MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,380

PICHA: Padri Martin Luther
Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa Katoliki wakati wake, yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya mtu. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo wa sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.

Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na cha Danieli.

Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi wa kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafuta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi wa Mungu hasa hawa wa kileo wasiojua historia vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.

Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati wa ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.

Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo wa majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.

Nimengi sana ya kujifunza lakini kwa Leo naishia hapa.

ZAIDI TAZAMA HAPA

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.


MAONI YA WADAU
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
--------------
--------------
--------------
Deogratius Kisandu,

DOCUMENYARY HII IMEJIBU



-------------
 
Martin Luther alishapata cheo cha , 'uaskofu' wakati huo. Dhana kwamba alifuta vitabu 7 napata shida mamlaka hayo aliyapata wapi? Mnyonge mnyonge lakini haki yake mpe

Mkuu kwa hili huna data.... Martine hakuwa Askofu, alikuwa Padre na miongoni mwa sababu zilizomuondoa kwenye kanisa Katoliki ni hili la Uaskofu, alipinga hairakia ya Kanisa na vyeo kama Uaskofu, Upapa na mengineyo. Sema tu mengi aliyoyapinga aliishia kuayatenda akiwa kwenye kanisa lake. Mengine ni suala la Useja, hakutaka kabisa kulisikia na alipoondoka aliondoka na Mtawa wa kike aliyeishia kuwa mkewe.

Mambo ni mengi sana na yanahitaji muda wa kutosha. Lakini niseme tu kwamba "siyo kila alilolipinga lilikuwa baya" mengine aliyapinga kihalali kabisa japo njia aliyoitumia haikuhalalisha kitendo chake!!!

Pili, Biblia za wapeotestanti na wapentekoste zina vitabu 66 wakati biblia ya Wakatoliki ina vitabu 72. Hili lilitokana na kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye vitabu hivyo (deuterokanoni) vinapingana na mafundisho yao. Sababu nyingi ni za kibinadamu tu!!! Hili lilikuwa rahisi sana kwake kwani suala zima la "Utaifa" liliingizwq kwenye huu mchakato wa Luther kujiondoa kanisa, matokeo yake kwa vile alikuwa Mjerumani, dhehebu lake likawa "dini dora" ya Ujerumani, katika hali kama hii, ni rahisi kwa uwezo wa kifedha kuchapisha Biblia zenye vitabi 66 na kuviondoa vile vingine!!!!
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao wanawapotosha, hawaijui biblia
Duh kaaazi kweli kweli hapo ndo mlipo mpa cheo binadamu mwenzenu awe mwombezi. mmesahau kwamba mariam na yeye ni binadamu kama niniyi na alishakufa anasubiri ufufuo siku ya mwisho.. sasa sijui nani kawadanganya kwamba maria yuko hai. Au ni katika kitabu gani kimemtaja Mariam Kwamba yi hai ambapo anaweza kusikia maombi yenu
 
Biblia inasema Bikra Maria ataitwa mbarikiwa, na dunia itamsifu kuwa yeye ni mbarikiwa. Bikra Maria kwa mujibu wa kumbukumbu za kanisha hakufa, alipaazwa. Ujui historia, huyu mama ni the special, hata waprotestant wakimtupa sisi Wakatoliki tutaendelea kutimiza unabii kwa kumuita mbarikiwa
 
alipazwa? lete andiko acha hizo historia za kanisa mlizo mezeshwa na zilizotungwa na watu ndio maana Luther mlishindwa kujibu hoja zake..

Haya lete andiko la kupazwa kwa Maria
 
Mbona hujaelezea jinsi ilivyokuwa watu wanauziwa vyeti baada ya kufanya dhambi kama uzinzi. eti kwa kununua cheti hicho atakuwa amesamehewa. Then anarudi tena anafanya as long as anapesa za kununua vyeti vya msamaha wa dhambi.....[HASHTAG]#hujui[/HASHTAG] tu hayo makasri ya huko Roma yamejengwaje.

njoo tukujuze..
 
uongo wa mchana hebu lete andiko.
maana maria ndiye aliyesema hivyo.
LUKA 1:46-48.
anasema watamwita mmbarikiwa lakini sio Mungu kusema tutamwita hivyo
 
Deogratius Kisandu,

Father Martin Luther alikuwa ni padre mwenye akili nyingi sana kuliko watu wengi wa kizazi chake cha karne ya 15.

1. Martin Luther aliviondoa baadhi ya vitabu katika canon ya Biblia baada ya kutoka katika Kanisa Katoliki.
2. Mambo mengi ambayo Martin Luther aliyasema katika karne ya 15 na kupingwa ndio ambayo Kanisa Katoliki linayatekeleza kuanzia karne ya 20. mfano. Kuchapisha Biblia katika Lugha asilia kama Kiswahili nk, kuruhusu lugha za kienyeji katika ibada ya misa nk
3. Kanisa Katoliki lililazimika kuitisha mtaguso mkuu wa Trenta ili kujibu hoja za martin Luther na kwa kuwa lilikuwa alikujiandaa liliishia kutoa makaripio ya kukemea tu anathema sit
4. Martin Luther ndio alisababisha katika kila chuo kikuu duniani lazima awepo padre anayeitwa chaplin
5. Martin Luther alipunguza pia idadi ya sakramenti kutoka 7 sa kanisa katoliki mpaka 3 za walutheri.
6. Martin Luther aliungwa mkono na taifa la Ujerumani.

Ahsante kwa sasa
 
Hapa mimi ndipo ninapochoka, sasa kwanini husemi kwa ushahidi, kuwa kifungu gani na wapi umepata hayo,
au ndio umeimbishwa tu? .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…