Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Nimekuuliza hivi; Abeid Amani Karume "mtwana" alimuoa lini Fatma "muungwana"? bado hujajibu.
Mkuu Zomba, mbona nilikujibu?!. Rejea kwenye ile posti yako kisha angalia jibu langu, ua ulitaka jibu unalotaka wewe?, ukiulizwa unajibu jibu ulilonalo wewe na sio lazima jibu la muuliza swali ndio maana hata maudhui ya uzi huu yameulizwa swali lililohitaji jibu fulani, mpaka sasa majibu ndio haya nayo ni majibu pia!.

Yale maswali ya jua huwa linachomoza upande gani na kuzama upande gani, huwa siyajibu!, hayo ni majibu hivyo ukiona kuna kitu sijajibu, hilo ndilo jibu langu!.
Nakaribia kukamilisha kuzijibu hoja zote nifungue uzi wa pili.
Pasco
 
Kenya Weekly News Dec 1963

It must be realized that for at least130 years Zanzibar has had a civilized and peaceful existence under an organized Goverment where racial and religious harmony has been the keynote and that ideas being tried out in neighbouring territories have been established practise in Zanzibar for many years.
End of qoute

What happened that Zanzibar backslided?

Ni ufisadi wa hawa wanaojiita ndugu zetu wa Tanganyika na chuki zao dhidi ya Waarabu. Yaani hawa wameteswa na wareno wajerumani na waingereza lakini chuki zao mpaka leo hapa Bongo ni Uarabu na hawa wagalatia kina Pasco ni Uislam and so ni dini ya Waarabu.
 
Pole Pasco, kumbuka hapa unapambana na watoto hadi vitukuu wa waliodai kunyang'anywa tonge mdomoni mwaka 1964...loo! hiyo ghadhabu yao utaiweza? Kuna watu wameamua ku"rewrite history" based on sources zilizotawaliwa na visasi, they will stop at nothing; watakubeza, watakutukana na watakulaani kwani chuki zao haziwezi kuwapa mwanya wa kufanya vinginevyo. Porojo za Ghassany na ngano za Mohamed? No, not worth my time and effort. Nakumbuka Sultani kijana Jamshid bin Abdullah alivyoduwaa baharini na boti lake asijue akimbilie wapi baada ya Kenyatta kumwekea ngumu kukanyaga Malindi, Kenya hadi Nyerere alipompa hifadhi ya muda Tanganyika...am out.
Wacha kupotosha katukanwa wapi yeye ndiyo analeta matusi na kejeli, ingia kwenye mnakasha msaidiane hapa ni hoja tu.
 
Last edited by a moderator:
Pasco vipi, jana usiku uliahidi "kesho sina kazi, nitazipangua hoja moja baada ya nyingine!, hakibaki kitu hapa!."

Ukatutia hamu, leo baada ya swalat' fajr tukakukalia hapa na uji wetu wa kunde tunakusubiri ujitutumuwe japo "kiduchu" lakini
naona upo kimya, umepatwa na kazi ya ghafla? au maji yamekuzidi kimo?
Mkuu Zomba, kumbe nawe ni Swala Tano?!, huelekei!. Sisi wengine kuamka Jumamosi zetu huanzia saa 4, hapa nimejitahiji na kwenye supu bado sijapita!, nasisitiza hoja zitapanguliwa zote!.
I will leave no stone unturned!.
Pasco
 
Mkuu Zomba, mbona nilikujibu?!. Rejea kwenye ile posti yako kisha angalia jibu langu, ua ulitaka jibu unalotaka wewe?, ukiulizwa unajibu jibu ulilonalo wewe na sio lazima jibu la muuliza swali ndio maana hata maudhui ya uzi huu yameulizwa swali lililohitaji jibu fulani, mpaka sasa majibu ndio haya nayo ni majibu pia!.

Yale maswali ya jua huwa linachomoza upande gani na kuzama upande gani, huwa siyajibu!, hayo ni majibu hivyo ukiona kuna kitu sijajibu, hilo ndilo jibu langu!.
Nakaribia kukamilisha kuzijibu hoja zote nifungue uzi wa pili.
Pasco
Mkuu Pasco

Naona unatafuta pakutokea huu uzi bado mbichi kabisa unataka kuanzisha mwingine.
 
Last edited by a moderator:
Ni ufisadi wa hawa wanaojiita ndugu zetu wa Tanganyika na chuki zao dhidi ya Waarabu. Yaani hawa wameteswa na wareno wajerumani na waingereza lakini chuki zao mpaka leo hapa Bongo ni Uarabu na hawa wagalatia kina Pasco ni Uislam and so ni dini ya Waarabu.
Pole kwa msiba na machungu ya Mapinduzi Matukufu ya 1964!. Endelea kujifariji ni wabara na wagalatia kina Pasco il;i roho yako itulie.

Unaelewa dhanna yako nzima ya "utwana" na "uungwana" wa Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi inauliwa na swali hilo. Wala sitegemei kupata jibu kutoka kwako, cha muhimu ni kuwa umelielewa swali na limekuingia.

