Kuelekea 2025 Mkutano wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa juu ya Sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea Chaguzi za 2024/2025 (siku ya pili)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,579
13,268
Leo ni Siku ya pili ambapo TCD inawakutanisha wadau katika Mkutano wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu ya sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wa Mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025.

Mkutano huu ulianza jana Mei 8 na unamalizika leo Mei 9, 2024.

Kujua yaliyojiri katika mkutano wa Mei 8, tafadhali soma hapa: Mkutano wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja wa Sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea Chaguzi za 2024/2025

UPDATES:

Isihaka Mchinjita, M/Mwenyekiti (Tanzania Bara) ACT-Wazalendo

Kwasababu tunasimamia kuwa uchaguzi huu usimamiwe na tume huru ya uchaguzi, mimi naona uchaguzi huu unaweza kusimamimwa na tume huru ya uchaguzi na sababu ni ileile kuwa yale mambo ya kuzingatia kile kilichopo nchini kwetu kuliko kile kilichopo katika nchi nyingine, kwasababu kuna nchi nyingine huu uchaguzi watu wanapiga kura na hakuna hata mawakala na matokeo yanatoka vizuri tu -aliyeshinda ameshinda! Hapa kwetu una mawakala, una msimamizi wa uchaguzi, una polisi ndani na kura zinaibiwa. Na wale wanaoenda kukamata kura feki wanakamatwa. Kwahiyo ndiyo statu tuliyokuwa nayo sisi. Kwahiyo, ili kuondoa hii nadhani ni muhimu na inawezakana kabisa kufanya hivyo.

Suala la uzalishajiwa karatasi za kura ni muhimu likawekwa kwenye sheria yetu.

Jambo lingine naomba nimalize. Mimi naona suala la daftari la kudumula wapiga kura linao uwezo wa ku-reflect vitongoji. Kwasababu tukikubaliana daftari liwe hivi, tunakubaliana pia kuwa liandikishwe upya. Tuliandikishe upya na liwe linaweza ku-reflect maeneo ambayo watu wanakaa. Kwahiyo ni jambo ambalo linawezekana.

Askofu Mwamakula
Mimi ningependa kujenga uelewa ambao huenda ukawa na faida zaidi. Prof. Kabudi ametoa hoja ambayo inatupeleka kwenye legitimacy (uhalali)…

Kwahiyo changamoto ninayoiona hapa, kama mmeandaa sheria na manataka iwe shirikishi, na ikubaliwe na watu wote, kabla haijaenda kwenye public (umma), tunawaita wale wadau wa kila upande kwamba tunaenda kutumia approach hii ya interpretation; kama tunatumia ya Uingreza, Wajerumani au whatever, lakini nadhani mnanieelewa.

Kwahiyo mkakubaliana wote kwa pamoja kwamba Jebra, kina Kibamba na watu wengine, wote tukakubaliana kwa pamoja kwamba tunaenda kwa approach hii halafu tutakuja kwenye public, haya hayatatokea. Sasa inaonekana wale draftsmen wa serikali wakajichimbia, wakatumia approach fulani huku wenzao wakiwa out of the picture. Wenzao wanapolalamika, wanasema tumetumia approach hii.

Hawa wadau, vyama vya siasa vikutane na serikali, na sisi viongozi wa dini tuwepo. Kwamba wote tunataka twende kwenye muelekeo huu. Tukifanya hayo hatutakuwa tunalaumiana, vinginevyo hata approach yako Profesa iwe nzuri kiasi gani, kama umejimbia peke yako, wengine watasema hatukuhusika. Wataipiga mawe tu.

Nuru Tamim, Mkurugenzi wa Wanawake wenye Ulemavu Tanzania, Movement of Women With Disabilities in Tanzania
Naenda moja kwa moja kwenye Sehemu ya 4 kifungu namba 34. Kinasema “Usaidizi”. Suala la usaidizi ni suala mtambuka. Usidizi ni mtu kuhitaji usaidizi moja kwa moja. Mfano mtu haoni au hajui kusoma na kuandika. Suala la kura si lazima nipigiwe na mtoto wangu. Inawezekana mtoto wangu mimi simuamini. Lakini kuna mtutunafanya naye kazi ofisini, sisi kama watu wenye ulemavu, ni mtu ambaye tunamuamini na ana hekima na ni mwadilifu, tunaweza kumtumia zaidi ya watu wawili. Mimi ningetamani hiki kifungu kiondolewe moja kwa moja.

