Michael Jackson ni mmoja ya watu wenye akili sana waliopata kuzaliwa Duniani

Huyu mshikaji sio wa kawaida mkuu...hua naangali performances zake youtube,aisee ni unheard of...

Kuna wapumb.avu wanasema sijui Beyonce ana live performance more than anyone in history,nikasema inabidi wakapimwe akili seriously...

Michale Jackson>>>>>>>>>>>>>Beyonce and the rest of em niggaz...

No one like michael
 
Wasomi wengi wanapoangalia suala la akili kuna vitu wanasahau. kuwa kuna multiple intelligence. or variety of intelligence. unaweza ukawa na akili ya darasani au akili ya uwanjani ikiwa umchezaji wa mchezo flan.

Michael Jackson alikuwa na akili ambayo wakati mwingine watu wanaamua kuita kipaji. ukiangalia music aliokuwa akiimba na kucheza michael jackson utagundua kuwa alikuwa anatumia akili nyingi sana kuuandaa na kufaham aucheze vipi. Angalia namna ambavyo majukwaa yake yalikuwa yanaandaliwa. wakati flan mpaka kifaru kilikuwa kinaletwa jukwaani.

Angalia tamasha alilolifanya live huko munich ujeruman. wajeruman maelfu walifurika jukwaani wengi wao hata english hawakuwa wakiijua lakini waliimba naye, wengine walizimia kwa hisia, walilia kwa kusikiliza tu maneno ambayo hawakuwa wakijua maana yake. lakini namna alivyokuwa akicheza na kuonesha hisia zake kwenye maneno hayo nao pia walikuwa wakijihisi wanaelewa na kusikia ile hali aliyokuwa akiisikia.

Hii ni kutokana na utunzi wa kiakili na uimbaji pia. utaona pia katika tamasha hilo jinsi ambavyo aliandaa mpaka kifaru kuja jukwaani na mazingira mbalimbali katika wimbo wake wa "What about us"

Akili si walikuwa nazo akina Aristotle,Socrates,Archimedes, Einstein etc. tukiangalia kwa upande huu mwingine pia ni akili nyingi zilitumika kwa yeye kuweza kuteka nyoyo za watu namna ile. kama ni mtu mwenye kuamini ushirikina ungesema aliwaroga ndio maana alipendwa kila sehemu.

Sikiliza mashairi ya nyimbo zake. kama huna akili huwezi tunga mashairi yale. angalia video zake. ambazo pia zilikuwa na maelekezo yake mengi anataka video iweje. Hii yote ni akili. wadau tunapowaza suala la akili tusiangalie upande mmoja tukasahau kila mtu ana akili zake kwa eneo lake.

Aina yake ya uchezaji ambayo ilikuwa ni ya kimapinduzi ni uvumbuzi alioufanya ukiangalia ile style ya moon walker au angalia ule ubunifu wa kwenye wimbo wa smooth criminal pale inapoonekana ameweza kuishinda gravitational force.

Anaenda mwili mzima yeye na wachezaj wake na kurudi pasipo kuanguka. umejiuliza aulitumia mbinu gani? Huoni kama hiyo ni akili kwa lolote alilolifanya?

Tumkumbuke kama mmoja ya watu waliokuwa na akili na wenye mchango wa kipekee hapa duniani. Kwa kupitia music wake wengi walikuwa motivated kuimba na kucheza na wengi waliburudishwa na kuelimishwa.
Hata we pia kuwaza mambo kama haya ni akili umeitumia vema. umemuelezea kitaalamu sana, hongera sana mkuu.
 
sawa lkn hao watu mbona hawajafanya kwa wengine? ndio tunajua kuwa alikuwa na team kubwa ya watu wengi katika kufanikisha hizo shughuli, lkn sifa bado tunampa mwenye team.Hongera sana Michael r.i.p the wacko
 
Kuna Wamebarikiwa hadi wanakera kama huyu Michael Jackson!! Hata uige vipi bado humuwezi!!

Pumzika kwa Amani ndugu Michael Jackson
 
Wasomi wengi wanapoangalia suala la akili kuna vitu wanasahau. kuwa kuna multiple intelligence. or variety of intelligence. unaweza ukawa na akili ya darasani au akili ya uwanjani ikiwa umchezaji wa mchezo flan.

Michael Jackson alikuwa na akili ambayo wakati mwingine watu wanaamua kuita kipaji. ukiangalia music aliokuwa akiimba na kucheza michael jackson utagundua kuwa alikuwa anatumia akili nyingi sana kuuandaa na kufaham aucheze vipi. Angalia namna ambavyo majukwaa yake yalikuwa yanaandaliwa. wakati flan mpaka kifaru kilikuwa kinaletwa jukwaani.

Angalia tamasha alilolifanya live huko munich ujeruman. wajeruman maelfu walifurika jukwaani wengi wao hata english hawakuwa wakiijua lakini waliimba naye, wengine walizimia kwa hisia, walilia kwa kusikiliza tu maneno ambayo hawakuwa wakijua maana yake. lakini namna alivyokuwa akicheza na kuonesha hisia zake kwenye maneno hayo nao pia walikuwa wakijihisi wanaelewa na kusikia ile hali aliyokuwa akiisikia.

