Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

........Kwanza hapo huyo mke anakuwa siyo msaidizi tena bali ni kama business partner tu hivyo ondoa kichwani suala la kumlazimisha akutii, hivi mnadhani mwanamke aliambiwa amtii mwanaume kwa misingi gani kama siyo kuhudumiwa maana huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayefurahia kutawaliwa na binadamu mwenzie asiyewajibika kwa lolote juu yake na kiuhalisia ukitoa huduma zinazohusisha pesa hakuna wajibu mwingine mwanaume alionao juu ya mwanamke.......
Mfumo dume ni mfumo wa kimbingu, 59/50=1 ni mfumo wa kishetani, humo ndo kuna ushoga, usagaji na mambo mengine ya kishenzi. Sababu unajaribu kuondoa utofauti kati ya mwanaume na mwanamke. Wote wakiwa sawa kila mtu anaweza kuwa mwanamke at the sametime akawa mwanaume
 
Hivi hawa viumbe wanaosema 50/50 wanajua kweli nini wanaka ama kisa tu mtu una bando na simu unamua kupost.?

Hivi ikitokea vita leo kwa mfano, hapa tz itakuwepo hiyo 50/50 au ndo yale yale ya Ukraine kwamba hivi viumbe vidai usawa na watoto huwa huondolewa kwanza na hapo hutoskia huu ujinga wa usawa wala nn

Majambazi wajika kwako usiku kuvamia kwa unavosema 50/50 je utakomaa nao kiume au ndo yale yale ya kupiga kelele kuomba msaada

hizi idea za ki feminist sina waponzaga sana, kifupi hamjielewi wengi wenu mna copy na kupaste ideology bila kuweza kudadavua uhalisia, alafu ndo uje useme unaweza kujisimamia.

Be logical hasa kwenye mada senstive kama hizi, usilete hisia as hivi viwili havichanganywi.

Povu ruksa
 
Hahaha we mzee wa vina hilo ndiyo suluhisho la kupunguza vilio vya wanaume kuhusu wanawake, lazima tuangalie tunakosea wapi siyo kila kitu tunakimbilia kuwatupia lawama wanawake, ni lazima tukubaliane na hali halisi vinginevyo tuendelee kulalamika tu hadi mwisho wa dahari
Kama lengo ni kuangalia wapi kosa limefanyika basi wakufanya hivyo ni sisi wanaume

Wanaume ndio tulifanya kosa kuwapeni uhuru uliopitiliza (tukiamini kufanya hivyo ni upendo) mpaka sasa uhuru huo unaenda kuwa silaha inayoturudia wenyewe.
 
Ndio, kuna msemo unasema "with great authority comes great responsibility" yani kila mamlaka makubwa huambatana na majukumu makubwa, lakini jambo la kushangaza ni kwamba wanaume wengi hasa wa kiafrika wanayataka hayo mamlaka tu ila majukumu hawayataki

Mimi naona ifike pahala dunia iachane rasmi na mfumo dume na haki sawa ishike hatamu, kwa sababu wanaume hawataki tena majukumu hivyo hata hayo mamlaka hayawafai, wanaume wengi hawataki haki sawa ila wanataka majukumu sawa tena ikibidi mwanamke ndio afanye zaidi ya mwanaume

MImi naona kusiwe tena na mgawanyo wa majukumu yani hata kazi za nyumbani zifanywe na wote kama ambavyo kutafuta pesa limekuwa ni jukumu la wote, majukumu ya mwanamke yabaki yale ya asili na ya kimaumbile tu ambayo ni kubeba ujauzito, kuzaa na kunyonyesha, hayo tu ndio ambayo mwanaume hawezi kuyafanya ila majukumu mengine yote ya nyumbani kama kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumba, kulea watoto tangu wakiwa wachanga mfano kuwasafisha, kuwauguza wakiumwa, nk yafanywe na wote kwa usawa kabisa