Kwakuwa umedhihirisha upeo wako ni mdogo sana nilitaka likuingie tu akilini mwako. Ntakukumbusha tena mjadala unapoendelea, nnayakini kuwa ntaipata fursa tena kutokea kwako, utakwepa vipi na uwezo wako ndio huo tuuonao hapa.
 
Mkuu Zomba, kumbe nawe ni Swala Tano?!, huelekei!. Sisi wengine kuamka Jumamosi zetu huanzia saa 4, hapa nimejitahiji na kwenye supu bado sijapita!, nasisitiza hoja zitapanguliwa zote!.
I will leave no stone unturned!.
Pasco

AlhamduliLlah mimi ni Muislaam na sipigwi chenga kuswali swala tano.

Tunangoja hizo hoja uzipangue lakini naona kila unapojaribu unazidi kujishindilia kwenye kina ambacho kimekuzidi.

Nakuuliza tena, Zanzibar ulikwenda lini mara ya kwanza na kwa sababu zipi? au na hili nalo inabidi uwe mwanasayansi kulijibu?
 
Pole kwa msiba na machungu ya Mapinduzi Matukufu ya 1964!. Endelea kujifariji ni wabara na wagalatia kina Pasco il;i roho yako itulie.
Pasco

Wala sihitaji pole yako na ya mwengine popote. Wape pole hao 'mliowakomboa' kwa mapinduzi na uhuru wa karatasi 1961 kwani mpaka leo miaka 50 majority wanaishi katika slums and living below poverty line.
Ahadi zote walizopewa hakuna hata moja iliyowafaidisha na kama si shule zenu za makanisa na misaada kutoka nje nadhani mngalikuwa bado mnasoma chini ya miembe na ujambazi na machangu doa kuzidi na pengine takwimu za ukimwi zingali sky rocket.

Mna kila kitu cha kujivunia kuweka watu korokorni hovyo kupiga na kuwauwa watu wasio na hatia sababu wanadai waliyoahidiwa na Uhuru na Mauwaji mnayoyaita Matukufu ya 1964.

Wazee wetu wako vindicated pale waliposema lets wait and see.

Katika uchaguzi wa 2010 wagombea wote 11 wa CCM walielekea Arabuni kuomba hela za kampeni kwa wenzao waliosoma nao madarasa pamoja Zanzibar. Ushahidi upo na hilo nakupa challenge kalifanyie utafiti.

Hiyo ndiyo Zanzibar usiyoijua!

Read the marks of time Pasco!
 
AlhamduliLlah mimi ni Muislaam na sipigwi chenga kuswali swala tano.

Tunangoja hizo hoja uzipangue lakini naona kila unapojaribu unazidi kujishindilia kwenye kina ambacho kimekuzidi.

Nakuuliza tena, Zanzibar ulikwenda lini mara ya kwanza na kwa sababu zipi? au na hili nalo inabidi uwe mwanasayansi kulijibu?
Mkuu zomba

Hapa Pasco kanasa kwenye trap kila akijaribu kujinasua ndiyo anazidi kunasa.
 
Last edited by a moderator:
Unaelewa dhanna yako nzima ya "utwana" na "uungwana" wa Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi inauliwa na swali hilo. Wala sitegemei kupata jibu kutoka kwako, cha muhimu ni kuwa umelielewa swali na limekuingia.

Kwakuwa umedhihirisha upeo wako ni mdogo sana nilitaka likuingie tu akilini mwako. Ntakukumbusha tena mjadala unapoendelea, nnayakini kuwa ntaipata fursa tena kutokea kwako, utakwepa vipi na uwezo wako ndio huo tuuonao hapa.

Pasco.
Nini?

Ufungue uzi wa pili?
Kwani huu ushakatika?

Umeyavulia maji nguo lazima ukogeshwe.
Usikimbie.

Tutakuchukua hapa taratibu hadi tukufikishe kizingitini kwako.
Jibu maswali yetu.

Iweje penye ubagzi Abeid Karume amuoe Fatma?
Iweje Sayyid Khalifa bin Haroub amuoe Bi Matuka mwanamke wa Kimanyema?

Unajua kuwa masultani wameingia katika mianandani yao hakuna hata mmoja
alikuwa na damu mikononi mwake?

Masultani hawakupata kuua wala kudhulumu raia wao.

Masultani walikuwa wakitembea Zanzibar nzima bila ulinzi na wakisimamisha gari
zao kuwapa lifti watu.

Haya unayajua?

Unajua utafiti uliofanywa baada ya mapinduzi uligundua kuwa hapakuwa na
''miscarriage of justice'' kwenye kesi yoyote baina ya Muarabu na Mwafrika
katika mahakama za Zanzibar?

Haya unayajua?

Bado hujanijibu kuhusu Ali Muhsin na ZNP.

Vipi ZNP walitegemea kushinda uchaguzi katika mazingira hayo unayodai ndiyo
yalitawala nyoyo za Wazanzibari?

Bwana mdogo soma na jifunze kutumia ubongo wako.
Vinginevyo utabaki kuwa ''court jester wa CHADEMA.''

