Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,719
- 5,368
Naandika waraka huu mfupi nikitambua kuwa kuna watu leo katika Nchi hii hawataki kusikia mawazo mbadala wala kukosolewa kwa mwenendo wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Mhe.Rais Magufuli chukua muda sikiliza pia mawazo mbadala kutoka kwa watu ambao hawakusifii tu!
Mhe.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekiri katika kitabu chake cha My Life, My Purpose kuwa kuna "wahuni" walimpotosha!
Lakini kumbuka alikuwa bingwa wa kuita wenye mawazo tofauti na yeye Wavivu wa kufikiri, leo yako wapi?!
Mhe.Rais Kikwete amelifanyia Taifa hili mambo mengi pia mazuri tena kwa unyenyekevu na uungwana wa hali ya juu!
Wakati wake kuna wapambe nuksi walikuwa hawawezi kumuita Mhe.Kikwete bila kuanza na neno "Dakta" tena kwa mbwembwe kweli! leo neno "Dakta" wamelisahau kabisa!
Hata wewe Mhe.Rais wetu Dr. Magufuli umezungukwa na wachumia tumbo wengi kweli ambao hawakwambii ukweli!
Wanajitahidi sana kutaja majina yako yote manne tena kwa mbwembwe ila wengine tunajua tu ni unafiki wa kutengenezea Ugali.
Kama unadhani nasema uongo Mhe.Rais Magufuli naomba uniwie radhi lakini nakuhakikishia tukiwa hai hapo utakapo kabidhi kijiti cha Urais pengine ukawa Rais Mstaafu utakayebezwa kuliko wenzako wote!
Na hata hawa wachumia tumbo uliowapa nafasi wanashindana kukutaja muda wote kwa majina manner(4) ya " Dokta John Pombe Joseph Magufuli" watapungua sana ama hutawasikia kabisa, na hata huko Chato hutawaona kabisa!
Ninatoa ushauri huu nikiamini kuwa viongozi tunapowachagua ni katika dhana ya kuwatanguliza mbele ili muongoze njia lakini si kwamba nyie mnajua kila kitu na mna hatimiliki ya kuhodhi mawazo na ubunifu wa kila jambo !
Mhe.Rais Dr.Magufuli hebu jaribu kuangalia kwamba Mfumo wako wa Utawala umeziua Halmashauri za miji,majiji na manispaa! ( ugatuzi wa madaraka haupo) ,kila kitu ni wewe tu ndo mpaka uamue!
Hii si sawa Tanzania ni Nchi kubwa! na Wananchi wanapaswa kujiamulia mambo yao kwa upana! Mwl.Nyerere alisisitiza sana umuhimu wa Serikali za Mitaa zenye Nguvu!
Hivi karibuni umepiga marufuku Wakurugenzi wasikope wasubiri Serikali iwape pesa za kujiendesha, hii si sawa unachelewesha maendeleo!
Pendekezo langu kwako ni kuwa rejesha Wizara ya TAMISEMI chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ,maana hata Waziri Mkuu kwa sasa ni sawa tu na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum!
Kingine Mhe.Rais Dr.Magufuli tambua kuwa popote Duniani Serikali ndiye mchezeshaji Mkuu wa Uchumi katika Nchi husika!
Leo wewe mifumo yako ya uendeshaji wa Nchi inaua sekta binafsi ( Private sector) na hata Ma- Guru wa sekta Binafsi wanaondoka nayo ( refer Mzee Mengi na Ali Mufuruki).These Guys knew the truth na perhaps wamemezwa na Depression tu!
Leo kuna vitu kama "Force Account" ,NHC,TBA na Suma JKT ndio Contractors wanaofanya kazi za Serikali!
Mhe.Rais watu wako watapata fedha kutoka wapi na kwa kazi zipi?
Rais Barack Obama alivyoingia madarakani nchini Marekani wakati wa recession alichofanya ni kuingiza fedha mitaani kupitia kufufua miradi mikubwa ya ujenzi na kupunguza budget za Vita ya Afghanistan na Iraq.
Wachumia tumbo waliokuzunguka wanakudanganya Mhe.Rais wetu,hawakuambii ukweli!
Uendeshaji wako wa Nchi unawafukarisha Watanzania wengi!
Mhe.Rais Dr.Magufuli kuhusu uchapaji kazi wako sijawahi kuwa na mashaka nawe hata kidogo.Wewe ni mchapakazi kweli kweli na kwa hili vizazi vingi katika Taifa hili vitakukumbuka Mzee.
Ila kwenye eneo la uzalishaji ( productivity) nina mashaka sana na taarifa tunazopewa na Serikali yako!
Umenunua Ndege, Unajenga Reli,Unajenga Stiglers Gorge na Structures kibao zingine na unasema kwa fedha za Ndani!
Fedha za Ndani zipi? Mbona Deni la Taifa tunaambiwa ulikuta ni Trillion 29 na leo limepanda hadi Trillion 52!
Kwanini Deni hilo lipande kama kuna uzalishaji na uwekezaji wa maana?!
Maana kuongezeka kwa uzalishaji na uwekezaji ndo kuongezeka kwa mapato (Kodi) ya Serikali ambayo tungesema ndiyo unatumia kujenga hiyo miundombinu!
Kuongezeka kwa Deni la Taifa ni kielelezo cha kutokuwepo kwa ongezeko katika uzalishaji na uwekezaji na matokeo yake ndo ukosefu wa ajira tunaouona katika kipindi chako!
Sekta binafsi imekufa na haiwezi kuajiri na pia Serikali yako haiajiri japo kuna matamko eti Rais kasema waajiriwe elfu 40!
Mhe.Rais hutakiwi wewe useme watu waajiriwe kanuni za uchumi uzungumza zenyewe!
Automatically waajiriwa huuitajika pale uchumi unapo- perform!
Mhe.Rais Dr.Magufuli niwie radhi nirudie kauli ya yule Mtanzania pale Igunga!
Mhe.Rais ACHIA HELA! Serikali yako imeua Liquidity katika Mabenki! Rudisha fedha kwenye commercial banks toka BOT ili watu wakopeshwe wafanye kazi!
Watu wenye nguvu sasa wameamua kukaa vijiweni wanapiga soga,wana bet n.k hakuna mitaji!
Naomba kwa leo niishie hapa Mhe.Rais.
Mhe.Rais Dr.Magufuli nakutakia wewe pamoja na Mama yetu mpendwa Mama Janet Magufuli heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2020.