Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,259
- 86,054
Ndio, kuna msemo unasema "with great authority comes great responsibility" yani kila mamlaka makubwa huambatana na majukumu makubwa, lakini jambo la kushangaza ni kwamba wanaume wengi hasa wa kiafrika wanayataka hayo mamlaka tu ila majukumu hawayataki
Mimi naona ifike pahala dunia iachane rasmi na mfumo dume na haki sawa ishike hatamu, kwa sababu wanaume hawataki tena majukumu hivyo hata hayo mamlaka hayawafai, wanaume wengi hawataki haki sawa ila wanataka majukumu sawa tena ikibidi mwanamke ndio afanye zaidi ya mwanaume
MImi naona kusiwe tena na mgawanyo wa majukumu yani hata kazi za nyumbani zifanywe na wote kama ambavyo kutafuta pesa limekuwa ni jukumu la wote, majukumu ya mwanamke yabaki yale ya asili na ya kimaumbile tu ambayo ni kubeba ujauzito, kuzaa na kunyonyesha, hayo tu ndio ambayo mwanaume hawezi kuyafanya ila majukumu mengine yote ya nyumbani kama kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumba, kulea watoto tangu wakiwa wachanga mfano kuwasafisha, kuwauguza wakiumwa, nk yafanywe na wote kwa usawa kabisa
Na vile vile kwa mfano mume akiweka laki mezani na mke naye aweke laki mezani mahitaji yote ya nyumbani wanunue kwa usawa bills zote walipe kwa usawa, na watoto wao wawahudumie kwa usawa ikiwemo kuwalipia ada na mahitaji yao mengine yote kwa usawa, hiyo ndio maana halisi ya 50 50 siyo mmoja anamtegea mwenzie eti mtu anataka pesa mtafute wote na bills mlipe wote, ila kazi za nyumbani na kulea watoto afanye mmoja na bado huyo mmoja amtii mwenzie na amlee kama anavyowalea watoto wake, what kind of cockamamie logic is this
Na jambo jingine naona pia tuachane na suala la mwanaume kumtawala mwanamke kila mtu ajitawale mwenyewe kusiwe na habari za kichwa cha familia, yani hakuna tena kusema kwamba mwanamke anatakiwa amtii mumewe kila mtu awe na maamuzi juu ya maisha yake mwenyewe, kusiwe na wa kumuongoza mwenzake na pia kusiwe na habari za kuoa wala kuolewa tena bali iwe ni kuoana
Mnawalaumu wanawake kuwa wanadai haki sawa halafu hawataki majukumu lakini mnasahau kwamba sababu ya wao kukataa hayo majukumu ni kwa sababu mnataka wafanye yale ya kwenu tu, ila ya kwao bado mmewaachia wenyewe hamtaki kuyafanya yani huwezi kumuambia mwanamke ajitafutie pesa zake na akusaidie majukumu, halafu hapo hapo bado unataka huyo mwanamke akufanyie majukumu ya nyumbani na bado akupe heshima na utii
Kwanza hapo huyo mke anakuwa siyo msaidizi tena bali ni kama business partner tu hivyo ondoa kichwani suala la kumlazimisha akutii, hivi mnadhani mwanamke aliambiwa amtii mwanaume kwa misingi gani kama siyo kuhudumiwa maana huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayefurahia kutawaliwa na binadamu mwenzie asiyewajibika kwa lolote juu yake na kiuhalisia ukitoa huduma zinazohusisha pesa hakuna wajibu mwingine mwanaume alionao juu ya mwanamke
Kama ikiwa mtoto anamtii mzazi wake kwa sababu amemzaa na amemlea, watu wa dini wanaitii miungu yao kwa sababu wanaamini imewaumba na inawapa uhai, je mwanamke anapaswa amtii mumewe kwa sababu gani, tena hata mtoto mwenyewe akishatoka kwao akaanza kujitegemea kinachobaki kwa mzazi wake ni ile heshima tu kuwa amemzaa, lakini huyo mzazi anakuwa hana mamlaka tena ya kumpangia mtoto maisha yake mfano afanye kazi gani au arudi nyumbani muda gani kwa sababu hamhudumii tena
Sasa inashangaza pale mwanaume anapotaka mkewe atafute pesa wasaidiane maisha kwa kisingizio kwamba mke naye ana mikono miwili na miguu miwili, ila huyo huyo mwanaume haoni ajabu kumtawala huyo mke mwenye mikono miwili na miguu miwili kama yeye, yani imefikia hatua wanaume wanaona uchungu kugawana mali na wake zao na wengine ndio kabisa hawataki kuoa kwa kisingizio kwamba eti wakishafanikiwa wake zao watadai talaka ili wagawane mali
Yani hawaconsider tena yale majukumu yote ambayo wake zao wanawafanyia pamoja na utii ambao wake zao wanawapa, siku hizi wanadai kwamba kila mtu ajitafutie pesa zake na ikitokea wameachana kila mtu aondoke na chake, lakini cha kushangaza kwenye majukumu mengine hawasemi kila mtu afanye kwa usawa na kwenye suala la mamlaka hawasemi kila mtu ajitawale mwenyewe
Wale waumini wa ukristo hasa wanaume kama mmeamua kufuata maandiko basi fuateni yote, na kama mmeamua kuyapuuzia basi yapuuzieni yote msichague yale yanayowanufaisha ninyi tu halafu mengine mnajifanya hamyaoni, kwa sababu maandiko yanasema mume ndio atakula kwa jasho na si mke, halafu mbele ndio yanaendelea kwamba mwanaume atamtawala mwanamke, yule mke mnayemuota wa Mithali 31 yalikuwa mawazo binafsi ya mfalme Suleiman na si maagizo ya muumba
Hivo basi ifike pahala wanaume mchague moja kati ya mwanamke mfanyakazi/mfanyabiashara au mama wa nyumbani, na aina yoyote utakayochagua hapo lazima ukubaliane na sifa zinazoambatana na aina hiyo ya mwanamke siyo unachagua mfanyakazi/mfanyabiashara mnasaidiana majukumu, halafu hapo hapo unataka awe kama mama wa nyumbani au unachagua mama wa nyumbani halafu hutaki kumhudumia unaanza kumuona golikipa