Mitandaoni wanatazama urembo badala ya kazi yangu'- Balozi wa vijana AU

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
700
1,452

AU

CHANZO CHA PICHA,DIANA CHANDO
Maelezo ya picha,Balozi wa vijana Umoja wa Afrika -AUMaelezo kuhusu taarifa
  • Author,Na Esther Namuhisa
  • Nafasi,BBC News, Dar es Salaam
  • Saa 7 zilizopita
"Unajua mimi nina macho makubwa, mara nyingi nikiweka kazi zangu watu wanaanza kuuliza kuhusu muonekano wangu, urembo wangu badala ya kazi na staki kudanganya hilo jambo huwa linanikera sana’ anasema Diana Chando, balozi wa vijana Umoja wa Afrika(AU).
Diana Chando (27) ni mwanasheria na mbobezi wa sera anayependa kugusa maisha ya vijana wenzake. Anasema lengo lake kubwa ni kufanya kazi na kuacha alama kubwa katika maisha yake kwa kubadilisha maisha ya watu.
Diana anasema wakati anasoma chuo kikuu kuna siku alipata fursa ya kuwasilisha mada kwa kuwa mhusika hakuwepo na mgeni rasmi alikuwa balozi kutoka Geneva, Uswisi.
Baada ya uwakilishi mzuri, alipewa fursa ya kwenda kwenye mafunzo ya amani, na ndipo safari yake ya kuwa mhamasishaji wa amani ilipoanza.


Ni binti aliyepata malezi kutoka kwa mama pekee, kwa kuwa baba yake alifariki dunia akiwa mdogo sana.
Diana anajivunia hatua aliyoifikia ya kuwa balozi wa vijana wa Afrika huku akiwa amejiwekea misingi thabiti ya kusimamia malengo yake au ndoto zake kubwa.
“Mama yangu ni mchapa kazi sana, mama amekuwa nguzo kwangu kwa kuwa nimeona kujitoa kwake, uaminifu wake, umahiri wake katika kazi na hata elimu aliyonipatia ni zawadi tosha kwangu.
AU

CHANZO CHA PICHA,DIANA

Adabu na uvumilivu ni silaha ya uongozi​

Mabinti tuna fursa nyingi sana, ukiwa binti mdogo mwenye malengo makubwa haswa kwenye jarida la uongozi lazima kuwa na kitu kinaitwa ‘adabu’.
Kama huna adabu huwezi kufika popote, kwa sababu kama huna adabu huwezi kujua namna nzuri ya kuongea na watu, hutaacha jina zuri kama huna adabu na hutaacha muonekano mzuri kwa watu kama huna adabu , ni utakuwa tu mwanamke mrembo lakini hamna kitu, adabu ni muhimu sana.”
Diana anasisitiza hilo kwa kuwakumbusha vijana kuwa ule msemo unaosemwa kuwa ‘si kila kikombe cha fursa kinachokuja mbele yako ni cha kwako, ni muhimu kujua kipi cha kwako na kipi sio cha kwako vinginevyo utakula sumu.
Adabu ni msimamo wangu wa kwanza katika kujua fursa yangu iko wapi.
Jambo lingine muhimu ni uvumilivu, sipendi kusikilizwa kwa sababu mimi ni binti. Kuwa mwanamke hakunifanyi mimi nifike sehemu bali naamini kuwa utendaji kazi wangu, akili na kujitoa ndiyo kunanifanya nifike sehemu. Sipendi nipewe kitu kwasababu ni mwanamke, bali napenda kupata kitu kwa kuwa nina weledi wa kukifanyia kazi.
Kuna wanawake wengi wanapewa nafasi katika uongozi lakini hawafanyi chochote, ni wakati sasa kutoangalia kwa sababu wewe ni mwanamke.
AU

CHANZO CHA PICHA,DIANA

Umuhimu wa kujitolea​

Mtanzania huyu anayewakilisha vijana wa Afrika Mashariki katika umoja wa Afrika AU amedhamiria kuwa kiongozi atakayeacha alama katika jamii. Anasema si kwa sababu yeye ni mwanamke mwenye uthubutu tu bali kwasababu anajiamini na anaweza kutoa mchango wenye tija katika ulingo wa uongozi. Ni vyema kwa vijana kutoangalia elimu peke yake, ni vyema kupata ujuzi.
‘Niliandika kuomba kazi ya ubalozi Umoja wa Afrika nikiwa najua fika sina kigezo cha shahada ya uzamili, lakini nilisema kwa sababu ukiomba kazi kuna kupata na kukosa, niliandika tu kujaribu na kujiamini kuwa naweza.’
Aidha nafasi hiyo ya ubalozi wa vijana imempa fursa ya kuweza kuongea mbele ya viongozi wakubwa jambo ambalo anajivunia na kuona kuwa vijana wakiaminiwa wanaweza.
‘Ninaamini nikiwa nafanya kazi vizuri, vijana wenzangu pia watapewa fursa hivyo mimi ni ninajiona kuwa ushuhuda na njia kwa wengine.
Kujitolea ni jambo muhimu sana, wakati ninasoma nilikuwa ninajitolea kwenye asasi kama Yuna, tunapanda miti na vitu vingi bila malipo lakini kwenye wasifu wangu ninaandika kila kitu na imenijenga.
Kuna Watoto wengi wanasoma hata nje ya nchi lakini wanasoma tu darasani na kurudi nyumbani yani hawajiongezi. Kiukweli, Kujiongeza kumechangia mafanikio yangu
au