Lakini pia, ningeomba Msajili wa Vyama vya Siasa. Kuna vyama vinapata ruzuku kutoka serikalini. Hivi vyama kama havitazingatia kuweka sera ya ujinsia na ujumuishwaji, view disqualified kupewa ruzuku. Hata kwenye kanuni liwekwe hili. Haya ni maoni yangu. Sijui kama nitapata platform ya kuonana na Msajili wa Vyama vya Siasa…

Lakini pia ningeomba tuwe na utamaduni wa kuridhika na kusifia. Kuna sheria za uchaguzi ambazo sisi watu wenye ulemavu tangu dunia ianze, hatujawahi kusikia tumeingiza kwenye mfumo isipokuwa ni hisani za vyama vya siasa. Utakuta kuna hisani ya chama fulani inatoa nafasi kwa watu wenye ulemavu lakini vyama vingine vinapiga tu kelele kushawishi watu; hawaangalii maskahi ya watu, wanyonge tena wa hali ya chini.

Jamani, tusilete tabia ya ushuzi kujambia chupi mpya na nguo mpya. Kila kinachofanyika kizuri hakisifiwi. Wewe ni ushuzi tu; nguo mpya unajambia, nguo ya zamani unajambia…

Esther Samanya, NCCR-Mageuzi
Mimi naenda kwenye kipengele cha sifa ya mpiga kura. Minapenda niseme hivi, labda tueleweshane kidogo hapa. Kuandikishwa kwenye mtaa. Mtaa kwa hapa Dar es Salaam si nyumba kumi-kumi. Mtaa ni kitu kikubwa. Hatufahamiani. Mimi labda natoka Mikocheni nakaa Mtaa wa Mikocheni B, ule mtaa ni mkubwa. Hatuwezi kufahamiana kule CocaCola hadi huku Ushindi. Nasema hivi kwa maana gani, katika uandikishaji huu tutakapokwenda kwenye serikali ya mtaa na utambulisho wowote kuwa nimejiandikisha.

Sasa nimepiga kura pale Mikocheni ninapoishi. Kumekuwa na kitu cha ajabu sana kwa sababu hii. Mtu anajiandikisha, unaambiwa nenda kajiandikishe kwa mtendaji nafika pale najiandikisha. Nimeandikishwa kwenye rejista lakini hamna kitambulisho kingine chochote kile, kwahiyo siku ya kupiga kura mimi niliyejiandikisha kama Esther Samanya anaweza akaenda Suzan, atapiga kura.

Kwahiyo, katika uandikishwaji kutakuwa na kitu kinaonesha kwamba mimi niliyejiandikisha katika mtaa huu ndiyo mimi niliyekuja kupiga kura? Maana uchaguzi wa serikali za mtaa tunaujua uhuni wake. Kwasababu saa 12 asubuhi unakuta aliye kwenye foleni kuanzia wa kwanza hai wa 1000 ni wa CCM na wana majina tofauti na wametoka mitaa mingine – Tandale, Manzese n.k…. Kwahiyo kazi ya ku-identify hawa watu si kazi ya Mtendaji kitafutwekitu kingine au kadi ya kuwapa.

Twaha Mwaipaya, Katibu Mwenezi – BAWACHA
Mimi nitazungumza machache kuhusu Muswada wa Sheria ambayo tunaijadili. Asilimia kubwa ya wahanga wa hii sheria ni vijana. Sisis vijana tulifika mbele ya Kamati ya Bunge kutoa maoni kama vijana na miongoni mwa aoni makubwa ambayo tulitoa kama vijana tulisema, kama Mtanzania akifikisha miaka 18 anahesabika kuwa mtu mzima, anaweza kakaoa au akaolewa, ni kwanini kijana wa miaka 18 anatumika kuwa daraja la kupiga kura peke yake… Kwanini vujana hawa wanatumika kama madaraja kwenye hii nchi?

Ukisoma hii sheria inasema mtu atakayegombea awe ana kazi halali ya kujiingizia kipato. Nchi hii Serikali imeshindwa kuwaajiri vijana wapo mtaani hawana kazi ya kufanya. Vijana wana elimu nzuri hawana ajira bado wananyimwa fursa na sheria hii kwenda kugombea.

