukio hili kamwe lisihusishwe na Imani za Dini yoyote. Ukatili na uovu siyo suala la kidini au Imani ya mtu fulani bali ni mambo ya watu tu wasio mhifadhi Mwenyezi Mungu ndani ya mioyo yao walio kwenye Dini zote ila Mungu hayuko ndani yao. Kwenye Kila Dini na Kila Imani watu wa aina hii wapo hivyoz tuwe macho...

Pia soma
~ Zanzibar: Nani anamlinda Ustadhi wa Madrasa anayedaiwa kumbaka na kumpa ujauzito binti wa Miaka 16?
~ Matukio ya Ukatili wa Kijinsia yaripotiwa kuongezeka Visiwani Zanzibar
 
Hao kumitano ñi waliosema je ameshalawiti intake ngapi za wanafunzi yawezeka kashatengeneza machoko hata elfumoja maana hutujui alianza lini na kashawaliti wangapi waliopita mikonini mwake
 
Sasa kama dini iliyoeenea sana ni ile ya madrasa unadhani kuna maadili na hofu gani kule? Dini yao imeshindwa kuzuia uovu mioyoni mwao wanafanya uovu bila hata mswalie mtume, hawana dhamiri ya kuwashitaki kuogopa dhambi kwa hofu ya kumkosea Mungu. Allah wanamtaja lakini hawana hofu naye uovu umewajaa wanahitaji ukombozi wazaliwe upya huko mafia kunako na hiyo dini kwa wingi
 
Shehk FaizaFoxy umepotelea wapi? mawazo yako yanahitajika hapa.
 
baada ya mda mrefu kuuliza kisiwa cha mafia naona wametuma salamu JF .
 
Dah asee ni hatari sana.
Nchi hii kesi hizi zimekuwa nyingi sana.
Rafiki yangu mmoja mwanasheria mwanafunzi anasema alipokwenda field mwezi Dec 2023 katika Mahakma Moja mikoa ya Kaskazini. Alishangaa kukuta mamia ya majalada watoto wa kiume wamelawitiwa. Anasema pengine kesi za ulawiti zimejaa mle kuliko hata kesi za mauwaji.
Hii inafikirisha. Hii hali ni mbaya kuliko kawaida.
Siku hizi naogopa hata kutembelea ndugu coz inawezekana muda wote wakawa na hofu juu ya watoto wao na mimi
 
Ushirikina kabisa hata kuna bibi juzi hapa alikuwa anamlilia makonda ni mambo ya ovyo sana ...Tatizo la serikali mtu anaachiwa anazurura anaweza asipewa hukumu .

Hapo wamemuachia sana , wampe kifungo cha maisha na fidia juu.
 
Cc adriz Accumen Mo Adiosamigo ielewemitaa mjingamimi Mamlukii hydroxo
 
Mkuu wa wilaya apewe ushirikiano.

Uovu kama huo si wa kunyamaziwa!
 
Wao watasema ni Papa Francisi kaleta Ushoga.

Wafrika ni watu wajinga sana. Uharifu wanafanya wao kwa mikono yao lakini hawaachi kusingizia Wazungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…