Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,509
- 22,387
Lengo la mada hii ni kuona wale wapenda demokrasia na siasa za kweli wakijongea hapa na kushusha nondo na madini mbalimbali katika kufanya kitu chitwa "brain storming".
Katika muktadha huo basi, tutaweza kuangalia sera za chama cha CCM ambacho ndicho chaongoza serikali ya Tanzania kwa sasa na pia ilani ya chama hicho na utekelezaji wake na wapi wamefikia.
Pia mada hii itatoa fursa ya kuangalia hali ya uchumi wa Tanzania kati ya 2015 na 2021 na baada ya hapo ni wapi tumekwama, sababu za kukwama na nini kifanyike kwa maana ya kwamba je, serikali ina washauri wanofaa wa uchumi "Think Tanks", taasisi binafsi za kuchambua sera za kiuchumi na wadau mbalimbali na nini nafasi yao katika kuishauri serikali katika nyakati ngumu au nyakati tata.
Hali kadhalika mada itakaribisha maoni ya upinzani, hali yake kisiasa, uwezo wake wa kuendeleza harakati na nini kifanyike ili kuleta chagizo ambalo litaweza kutikisa hali ya kisiasa nchini hususan CCM.
Hakika uchaguzi wa Kenya umetoa funzo kubwa kwa wale wanofuatilia harakati za kisiasa na kutufumbua macho wengi wetu kuwa kweli Wakenya wana demokrasia ya kweli.
Lakini kuna mambo matatu makubwa ambayo ndiyo yaliyonichagiza kuamua kuanzisha mada hii.
Kwanza, ni Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya ambayo imeonyesha hali yake ya kuwa yajitegemea, ni huru na haina mashinikizo kutoka sehemu yoyote ile. Tume ikatangaza ushindi wa Rais Ruto licha ya kwamba Rais aliyepita Bwana Uhuru Kenyatta alikuwa waziwazi akimuunga mkono Bwana Raila Odinga. Hata humu JF yumo mwenzetu mmoja na wengine kadhaa ambao walionyesha kuumunga mkono Bwana Odinga.
Bwana Odinga alipinga matokeo hayo kwa kudai kulikuwa na mizengwe ya udanganyifu na mwishowe mahakama uamuzi wa kuthibitisha ushindi wa Bwana Ruto, uamuzi ambao wapiga kura wengi wa Kenya waliukubali kuwa ulikuwa wa haki na ukweli.
Lakini ushindi wa Rais Ruto ulionyesha kuwastua wana CCM na wafuasi wao kwani katika uchaguzi wa Kenya hakukuwepo na ahadi ya goli la mkono.
Hii dhana ya goli la mkono ni kuthibitisha kuwa CCM ni chama dola na kina uwezo wa kuamua kuwa madarakani kwa muda wowote ambao chama hicho kitapenda kukaa na chaguzi zote zitaamuliwa na wao kwa kutumia vyombo vya dola.
Pili, wenzetu Wakenya uchaguzi wao ulikuwa na maandalizi ya kutosha, kuanzia wapiga kura kujiandikisha hadi kila kituo cha kupigia kura kuwa tayari kimepokea fomu zote za kupigia kura.
Moja ya sababu kubwa ya hapa ni uwezo wa wagombea wa upinzani kuweza kuchukua fomu au kujiandikisha uzuri kituoni salama bila kubughudhiwa na kuthibitishwa na kisha kuketi mahala au kwenda nyumbani kusubiri matokeo salama.
Hali nyingine ni kwa vituo vya kupigia kira kuendelea kupokea wapiga kura na kufungwa mara tu na inapothibitika kwamba wapiga kura wote wa CCM na vyama vingine wametumia haki yao hiyo ya kikatiba kufanikisha zoezi hilo.
Tatu, mitandao ya "internet" ni muhimu sana katika nyakati za uchaguzi na husaidia taasisi kama tume ya uchaguzi kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi kwa kuweka fomu za kujiandikisha katika tovuti yake ambapo wapiga kura wataweza kunywila fomu hizo kwa haraka na kuzirudisha vituoni bila kuchelewa.
Pia hiyo itasaidia kuwawezesha wapiga kura kufuatilia matokeo ya uchaguzi mitandaoni bila kusubiri kwa muda mrefu. Pia mitandao itasaidia kurahisisha mawasiliano baina ya watanzania waliopo maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi bila kuzuiwa wala kukwamishwa.
Hayo mambo matatu ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha uchaguzi wa hawa majirani zetu jambo ambalo ni la kujivunia kwao na kulitamani hapa kwetu Tanzania.
Sasa basi, Tanzania yaelekea kufanya Uchaguzi wake Mkuu wa Urais mwaka 2025 na kabla ya hapo utakuwepo uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024. Jambo la msingi ambalo CCM na serikali yake yapaswa kufanya ni kutorudia hali ya mwaka 2019 ambapo vyama vya siasa baada ya kukaa pembeni kwa miaka mitatu hadi minne ndiyo vikaja kushiriki uchaguzi.
Jambo jingine ni CCM na serikali yake kuhakikisha wapinzani hawapati bughudha kutoka kwa vyombo vya dola hasa Polisi na Usalama wa Taifa.
Wakati sasa umefika wa wapinzani kuamua kuwa imetosha na kazi ianze. Lakini wanaanza vipi kampeni ilihali mikutano imepigwa marufuku?
Hapa ndipo penye kiini cha mada na wapinzani wapaswa kuja na mikakati na mipango sahihi na thabiti.
Kuna kitu chaitwa "Tools for Activists" au kwa kiswahili ni nyenzo kwa wanaharakati ambazo hutumika kuandaa shughuli za chama mbadala. Napenda kutoa picha ya chama mbadala yaani "alternative party" kwa CCM.
Chama mbadala kitatoa mawazo mbadala kuhusu nini kifanyike katika maeneo ya siasa, uchumi na kijamii.
Moja ya sababu kubwa ya vyama vya upinzani kama CHADEMA kushindwa katika kukabiliana na chama chenye nguvu kama CCM ni kushindwa kuunda nyenzo sahihi za wanaharakati wake na kuzitumia kufasaha. Nyenzo hizi husaidia shughuli za chama, wanachama na wafuasi kuwa pamoja na kueneza ujumbe.
Kwa kuwa CHADEMA ndiyo chama pekee na kikubwa cha upinzani kwa sasa, itabidi chama hicho kipigwe msasa na nakshi ili kiweze kuwa na taswira ya chama tishio na kilicho tayari hasa kuchukua madaraka ya kuongoza Tanzania.
Hivyo basi, tuangalie safu yake ya uongozi, makada wake na wanachama wake ambao wataamua kusimama katika chaguzi zijazo. Sasa hilo ni suala ambalo CHADEMA wenyewe wapaswa kuamua haraka maana katika saa ya kisiasa muda huu ndiyo chama kipo katikakati.
Baada ya kuangalia huko juu kwenye uongozi tushuke chini kidogo kuangalia idara ya uenezi na propaganda. Hivyo ni lazima kwanza CHADEMA wakiri kwamba hakuna watu wenye uwezo au waliopo ni wachache . Hivyo kuwepo na timu maalum ambayo itashughulika na masuala ya teknolojia na mitandao yote IG, Twitter na kwingine na hilo ni jambo la dharura.
Hizi nyenzo au "tools for activists" zipo za aina mbili zipo za kawaida kabisa yaani kwenye uwanja wa kisiasa na zipo zile ambazo hutumika mitandaoni.
Sasa baada ya kuongea hayo na kutambulisha mada hii ambayo kama nilivyoomba hapo mwanzoni kwamba iwe endelevu hadi ifikapo wakati wa chaguzi zote (2024 na 2025) ningependa kuungwa mkono na wadau wote ambao wanataka kuona Tanzania yarudisha uchumi wa kati na uchumi huo hautetereki.
Kisha nitaendelea kutoa kidogokidogo zile nyenzo ambazo wanaharakati na wanasiasa wa upinzani wazihitaji ili kuiga mazuri ya uchaguzi wa Kenya na busara za mzee Raila Odinga kukubali kushindwa uchaguzi bila kinyongo.
Karibuni sana ndugu zanguni na naomba tuache utani na maneno yasiyofaa.