Lakini ukisoma hizi sheria, hazijaweka wazi majukumu ya mwenyekiti wa serikali ni nini. Kwasababu vijana tukitaka kugombea serikali za mitaa, tunaambiwa yule kijana anataka kugombea anaweza kusuluhisha ndoa? Kwani kazi ya M/kiti wa Serikali ya Kijiji au Mtaa ni kusuluhisha ndoa? Majukumu ya M/kiti wa Serikali ya Kijiji, Kitongoji au Mtaa yawekwe wazi. Nilikuwa niko Bungeni mbele ya Kamati ya Bunge ya kupokea maoni, vijana wote vyuo vikuu walikuja na ajenda kijana akifikisha miaka 18 apewe haki ya kuchaguliwa. Sasa kwanini mnataka kututumia vijana peke yake? Hili hatuwezi kukubaliana nalo.

Lakini leo, yamezungumzwa mambo mengi sana kuhusu sheria. Hii sheria ya 2019 tuliitunga lakini haikufuatwa na serikali.Watu walipoteza muda kama hivi lakini hizi sheria hazifuatwi. Kuna changamoto kubwa sana kwenye hizi chaguzi za serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kuliko hizi ambazo tunazizungumza hapa. Hizi sheria tunazitunga kutimiza wajibu tu lakini hizi chaguzi zina ukiritimba kuliko chaguzi zote.

Sisis vijana msimamo wetu ni uleule. Tumetumika kiasi cha kutosha. Tumedharaulika kiasi cha kutosha. Asilimia kubwa nguvu ya taifa la Tanzania ni vijana. Tunatumika kwenye shughuli za kutumia nguvu lakini kwenye hizi chaguzi ambazo zinakuja hatutaruhusu kuona nchi yetu inaendelea kuchezewa.

Kama ambavyo ukienda pale Kariakoo, mwizi wa simu wa simu akikamatwa anachomwa moto. Mwizi wa kura atachomwa moto kwenye kituo cha uchaguzi. Mnatengeneza sheria mnashindwa kuzitekeleza mnategemea sisi vijana tutafanya nini? Ttaisaidia nchi yetu. Ipo siku sisi vijana tutahamasishana kugombea nafasi mbalimbali nan a tukichukua hizo nafasi tutakwenda kufanya mabadiliko ambayo ninyi hamtaki kuyafanya.

Antony Ishika Mghamba, ACT Wazalendo
Kukazia alichosema Twaha, vijana wa vyama vya siasa tuna mkakati wa kwenda kugombea serikali za mitaa. Niseme jambo moja kwamba, tangu jana na mpaka leo tunajadili. Tulishajadili mambo mengi na hapa bado unajadili. Na mambo haya ambayo tunajadili viko vyombo ambavyo vinapaswa kuchukua maoni haya kwenda kuyafanyia kazi.

Watu wa Tume, katika pekenyuapekenyua, naambiwa walialikwa. Wako wapi? Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wamealikwa. Wako hapa? Haya tunayoyajadili hapa, baada ya hapa, hivyo ndivyo vyombo vinavyotakiwa kwenda kuyafanyia kazi haya maoni tunayoyatoa hapa. Hawako hapa. Tunajadili.

Na hisia za watu wengi hapa wale ndiyowalitakiwa wazichukue lakini hawapo. Kwahiyo mimi nishauri kwamba moja ya maazimio tunalopaswa kutoka nalo hapa, hivi vyombo ambavo ndiyo vilipaswa kupokea maoni yetu na vyama vyote hapa lakini vyenyewe havipo hapa, kuwepo na mkakati wa pamoja wa wadau na wajumbe walioko hapa wa namna ya kuanza kuandaa taarifa na kuwafikishia ofisini kwao haya maoni yetu hapa kwakuwa wamealikwa na wamegoma kuja. By the way, ingekuwa ni kule kwenye vikao vyetu vya vijana, tungesema wametudharau.

Kwenye hizi chaguzi za serikali za mitaa, wanaopiga kura ni wale kule kwenye kaya. Yaani uchaguzi wa serikali za serikali za mitaa wapiga kura ni kaya. Yaani boma la mtu fulani lina watu kadhaa. Kama ilivyoelezwa, mjini ni ngumu kufahamiana, lakini kule kwetu vijijini watu wanafahamiana – mtu wa Kijiji hiki anafahamiana na mtu wa Kijiji kingine.

Kwa wale tulioenda huko mikoani kufanya siasa, wananchi huku chini wamelishwa matango pori kwamba chama pekee kinachoweza kuongoza hii nchi, ni Chama cha Mapinduzi. Kitu ambacho si kweli. Unafika unakutana na mtu anakwambia hana chama lakini hata nikienda kupiga kura si CCM tu watakaoshinda kwasababu kuna matango pori ambayo wananchi wamelishwa.

