Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 213
- 966
Licha ya Serikali kupambana kupiga vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini bado Wananchi na wakaadhi wa Kisiwa cha Mafia baadhi yao wameonekana kutia pamba masikio na kupelekea kuongezeka kwa vitendo hivyo hasa kwa watoto wakiume
Akizungumza kwa hisia kali kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Kilindoni, Kitongoji cha Msufini, Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Ally Mangosongo ameleza tangu aanze kuhudumia Taifa kwa mara ya kwanza amekutana na wilaya inayo ongozo kwa vitendo vya ulawiti kwa watoto wakike na wakimue,ubakaji na mimba kwa wanafunzi hali ambayo inatishia usalama kwa watoto.
Aidha, Mangosongo ameeleza tayari wamemkamata Ostadh wa Madrasa amelewiti Watoto 15 na kesi nyengine zinaendelea kuchunguza huku akiwataka wazazi kushirikiana kuwalinda watoto wao.
Upande wake Zaynab Matitu Vullu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Pwani amemuomba Mkuu wa Wilaya Mafia kuangalia vyema ushahidi wa vitendo hivyo na kuwachukulia hatua kali wanaobainika ili kuwa funzo kwa wengine wenye tabia kama hizo.
====
Mafia nimekutana na changamoto ya Ulawiti na Ubakaji. Katika wilaya zote ambazo nimehudumu sijawahi kukutana na changamoto kubwa ya Ulawiti na Ubakaji kama ambavyo ipo Mafia.
Mwalimu mwingine wa Madrasa amelawiti watoto kama sita hivi.
Hapa tu kuna mwalimu wa madrasa amelawiti watoto 15, bora nieleze hapa wazazi mkiwa mnasikia, watoto wa kiume ni wengi kuliko watoto wa kike.
Mkuu wa wilaya ya Mafia Aziza Mangosongo ameyasema haya kwenye mkutano na wananchi wakati wa ziara ya viongozi wa UWT mkoa wa Pwani.
==== =========
Alichoandika Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu, Dk Dorothy Gwajima kuhusu suala hilo:
NAKUPONGEZA SANA MHE. DC MAFIA KWA KUWA MSTARI WA MBELE. PONGEZI KWA WAHE WAKUU WA MIKOA NA WILAYA ZOTE MLIO MSTARI WA MBELE....
Hii ndiyo maana ya madaraka kusogezwa karibu na wananchi kwamba, ofisi ya mkuu wa wilaya ni mamlaka yenye vyombo vyote na wizara zote chini yake. Lakini pia, wananchi wamewakilishwa na Wahe. Madiwani wao kupitia baraza la madiwani la halmashauri husika. Hivyo, ukiona wakuu wa wilaya wanakuwa kazini kama hivi kupambana na mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia na kwa watoto, unaona wazi kuwa, sasa ushindi unaenda kupatikana.
HONGERA SANA MHE... nitakuja kutembelea Mafia nikupe pongezi mubashara.....
ANGALIZO
Tukio hili kamwe lisihusishwe na Imani za Dini yoyote. Ukatili na uovu siyo suala la kidini au Imani ya mtu fulani bali ni mambo ya watu tu wasio mhifadhi Mwenyezi Mungu ndani ya mioyo yao walio kwenye Dini zote ila Mungu hayuko ndani yao. Kwenye Kila Dini na Kila Imani watu wa aina hii wapo hivyoz tuwe macho...
Pia soma
~ Zanzibar: Nani anamlinda Ustadhi wa Madrasa anayedaiwa kumbaka na kumpa ujauzito binti wa Miaka 16?
~ Matukio ya Ukatili wa Kijinsia yaripotiwa kuongezeka Visiwani Zanzibar