CHANZO CHA PICHA,DIANA

Umaarufu mtandaoni wakati wa uchaguzi wa rais Zimbabwe 2023​

AU

CHANZO CHA PICHA,DIANA
Diana Chando alipata umaarufu mkubwa sana mtandaoni wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu wa urais nchini Zimbabwe baada ya picha yake kusambaa mitandaoni.
‘Uchaguzi niliosimamia Zimbabwe, ulinitingisha sana.’
Katika uchaguzi, Umoja wa Afrika huwa wanatuma waangalizi na Diana alienda ikiwa sehemu ya jukumu lake la kusimamia uchaguzi akiwakilisha vijana.
‘Siku moja kabla ya kupiga kura, nilizunguka vituo zaidi ya 100, nilichoka sana na kuamua kupiga picha nikiwa kwenye gari nikaandika kuwa vijana wenzangu kesho uchaguzi ni vyema mkapige kura.
Niliandika twitter (X) lakini ile picha ilisambaa sana kwenye magroup ya whatsapp.
Nilipata umaarufu sana kwenye makundi ya vijana na walitaka kunihoji kwa sababu mimi ni binti mrembo katika kusimamia uchaguzi, jambo ambalo sio sahihi.
Vilevile Ukurasa wa Ikulu, ulitumia picha yangu kushukuru wasimamizi wote wa uchaguzi na hapo ndiyo tatizo lingine likatokea baada ya kushukuru.
Wapinzani waliibuka kwenye twitter wakitumia na maneno mengi makali, nikawa natumika kama fimbo ya kuchapia walioshinda.
Nilijisikia vibaya, maana niliambiwa kuwa natumika.Hata rais pia alishangaa huyo binti ni nani anayezungumziwa nchini kwake? Na mimi pia nilishangaa sana gumzo lililoibuka katika mitandao ya kijamii kuhusu mimi?
Lakini tukio hilo lilinipa funzo kuwa ni vyema kutumia mitandao ya kijamii, vizuri.

Hata kama mtu ni kiongozi lakini yeye pia ni binadamu ana hisia.​

AU

CHANZO CHA PICHA,DIANA
Ingawa ni kweli huwezi kumchagulia mtu maneno ya kusema, Nimejifunza pia kuwa ukichagua kikombe ambacho kinajumuisha maamuzi ya watu wengi, ni vyema kukubali kuendelea kukishikilia na kukubali.
Hekima ya kutojibu, ndio ilikuwa silaha yangu, mimi ni mtu wa kusikiliza tu AU pia walikuwa wananipigia simu kunijulia hali yangu, ila niliwaambia kuwa niko sawa tu nilijua itachukua siku kadhaa.
Ila ilichukua zaidi ya mwezi mpaka leo hii mwaka umepita bado kuna watu wanaandika kwenye ukurasa wangu, wanasema wamenikumbuka Zimbabwe.
Hata hivyo, tukio hilo la ushambuliaji mtandaoni kwa sababu ya muonekano wangu halikunifanya nirudi nyuma, bado ninaendelea na kazi yangu nilikwenda Comoro, ambako ni kisiwa na ghasia zilikuwa kubwa. Ninashukuru Mungu kuwa nimejifunza siasa za Afrika nikiwa na umri mdogo.

Urembo wangu usiwe kikwazo katika kazi yangu​

m

CHANZO CHA PICHA,DIANA
Mara nyingi nikiweka ujumbe kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii kwa asilimia kadhaa ujumbe huwa unafika na wanatoa mapendekezo yao au kuuliza maswali ila wengi huwa wanazingatia urembo wangu.
Mimi kama binti huwa najisikia vibaya nisiwe muongo mpaka sasa ukiangalia Instagram yangu ninaweza kupita miezi miwili bila kuweka chochote mtandaoni na si kwamba hakuna kazi ninazofanya ila watu wanaweka maoni kuhusu mimi badala ya kazi ninayoifanya.
Wengine huwa hata hawasomi nilichoandika, wanaangalia urembo wangu tu au macho na wanaacha ujumbe muhimu niliouweka.
Staki uhalisia wa kazi yangu ubebwe na urembo wangu.
Sipendi hata kujibu maoni ya watu kwa sababu hiyo.
Kwa mfano, nimepiga picha na rais ila mtu anakuja kutoa maoni ya urembo. Urembo wangu usiwe silaha ya kuchapiwa, sikuamka na kutaka kuumbwa hivi huwa najisiki vibaya sana.
Nataka kutambulika kuwa huyu binti ambaye ana macho makubwa anafanya kazi, ana akili, anawakilisha nchi, ana heshima na anajitambua. Hali hiyo inaniwekea hofu kuwa urembo unaficha uwezo wangu. Inanifanya nijihukumu, wakati staki malengo yangu yafungwe.
AU