Na vile vile kwa mfano mume akiweka laki mezani na mke naye aweke laki mezani mahitaji yote ya nyumbani wanunue kwa usawa bills zote walipe kwa usawa, na watoto wao wawahudumie kwa usawa ikiwemo kuwalipia ada na mahitaji yao mengine yote kwa usawa, hiyo ndio maana halisi ya 50 50 siyo mmoja anamtegea mwenzie eti mtu anataka pesa mtafute wote na bills mlipe wote, ila kazi za nyumbani na kulea watoto afanye mmoja na bado huyo mmoja amtii mwenzie na amlee kama anavyowalea watoto wake, what kind of cockamamie logic is this

Na jambo jingine naona pia tuachane na suala la mwanaume kumtawala mwanamke kila mtu ajitawale mwenyewe kusiwe na habari za kichwa cha familia, yani hakuna tena kusema kwamba mwanamke anatakiwa amtii mumewe kila mtu awe na maamuzi juu ya maisha yake mwenyewe, kusiwe na wa kumuongoza mwenzake na pia kusiwe na habari za kuoa wala kuolewa tena bali iwe ni kuoana

Mnawalaumu wanawake kuwa wanadai haki sawa halafu hawataki majukumu lakini mnasahau kwamba sababu ya wao kukataa hayo majukumu ni kwa sababu mnataka wafanye yale ya kwenu tu, ila ya kwao bado mmewaachia wenyewe hamtaki kuyafanya yani huwezi kumuambia mwanamke ajitafutie pesa zake na akusaidie majukumu, halafu hapo hapo bado unataka huyo mwanamke akufanyie majukumu ya nyumbani na bado akupe heshima na utii

Kwanza hapo huyo mke anakuwa siyo msaidizi tena bali ni kama business partner tu hivyo ondoa kichwani suala la kumlazimisha akutii, hivi mnadhani mwanamke aliambiwa amtii mwanaume kwa misingi gani kama siyo kuhudumiwa maana huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayefurahia kutawaliwa na binadamu mwenzie asiyewajibika kwa lolote juu yake na kiuhalisia ukitoa huduma zinazohusisha pesa hakuna wajibu mwingine mwanaume alionao juu ya mwanamke

Kama ikiwa mtoto anamtii mzazi wake kwa sababu amemzaa na amemlea, watu wa dini wanaitii miungu yao kwa sababu wanaamini imewaumba na inawapa uhai, je mwanamke anapaswa amtii mumewe kwa sababu gani, tena hata mtoto mwenyewe akishatoka kwao akaanza kujitegemea kinachobaki kwa mzazi wake ni ile heshima tu kuwa amemzaa, lakini huyo mzazi anakuwa hana mamlaka tena ya kumpangia mtoto maisha yake mfano afanye kazi gani au arudi nyumbani muda gani kwa sababu hamhudumii tena

Sasa inashangaza pale mwanaume anapotaka mkewe atafute pesa wasaidiane maisha kwa kisingizio kwamba mke naye ana mikono miwili na miguu miwili, ila huyo huyo mwanaume haoni ajabu kumtawala huyo mke mwenye mikono miwili na miguu miwili kama yeye, yani imefikia hatua wanaume wanaona uchungu kugawana mali na wake zao na wengine ndio kabisa hawataki kuoa kwa kisingizio kwamba eti wakishafanikiwa wake zao watadai talaka ili wagawane mali

Yani hawaconsider tena yale majukumu yote ambayo wake zao wanawafanyia pamoja na utii ambao wake zao wanawapa, siku hizi wanadai kwamba kila mtu ajitafutie pesa zake na ikitokea wameachana kila mtu aondoke na chake, lakini cha kushangaza kwenye majukumu mengine hawasemi kila mtu afanye kwa usawa na kwenye suala la mamlaka hawasemi kila mtu ajitawale mwenyewe

