Wananchi,
Chanzo cha matatizo yote yanayotusibu hivi sasa ni sisi wenyewe wananchi. Wanasema, mvunja nchi ni mwananchi. CCM ni Chama cha Mapinduzi. Tumeshakaa kitako tukajiuliza, chama hiki kinampindua nani? Je, nchi yetu inahitaji mapinduzi? Mapinduzi ya kitu gani? Na huyu anayepindua ni nani?
Hiki ni kikundi cha watu wachache wajanja waliojiwekea au niseme wanaojiwekea nafasi ya kutumia migongo ya wengi kujipangia na kujiwekea nafasi ya kujijengea na kujilindia maslahi yao na ya familia zao.
CCM hii leo, si chama cha siasa bali ni chama cha sihasa. Ukimwona mwananchi anaishabikia sana CCM hivi sasa basi ujue ni mjanja 1. Anakula nayo 2. Anawake humo naye ni kupe 3. Anamatumaini ya kupata nafasi ya kujiingiza humo aweze kuwa mmoja wao au 4. Mjinga, anashabikia CCM kama anavyoshabikia chama cha mpira wa miguu, kufuata sherehe za ushindi. Hasa akishavishwa kofia za magwanda ya kijani na njano.
Wale watu wote wanaogombania uongozi katika CCM kwa hali na mali usidhani kuwa wanafanya hivyo kwa kuwa ni wanasiasa na kwamba wanauchungu na nchi yao na kwamba wanataka kuinua maisha ya mwananchi wa kawaida. Kalaga baho na ubozi wako!
"Mwizi ni yule mwenye kukamatwa na yule ambaye hajakamatwa si mwizi ingawa wote ni wezi." Kila anayepatikana na kashfa ya wizi na ufisadi mpaka hivi sasa ni mwanachama wa CCM, tena kada kiongozi wa CCM au serikali ya CCM au vyote. Umepata kufikiria wamo wangapi wengine humo ambao bado hawajakamatwa? Haiwezekani mtu asifikirie kuwa wamo wengi tu.
Kama hivyo ni kweli, itwezekana vipi humo wapatikane watu wa tume ya kuwachunguza wenzao na kuwachukulia hatua ya kuwadhibiti?
Mambo haya hayakuanza leo ndani ya CCM, mambo haya yameanza tangu TANU. Mwalimu ilikuwa ni kawaida yake kiongozi akiharibu hapa, adhabu yake ilikuwa ni kiongozi huyo kuhamishiwa kwenye uongozi palee. Anaambiwa ni lazima alindwe maana ni mwenzetu huyo.
Eti wanalindana!
Pamoja na kuyajua haya yote, sisi wananchi tumekazana kuwarudisha madarakani miaka yote hii tangu 1961. Tunadanganywa na kukubali eti hii ni serikali ya Nyerere, hii ni serikali ya Mwinyi, hii ni serikali ya Mkapa na hii ni serikali ya Kikwete.
Hakuna lolote wala chochote, hii ni serikali ile ile ya TANU, AFRO SHIRAZ na CCM.
Imefika wakati wananchi tuamke tuibadili hii serikali tuwape wapinzani. Hasa wananchi wanaotakiwa kuamka zaidi ni wale wanaoishabikia CCM kama timu ya mpira wa miguu, niliowataja katika kundi la nne hapo juu.
Wao ndio wanaotumiwa sana katika kuiba kura, kuanzia kwenye undikishaji, upigaji kura mara mbili mbili, kubeba masanduku ya kura haramu, uwakilishaji na uhesabuji wa kura na kuwapigia debe huku sauti zikiwakauka na jasho kuwamwagika. Kila mwaka wa uchaguzi viongozi wanatoa ahadi hewa na wananchi wanakazana kuwa shangilia.
Uchaguzi ukimalizika, mambo ni yale yale, njaa tupu, matumbo yamejaa matumaini hewa na vichwani hatufikiri na kujiuliza tuliyoahidiwa yako wapi? Lile kundi la wajanja linazidi kuneemeka na kupanga mikakati ya uchaguzi ujao. Wajinga ndio waliwao.
Ndio, nasema tuwape wapinzani hata kama na wao ndio hao hao. Hawa nao wakiwa wapuuzi, tuwanyime kura nao. Tuwapindue pindue kama wanavyotupindua pindua sisi. Katika vile vipindi wanavykosa kura na kula, njaa itawafundisha nidhamu.
Wananchi tukijijengea uwezo wa kuwaingiza na kuwaondoa hawa madarakani, watatuogopa na watatuheshimu. Hali hii itawafanya watufanyie kazi sisi badala ya matumbo yao.
Wajengaji ni sisi wananchi na wabomoaji ni sisi wananchi. Hatughadhibiki? Hawa watu mpaka wanafikia hatua ya jeuri ya kuita $1,000,000 vijisenti! Vijisenti? Wananchi hawajui leo watakulanini hii leo, licha ya hiyo kesho. Halafu mtu anadiriki kusema vijisenti. Jeuri hii anaitoa wapi, kama sio kwetu sisi wananchi. Ndio, sisi ndio tunaowapa hawa jeuri na majivuno. Ni kosa letu.
Haya, nasikia eti Yona naye anasema, "kama yuko mwananchi mwenye ubavu, amfikishe mahakamani." Kama hii si jeuri, basi ni nini?
Ngoja tuone Mr. Clean naye atakavyotuchamba, tupate habari yetu.
Ni kosa letu wananchi. Kumekucha, tuamke!