CHANZO CHA PICHA,DIANA
Maelezo ya picha,Diana akiwa na rais wa Kenya William Ruto
Mfano kwenye picha na rais wa Kenya, ambayo aliniita 'hustler' na alikuwa amepitisha nakala kuhusu vijana. Ilikuwa kazi kubwa sana niliyoshiriki mpaka ilipitishwa bungeni ila badala ya kusoma nilichoandika wao wakawa wanaangalia picha ya kwa nini rais amesimama hivyo, wakati maudhui ya nakala kupita ilikuwa muhimu sana na itabadilisha maisha ya vijana wengi Afrika.

Si kila kitu ni utani katika mitandao ya kijamii​

nn

CHANZO CHA PICHA,DIANA
Maoni ambayo vijana wengi wanayatoa katika mtandao ya kijamii ndiyo sababu kubwa ya vijana wengi, kuchukulia kila kitu ni utani.
Hata wakati nilipopata nafasi hii ya AU nilikuwa mtanzania peke yangu, hii ni kwa sababu vijana wengi hawajui kwamba kuna fursa nyingi mtandaoni. Huwa inategemea kile ambacho unakifuata mtandaoni, ila iwapo unafuatilia habari au fursa za vijana, ukiamka asubuhi unaona waridi wa BBC, fursa za wanawake lakini vijana wengi wanapenda kufuatilia umbea yaani udaku, yani hizi kurasa za udaku zina wafuatiliaji wengi sana vijana nchini Tanzania.
Ukiangalia kitu ndiyo kinakushawishi, ukiwa unafuatilia burudani tu basi masuala ya maendeleo yanakupita.
Ukiamka asubuhi ukijaza akili yako na masuala ya udaku ni ngumu kupenya kwenye majukwaa ya kimataifa ndiyo unakuta wengi ni Wakenya.
Mimi si kwa sabau ni binti ila nina vigezo vyote vya kupata nafasi, na naitumia vizuri hiyo fursa.
Mashirika ya kimataifa hayaangalii hayo mambo ya wewe mwanamke bali ni kazi umefanyaje au unafanyaje.
Tukiwa tunaoongelea masuala ya kijinsia tuwe makini sana, Diana anafanya kazi nzuri ndiyo maana kapata fursa fulani si kwa sababu ana muonekano huu.
Nilivyokuwa mdogo nilikuwa sipendi macho yangu ila sasa nimekuwa ninasifiwa kwa sababu ya macho.
n

CHANZO CHA PICHA,DIANA

Vijana tuna nguvu kubwa sana​

Lengo kubwa la Umoja wa Afrika ni kupata Afrika tunayoitaka Agenda 2063 yani kama nikitaka kwenda DRC nisihitaji hati ya kusafiria.
Natamani vijana tungeweza kutumia lugha ya Kiswahili kuwa na Afrika tunayoitaka.
Lugha inaweza kutumika kutenganisha au kujumuisha watu..
Natamani lengo la kujumuisha Afrika, umoja wa Afrika lifanikiwe katika lugha na hatua ya kukithibitisha Kiswahili kama lugha rasmi ni hatua kubwa.
Ila vijana watambue kuwa wao ni watu muhimu sana katika mabadiliko ya bara la Afrika.
Si vijana wote wanaweza kuajiriwa, vyema kupewa mafunzo na kusisitizwa amani. Vijana wana nguvu sana katika bara la Afrika, tusiruhusu misingi yetu ipotoshwe na najiona baada ya miaka 10 kuna mambo mengi ambayo nitaacha alama kubwa zaidi barani afrika.

Credit: BBC SWAHILI
 
Hata yeye anajua anauza SURA tu hakuna lolote, nimejaribu kuelewa alichokuwa anaandika sikuelewa, ila nimeona anauza urembo wake tu.

Aweke makala hata moja ya kazi zake tuone kama kweli hajabebwa tu. Tuwe wakweli ana tafuta umaaraufu kwa sura hiyo.
Na urembo wenyewe anaouza sijaona hata robo ya mashangazi zangu Evelyn Salt na Kasie Mahaba Matata....
 
Back
Top Bottom