Wale waumini wa ukristo hasa wanaume kama mmeamua kufuata maandiko basi fuateni yote, na kama mmeamua kuyapuuzia basi yapuuzieni yote msichague yale yanayowanufaisha ninyi tu halafu mengine mnajifanya hamyaoni, kwa sababu maandiko yanasema mume ndio atakula kwa jasho na si mke, halafu mbele ndio yanaendelea kwamba mwanaume atamtawala mwanamke, yule mke mnayemuota wa Mithali 31 yalikuwa mawazo binafsi ya mfalme Suleiman na si maagizo ya muumba

Hivo basi ifike pahala wanaume mchague moja kati ya mwanamke mfanyakazi/mfanyabiashara au mama wa nyumbani, na aina yoyote utakayochagua hapo lazima ukubaliane na sifa zinazoambatana na aina hiyo ya mwanamke siyo unachagua mfanyakazi/mfanyabiashara mnasaidiana majukumu, halafu hapo hapo unataka awe kama mama wa nyumbani au unachagua mama wa nyumbani halafu hutaki kumhudumia unaanza kumuona golikipa
Sasahivi mnagombea 50 zenu na mashoga
 
Iko hivi mwanamke mwenye pesa kukuzidi au mkalingana huyo kidume mwenzio, hapo ndani kuna njemba mbili, hapakaliki tena.

Mwanamke hapaswi kukuzidi kipato.

Mwanamke hapaswi kukuzidi elimu.

Mwanamke hapaswi kukuzidi umri.

Mwanaume ameumbwa kutii na sio kuheshimu, kuheshimu tunaheshimu mzazi tu labda, ila siwezi heshimu mwanaume mwenzangu. Ndio jeshini ukiona mwanaume anapewa adhabu na anafanya huo ni utii si heshima.

Mwanamke kaumbwa kuheshimu na kutii, amheshimu mumewe na kumtii.

Kwenye ndoa mwanamke apendwe, mwanaume aheshimiwe, hio ni asili huwezi badilisha.

Unachozungumza ni kama kusema wanaume na wanawake wote tufanane maumbile, wote tuwe na misambwanda, wote tubebe mimba, wote tuvae shimizi..

Wanawake hamuwezi haki sawa, mtaongea tu, lakini majukumu usawa kwa usawa na mwanaume yupo hamuwezi, mtaanza kutegea tu.

Mfumo dume uendelee, tena sasa hivi msiajiriwe kabisa mkae nyumbani.
Haki sawa inahubiriwa kwenye vitu simple

Hususani kwenye mgawanyo wa mali ndio sera hii inatumika sana.

Kwenye mambo magumu hili swala halipo na hata wao wanajua.

50/50 ni myths ya wanaharakati wa mitandaoni wala haipo applied mitaani.

Dada zetu wanaamini huo ndio mfumo uliokuja kumuokoa mwanamke lakini binafsi naona majibu ni tofauti.

Mwanaume akiwa na hela wakivunja ndoa na mkewe utasikia 50/50 kwenye mali.

Mwanamke mwenye hela akiolewa na na mwanaume choka mbaya then ndoa ikavunjika, mwanaume ataondoka kama alivyokuja. Hapo hakuna tena 50/50.
 
Haki sasa inahubiriwa kwenye vitu simple

Kabisa.
Hata nchi za Ulaya na Amerika ambapo ndugu zetu hawa wanatolea mifano 50-50 wanatumia katika baadhi ya majukumu tu kwenye kulipa bill, kazi za nyumbani n.k...

Lakini ikitokea vita 50-50 haipo, wanaume ndio wapo front kumaliza, wanawake wapo lakini sio kama wanaume.
 