Nini cha kufanya katika hili? Lazima kuwae na mkakati madhubuti wa kutoa elimu za uraia huku chini kwa wananchi. Asasi mbalimbali ambazo zinatoa hizi elimu, tuwe na mkakati wa kuwafikia watu huku chini tusibaki tu hapa Dar es Salaam. Huko chini wananchi wana uhaba wah ii elimu ya uraia na hizi elimu za sheria za chaguzi ambazo zinaamua maendeleo yao.

Nimalizie kwa kusema kuwa vijana awamu hii tunaanzia na uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Mimi natokana na Chama cha Mapinduzi”
Ndugu zangu, nimesikiliza maoni toka jana, lakini lengo la mkutano kwa mwaliko wangu nilioupata ni kutetea wanawake na vijana watakapopata nafasi katika uongozi na wanawake waongezeke asilimia kwasababu tunaona asilimia sio kubwa, hatujafikia.

Lakini nilivyosikiliza toka jana ni lawama, lawama toka mwanzo hadi mwisho. Mimi nashauri, huwezi ukakaa na ukajadili Dar es Salaam ukajadili mikoani mambo ya vijijini na vitongoji. Lazima urudi kule, ujipange uwe na ushirikano na wapiga kura.

Kwa mfano mimi, nahamasisha vikundi vyote katika wilaya ya Monduli, nahamasisha wamama wajitenge kwenye vikundi wacheze hisa. Ila kwakuwa natokana na chama changu, na ninapenda kibaki madarakani, naingiza hilo jambo hapo. Je, wewe umejipangaje au unakuja tu kulaumu?

Hapohapo, kwenye msiba nakuwepo, kwenye mwanafunzi anayekosa nauli nakuwepo, mama aliyelala njaa nagawana naye kilo kumi, kilo tano. Kwahiyo, siku ya kura yule mama takuelewa vipi wewe mgeni wakati hujashiriki naye kwenye shida?

Naomba tujikite kwa wanawake kuwa watashirikije na watapataje nafasi.

Janeth Rithe, Naibu Katibu Mwenezi wa chama – ACT Wazalendo
Naomba nichangie kwa vitu viwili au vitatu. Suala zima la uchaguzi serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, hayajawa ni mazingira rafiki. Sheria ambazo zipo, zinazotuongoza kwenya hizi chaguzi bado serekali za mitaa, vijiji na vitongoji havionekani kama ni vitu vya msingi na vya muhimu kupata viongozi walio sahihi.

Wakati wa uandikiswhaji wa watu kwenye daftari au kule kwenye vijiji na vitongoji, huwa ni majina tu yanaandikwa. Nitawapa mfano mmoja. Mwaka 2014 kwenye kata moja hapa jijini Dar es Salaam, CCM mara nyingi wanajidai kuwa ni wajanja sana. Lakini na sisi inabidi tujifunze ujanja wao sasa. Waliandika majina ya wapiga kura kwenye serikali ya mtaa, baada ya kura kwenye serikali yale majina hayapo.
 
Unadhani Chadema haijachongwa na Nyerere kupitia Edwin na Bob?
Sawa lakini ccm tumeshiba Hadi ubongo umevimbiwa hatufikirii sawa sawa. Tune zote za warioba,kisanga,nyalali zote zimeeleza mambo Yale Yale na sisi ndio tuna serikali kwanini tusingeyafanyia kazi?

Tumekalia siasa chafu za sumu kwenye maji,na kupiga dili.plus wizi bhasi hakuna kingine!

Leo hatuna ujanja tulinywe tu.
 
SAWA lakini ccm tumeshiba Hadi ubongo umevimbiwa hatufikirii sawa sawa!!tune zote za warioba,kisanga,nyalali zote zimeeleza mambo Yale Yale na sisi ndio tuna serikali kwanini tusingeyafanyia kazi!!?

Tumekalia siasa chafu za sumu kwenye maji,na kupiga dili.plus wizi bhasi hakuna kingine!!

Leo hatuna ujanja tulinywe TU!!
Tatizo la CCM ni kurithishana Uongozi bila maandalizi ya Vizazi kwa mtazamo mpana wa Dunia

Wamekariri kuwa Uongozi ni Jina la Ukoo

Chadema ina vijana walioandaliwa na wengine Maguful aliwaingiza CCM akidhani wanaunga Juhudi zake kumbe walikuwa mbele yake zaidi

Vijana hao ndio wataleta mabadiliko ya " ghafla" ndani ya Lumumba
 
Back
Top Bottom