Utabaki kuwa Launcelot Gobbo.
 
Pole kwa msiba na machungu ya Mapinduzi Matukufu ya 1964!. Endelea kujifariji ni wabara na wagalatia kina Pasco il;i roho yako itulie.
Pasco

Pasco,

Wewe huwajui wa kuwapa pole.

Mbona kitabu unacho kama unavyojigamba?
Au wewe mvivu wa kusoma?

Hujasoma na kujiuliza?
Wale watu waliua hakuna aliyejua.

Allah aliwasitiri.

Iweje ghafla wanamkimbilia Dk. Ghassany nakueleza jinsi walivyowaua akina
Kassim Hanga, Othman Shariff na wengineo?

Soma na sikiza maneno yao ya kujuta.
Hawa ndiyo wa kupewa pole.

Umemsoma Sheikh Baramia anasema nini kuhusu mauaji ya Karume?

Mimi nitakusaidia Pasco.
Nakuwekea hapa attach. Taazia niliyomwandikia Ali Nabwa alipokufa.

Soma utakuwa mwerevu kuliko ulivyokuwa jana.

Kitu kimoja nataka ujue na nakitanguliza kabla maana huenda usisome
kwani sipati picha kama wewe ni mtu wa kusoma.

Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala walikuwa rafiki wa baba yangu.
Hawa walidhulumiwa roho zao.

Baba yangu alikuwa akitembelewa na jamaa kutoka Zanibar akiuliza habari
za wajane wao na mzee alikuwa akiwataja hawa rafiki zake alikuwa akinong'ona.

Wape pole hawa na mfano wa hawa pamoja na baba yangu.
 
Attachments

  • ALI NABWA.doc
    50 KB · Views: 106
Ni ufisadi wa hawa wanaojiita ndugu zetu wa Tanganyika na chuki zao dhidi ya Waarabu. Yaani hawa wameteswa na wareno wajerumani na waingereza lakini chuki zao mpaka leo hapa Bongo ni Uarabu na hawa wagalatia kina Pasco ni Uislam and so ni dini ya Waarabu.

waingereza walikuwa hawanyofowi korodani
 
Mkuu Pasco

Naona unatafuta pakutokea huu uzi bado mbichi kabisa unataka kuanzisha mwingine.
Mkuu Ritz, ziko series 5 zinatakiwa ziwe zimeisha kabla ya January 12, nimedhamiria kuzivurumisha kabla ya mwisho wa mwaka ndipo nitie timu Zanzibar kwenda kuyashrehekea hayo Mapinduzi Matukufu.
Pasco
 
Pasco,

Wewe huwajui wa kuwapa pole.

Mbona kitabu unacho kama unavyojigamba?
Au wewe mvivu wa kusoma?

Hujasoma na kujiuliza?
Wale watu waliua hakuna aliyejua.

Allah aliwasitiri.

Iweje ghafla wanamkimbilia Dk. Ghassany nakueleza jinsi walivyowaua akina
Kassim Hanga, Othman Shariff na wengineo?

Soma na sikiza maneno yao ya kujuta.
Hawa ndiyo wa kupewa pole.

Umemsoma Sheikh Baramia anasema nini kuhusu mauaji ya Karume?

Mimi nitakusaidia Pasco.
Nakuwekea hapa attach. Taazia niliyomwandikia Ali Nabwa alipokufa.

Soma utakuwa mwerevu kuliko ulivyokuwa jana.

Kitu kimoja nataka ujue na nakitanguliza kabla maana huenda usisome
kwani sipati picha kama wewe ni mtu wa kusoma.

Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala walikuwa rafiki wa baba yangu.
Hawa walidhulumiwa roho zao.

Baba yangu alikuwa akitembelewa na jamaa kutoka Zanibar akiuliza habari
za wajane wao na mzee alikuwa akiwataja hawa rafiki zake alikuwa akinong'ona.

Wape pole hawa na mfano wa hawa pamoja na baba yangu.
Poleni sana!, poleni wote!.
Pasco.
 
Nipo hapa jamvini toka jana usiku nikisubili majibu ya swali alilouliza Pasco hakuna hata mmoja anajibu zaidi tunaletewa hadithi ambazo zimo humu toka 2010!
 
Sinapindu ahsante sana mimi ni Samitungo Muyukwa Mwekapopo siyo Semitungo.

Shukran sana kwa ukumbusho Sheikh Mohammed Said.

Nilikuja Tanga na Kitabu chako cha Uamuzi wa Busara wa Tabora, Banu Kihere, Banu Mohammed Jambia, Banu Mustafa Shauri na Banu Rashid Makoko wanalalama kuwa Kitabu kizima umejaza picha za Sheikh Suleiman Taqadir tu kama Kitabu kilihusu maisha yake tu.

Uje upate picha zao nao kuweka kumbukumbu sawa. Binafsi wamenipa picha ya Nyerere akiwa na Mzee Rajabu Diwani, M M Kihere, Peter Mhando, Mama Batuli Dezo, Dkt Krishna na Mamboleo Rashid Makoko.
 
Back
Top Bottom