Hii ni kutokana na utunzi wa kiakili na uimbaji pia. utaona pia katika tamasha hilo jinsi ambavyo aliandaa mpaka kifaru kuja jukwaani na mazingira mbalimbali katika wimbo wake wa "What about us"

Akili si walikuwa nazo akina Aristotle,Socrates,Archimedes, Einstein etc. tukiangalia kwa upande huu mwingine pia ni akili nyingi zilitumika kwa yeye kuweza kuteka nyoyo za watu namna ile. kama ni mtu mwenye kuamini ushirikina ungesema aliwaroga ndio maana alipendwa kila sehemu.
Nakubali kuwa MJ alikuwa ni miongoni mwa biadamu wenye vipaji vya hali ya juu lakini hakuwa wa kipekee kiviile maana wapo akina Bob Marley ambao wamegoma kufa kwa miaka 35 leo,huyu kafa mwaka 2009 lakini anazidi kupotea tu.....
Sikiliza mashairi ya nyimbo zake. kama huna akili huwezi tunga mashairi yale. angalia video zake. ambazo pia zilikuwa na maelekezo yake mengi anataka video iweje. Hii yote ni akili. wadau tunapowaza suala la akili tusiangalie upande mmoja tukasahau kila mtu ana akili zake kwa eneo lake.
Hapa unatakiwa utuoneshe hicho cha ajabu ulichokiona kwenye nyimbo zake.Nikikuambia leo kuwa kulikuwa na kitu cha kipekee kwenye nyimbo za Lucky Dube utalazimika kunitaka nikuoneshe hicho kilicho cha ajabu.Na wewe ni lazima utuoneshe hicho ulichokina kwenye nyimbo za MJ maana mimi sikioni....
Aina yake ya uchezaji ambayo ilikuwa ni ya kimapinduzi ni uvumbuzi alioufanya ukiangalia ile style ya moon walker au angalia ule ubunifu wa kwenye wimbo wa smooth criminal pale inapoonekana ameweza kuishinda gravitational force.

Anaenda mwili mzima yeye na wachezaj wake na kurudi pasipo kuanguka. umejiuliza aulitumia mbinu gani? Huoni kama hiyo ni akili kwa lolote alilolifanya?
Wewe jamaa bana,kwani hujui kuwa kuna viatu maalum kwaajili ya uchezaji ule?

Hata P Square walifanya hivyo kwenye wimbo wao Personally,au na wao waliishinda hiyo gravitation?
Tumkumbuke kama mmoja ya watu waliokuwa na akili na wenye mchango wa kipekee hapa duniani. Kwa kupitia music wake wengi walikuwa motivated kuimba na kucheza na wengi waliburudishwa na kuelimishwa.
Ni kweli lakini siyo kwa kiwango hicho....
 
Kwahiyo kutumia mkorogo pia ni akili sio??
Hakutumia mkorogo kwa kupenda,aliwahi kuugua aina ya ugonjwa WA ngozi baada ya kupona alibaki na mabaka mabaka ndio doctor wake aka mshauri kutumia dawa ya kuondoa mabaka mwilini ila matokeo Yale hakuthubutu kuyapenda kabisa. Na SII hivyo tuu mwilini wake umekumbwa na majanga
 
Michael Jackson alikuwa ni kibaraka/Ajenti wa Shetani.

---Freemason walianza kumlea ktk fani ya mziki tangu akiwa mdogo sana, mpaka pale alipofika ni masonic ndo wamemfikisha.

---Michael alitumiwa kama Ajent wa kuutangazia ulimwengu kuwa kubadili dini it is possible na ni normal. Na ni kweli baada ya yeye kubadili rangi, dunia nzima ikaona ni mambo ya kawaida kubadili rangi.

---Kupitia yeye ndie alieusambazia ulimwengu suala la watoto wa kupandikiza.

---Haya mambo ya kuchonga pua na baadhi ya viungo vya mwili vilisambazwa na Michael Jackson.

---Hata Nyota ambayo jamaa alikuwa aking'ara nayo ni nyota ambazo jamaa alipandikiziwa, ktk ulimwengu wa roho mtu kupewa nyota ambayo sio yako inawezekana kabisa. Na hata hapa Tanzania kuna viongozi wetu tu ambao walipewa na wanapewa hizi nyota.

---Hizi alama sijui za kukunja vidole na styles zingine nyingi kutoka kuzimu zilisambazwa na huyu bwana. Ile ya vidole kuna haitoshi, wakaamua watengeneze film inayoitwa "SPIDERMAN" ili kuwahadaa watu na hiyo style na wanadamu tuone kuwa ni kawaida.

Michael Jackson alikiri kuwa ni kweli yeye alikuwa freemason, na alitoka huko baada ya kuona freemason wanampa majukumu mazito zaidi na Michael akakataa. Hapo ndipo ugomvi wao ulipoanza, Michael aliandamwa sana maana amekiuka Agano kati yake na Malango ya Giza. Moja ya matukio makubwa ni lile la kutaka kumfilisi kwa kupitia dada yake kucheza kanda ya ngono. Kuna Album yake moja hivi aliitoa ikiwa na nembo flani hivi ya ajabu, ktk ile nembo kuna sura, wanyama na vitu vingine. Sasa pale kila kitu kilikuwa na maana yake.

Michael Jackson alijisemea kabisa kwamba yeye alikuwa ni Freemason, Je tuna watu mashuhuri wangapi duniani ambao hawajajisema?
Hizi story za vijiweni toa hapa
 
Back
Top Bottom