Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Dangote Mtwara apandishwa kizimbani

Tutashuhudia mengi sana awamu hii ya mh. Magu. Ukipita Dangote nje ya kiwanda utawakuta vijana wengi wa kitanzania wapo wamepiga kambi nje getini wanasubiri ajira.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara ameagizwa kwamba akiwakuta hapo nje vijana hao awakamate na kuwapeleka kambini wakalime
 
Wacha tu. Naona ile mada ya awali imejibu. Hongera sana aliyeleta ile mada. Sasa hawa wahamiaji haramu aidha waondoke au wafuate taratibu za msingi kuishi hapa nchini
 
Nilisikiaga kwamba endapo kampuni ya Dangote ingekamilika ingeweza kuajiri vijana wa Kitanzania zaidi ya 3000 ama mimi nilisikia vibaya??
 
Kama taarifa hiyo nikweli basi jibu limepatikana. Hawa ndio wanatufanya tuwe maskini
 
Mi nashauri wizara ya mambo ya ndani waweke portal ya sisi raia wema kureport hawa wageni. Watu tunajua mengi lakini tunashindwa tutaenda kusemea wapi? Mtu aende Uhamiaji wanapopokea rushwa kutoa habari kama hii, haki ya nani hamalizi week 2 utasikia kapigwa risasi kafariki na watu wasiojulikana.

Kwanini serikali isifaidike na maendeleo ya kimawasiliano. Waeke portal watu watiririke......kuna wahindi, wakenya, waganda, na wachina wengi tu humu wanazurura bila vibali na wanafanya kazi ambazo mimi na wewe mtanzania mwezangu tunazimudu.
Mkuu watu wanahofia usalama wao, huo mfano uliotoa wa mtu kusikia kapigwa risasi ni mfano wenye uhalisia ndio maana hata polisi hawapati ushirikiano mzuri na raia hadi wakamate watu kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom