Agenda ya katiba mpya ipo pale pale. Hata wale waliojaribu kutuhadaa kwa "katiba pendekezwa" ambayo ni katiba ya watawala badala ya katiba ya wananchi, wanajua fika kwamba hawakututendea haki na bila shaka wanajipanga upya. Isitoshe katika uchaguzi uliopita UKAWA walileta changamoto kubwa na kupata mafanikio makubwa ambayo bila shaka yatawafanya kutafuta kuimarisha ushirikiano wao. Watanzania wenye mapenzi mema na nchi hii wanawaombea UKAWA usiku na mchana kwani hata watawala wetu sasa wanazungumza MABADILIKO. Tanzania imebadilika sana kutokana na uchaguzi wa 2015 na UKAWA imechangia mabadiliko haya.