Mkuu nafikiri hayo ulitakiwa uwaambie wanaume wenzio kwamba wanaposema wanawake nao watafute pesa wasiwe ombaomba huwa wanamaanisha nini,

Ndio maana mwishoni nikamalizia kwa kusema lazima mwanaume achague mwanamke wa aina moja, kati ya hizo aina mbili na akubaliane na sifa za kila aina ya mwanamke, asilazimishe mwanamke wa aina fulani awe na sifa za mwanamke wa aina nyingine

Hapo kwenye suala la kutegea labda nikuulize swali hivi laiti kama tungeamua kuswitch majukumu kwa muda fulani, ya mwanaume afanye mwanamke na ya mwanamke afanye mwanaume unahisi ni nani atakuwa wa kwanza kusurrender, unaweza kulinganisha idadi ya wanawake wanaotafuta pesa na idadi ya wanaume wanaofanya kazi za nyumbani kila siku (achilia mbali wale wanaojifanya wanasaidia wake zao mara moja moja tena ni hadi waumwe)
Kazi za nyumbani ndio kigezo kikubwa cha kutaka 50/50?

Nikatika tu kufikiria wapi kuna huo ugumu kwenye hizo kazi za nyumbani. (Maana hata kabla hajakuoa naye hizo kazi alikuwa akifanya)

So labda uniambie

Inawezekana home kila siku lazima ujaze Simtank la lita 10,000 za maji, maji ambayo unayafuata kilomita 30 kwa mguu tena ukiwa peku kwenye njia yenye miba, majabali na miamba kiasi kazi hizo zionekane ngumu kwako?

Au kwenye kupiga deki huwa unapiga deki stadium kama ya Mkapa?
 
Mfumo dume ni mfumo wa kimbingu, 59/50=1 ni mfumo wa kishetani, humo ndo kuna ushoga, usagaji na mambo mengine ya kishenzi. Sababu unajaribu kuondoa utofauti kati ya mwanaume na mwanamke. Wote wakiwa sawa kila mtu anaweza kuwa mwanamke at the sametime akawa mwanaume
Yaan siku hizi kila kitu, lazima lawama utupiwe ushoga.
Hebu muupumzishe bas, suala hapa ni mwanamke na mwanaume walio ktk ndoa, sasa ushoga unakujajee??
 
........Kwanza hapo huyo mke anakuwa siyo msaidizi tena bali ni kama business partner tu hivyo ondoa kichwani suala la kumlazimisha akutii, hivi mnadhani mwanamke aliambiwa amtii mwanaume kwa misingi gani kama siyo kuhudumiwa maana huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayefurahia kutawaliwa na binadamu mwenzie asiyewajibika kwa lolote juu yake na kiuhalisia ukitoa huduma zinazohusisha pesa hakuna wajibu mwingine mwanaume alionao juu ya mwanamke.......
Nonesense
 
Kabisa.
Hata nchi za Ulaya na Amerika ambapo ndugu zetu hawa wanatolea mifano 50-50 wanatumia katika baadhi ya majukumu tu kwenye kulipa bill, kazi za nyumbani n.k...

Lakini ikitokea vita 50-50 haipo, wanaume ndio wapo front kumaliza, wanawake wapo lakini sio kama wanaume.
Wakati vita ya Ukraine inaanza nilisikia raisi wa Ukraine akitoa tamko kuwa wanawake na wazee wote wasafirishwe kupisha vita.

Mimi nikahoji kwanini wale wanaharakati wa haki za wanawake wakae kimya huku haki ya mwanamke ya kuoigana vita ikidhulumiwa?

Kwanini wasijitokeze na sera yao ya 50/50 kwa msukumo uleule ambao tumekuwa tukiwaona kwenye mambo ya mgawanyo wa mali nk?

Na wanawake wenyewe kwanini walikuwa kimya kuona haki zao zinadhulumiwa?

Hata humu JF sikuona feminist yeyote akilaani kile kitendo.

Sasa kama hapo nini maana ya 50/50 kama kwenye mambo magumu wanawake wanawekwa nyuma?
 
Hiyo 50-50 unaitaka katika familia yako pekee au dunia nzima na katika kila kitu? Kama ni katika familia yako haina tatizo ila ni kama ulivyoandika kwenye title ya uzi wako, I have bad news for you, ni kila kitu kitacollapse na ulimwengu wote utashindwa kua normal.

50-50 inaweza kua achieved katika household tena inategemea na aina ya mwanaume uliye naye ila katika overall life situation ya sasa haiwezekani na haitokuja kuwezekana na sababu kuu ya kutokuwezekana ni huyo huyo mwanamke.
50/50 maana yake fursa sawa kwa jinsia ya ke na me kielimu , nakadhalika haina maana nyingine sema watu hawaelewagi wanachukua maneno ya vijiweni kuwa mwanamke kuwa sawa na mwanaume kitu ambacho sio kweli.
 
Ndio, kuna msemo unasema "with great authority comes great responsibility" yani kila mamlaka makubwa huambatana na majukumu makubwa
Actually: With great responsibility comes great authority (powers)

Kiotomati yule anayewajibika kwa watu wengi zaidi, au kwa jukumu kubwa zaidi popote ndiye anayekuwa na uwezo mkubwa.

Ilikuwa na bado ni kweli kabisa ilipoandikwa:

"Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;"

Na sasa uliyoyaongea kwenye zote hasa ya mwisho ni bonge la logic. Ni kama simu tu, kila mmoja achague profile anayoipenda na anayoendana nayo na aishi nayo kikamilifu. Sio mtu achague silent halafu atake akipigiwa iite kwa mziki wa reggae aliouchagua whata aa......

"bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; " so yule anayefanya kazi kubwa zaidi kuijenga hiyo familia na awe kiongozi. Na kama wote wanafanya kazi sawa basi wawe partners
 
Ndio, kuna msemo unasema "with great authority comes great responsibility" yani kila mamlaka makubwa huambatana na majukumu makubwa, lakini jambo la kushangaza ni kwamba wanaume wengi hasa wa kiafrika wanayataka hayo mamlaka tu ila majukumu hawayataki

Mimi naona ifike pahala dunia iachane rasmi na mfumo dume na haki sawa ishike hatamu, kwa sababu wanaume hawataki tena majukumu hivyo hata hayo mamlaka hayawafai, wanaume wengi hawataki haki sawa ila wanataka majukumu sawa tena ikibidi mwanamke ndio afanye zaidi ya mwanaume

MImi naona kusiwe tena na mgawanyo wa majukumu yani hata kazi za nyumbani zifanywe na wote kama ambavyo kutafuta pesa limekuwa ni jukumu la wote, majukumu ya mwanamke yabaki yale ya asili na ya kimaumbile tu ambayo ni kubeba ujauzito, kuzaa na kunyonyesha, hayo tu ndio ambayo mwanaume hawezi kuyafanya ila majukumu mengine yote ya nyumbani kama kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumba, kulea watoto tangu wakiwa wachanga mfano kuwasafisha, kuwauguza wakiumwa, nk yafanywe na wote kwa usawa kabisa

Na vile vile kwa mfano mume akiweka laki mezani na mke naye aweke laki mezani mahitaji yote ya nyumbani wanunue kwa usawa bills zote walipe kwa usawa, na watoto wao wawahudumie kwa usawa ikiwemo kuwalipia ada na mahitaji yao mengine yote kwa usawa, hiyo ndio maana halisi ya 50 50 siyo mmoja anamtegea mwenzie eti mtu anataka pesa mtafute wote na bills mlipe wote, ila kazi za nyumbani na kulea watoto afanye mmoja na bado huyo mmoja amtii mwenzie na amlee kama anavyowalea watoto wake, what kind of cockamamie logic is this

Na jambo jingine naona pia tuachane na suala la mwanaume kumtawala mwanamke kila mtu ajitawale mwenyewe kusiwe na habari za kichwa cha familia, yani hakuna tena kusema kwamba mwanamke anatakiwa amtii mumewe kila mtu awe na maamuzi juu ya maisha yake mwenyewe, kusiwe na wa kumuongoza mwenzake na pia kusiwe na habari za kuoa wala kuolewa tena bali iwe ni kuoana

Mnawalaumu wanawake kuwa wanadai haki sawa halafu hawataki majukumu lakini mnasahau kwamba sababu ya wao kukataa hayo majukumu ni kwa sababu mnataka wafanye yale ya kwenu tu, ila ya kwao bado mmewaachia wenyewe hamtaki kuyafanya yani huwezi kumuambia mwanamke ajitafutie pesa zake na akusaidie majukumu, halafu hapo hapo bado unataka huyo mwanamke akufanyie majukumu ya nyumbani na bado akupe heshima na utii

Kwanza hapo huyo mke anakuwa siyo msaidizi tena bali ni kama business partner tu hivyo ondoa kichwani suala la kumlazimisha akutii, hivi mnadhani mwanamke aliambiwa amtii mwanaume kwa misingi gani kama siyo kuhudumiwa maana huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayefurahia kutawaliwa na binadamu mwenzie asiyewajibika kwa lolote juu yake na kiuhalisia ukitoa huduma zinazohusisha pesa hakuna wajibu mwingine mwanaume alionao juu ya mwanamke

Kama ikiwa mtoto anamtii mzazi wake kwa sababu amemzaa na amemlea, watu wa dini wanaitii miungu yao kwa sababu wanaamini imewaumba na inawapa uhai, je mwanamke anapaswa amtii mumewe kwa sababu gani, tena hata mtoto mwenyewe akishatoka kwao akaanza kujitegemea kinachobaki kwa mzazi wake ni ile heshima tu kuwa amemzaa, lakini huyo mzazi anakuwa hana mamlaka tena ya kumpangia mtoto maisha yake mfano afanye kazi gani au arudi nyumbani muda gani kwa sababu hamhudumii tena

Sasa inashangaza pale mwanaume anapotaka mkewe atafute pesa wasaidiane maisha kwa kisingizio kwamba mke naye ana mikono miwili na miguu miwili, ila huyo huyo mwanaume haoni ajabu kumtawala huyo mke mwenye mikono miwili na miguu miwili kama yeye, yani imefikia hatua wanaume wanaona uchungu kugawana mali na wake zao na wengine ndio kabisa hawataki kuoa kwa kisingizio kwamba eti wakishafanikiwa wake zao watadai talaka ili wagawane mali

Yani hawaconsider tena yale majukumu yote ambayo wake zao wanawafanyia pamoja na utii ambao wake zao wanawapa, siku hizi wanadai kwamba kila mtu ajitafutie pesa zake na ikitokea wameachana kila mtu aondoke na chake, lakini cha kushangaza kwenye majukumu mengine hawasemi kila mtu afanye kwa usawa na kwenye suala la mamlaka hawasemi kila mtu ajitawale mwenyewe

Wale waumini wa ukristo hasa wanaume kama mmeamua kufuata maandiko basi fuateni yote, na kama mmeamua kuyapuuzia basi yapuuzieni yote msichague yale yanayowanufaisha ninyi tu halafu mengine mnajifanya hamyaoni, kwa sababu maandiko yanasema mume ndio atakula kwa jasho na si mke, halafu mbele ndio yanaendelea kwamba mwanaume atamtawala mwanamke, yule mke mnayemuota wa Mithali 31 yalikuwa mawazo binafsi ya mfalme Suleiman na si maagizo ya muumba

Hivo basi ifike pahala wanaume mchague moja kati ya mwanamke mfanyakazi/mfanyabiashara au mama wa nyumbani, na aina yoyote utakayochagua hapo lazima ukubaliane na sifa zinazoambatana na aina hiyo ya mwanamke siyo unachagua mfanyakazi/mfanyabiashara mnasaidiana majukumu, halafu hapo hapo unataka awe kama mama wa nyumbani au unachagua mama wa nyumbani halafu hutaki kumhudumia unaanza kumuona golikipa
Hahahahahaha..mnavyopenda kitonga hamuwezi hii kitu
 
Back
Top Bottom