Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Mkuu Maalim Mohamed Said, kiukweli nilitumwa!, nimeimbishwa na sasa naenda kumuuliza alienituma kama tuendelee na huu mnakasha au tuufunge maana hatukutegemea mtu kama wewe ungeingia humu na ukiingia pahali, shughuli yake pevu!.

Ni kweli sina moja ninalojua ndio maana nimeuliza?!.

Pia ni kweli siwajui kabisa komred Salim Jinja wala komred Badawiy Qullatein, naomba unieleweshe wanahusika na nini katika mada yangu kuu ya uzi huu!. Ndio hao waliomsindikiza Shamte kule UNO au ndio waliopeleka yale malipo ya miaka kadhaa mbele au ndio waliofanya nini haswa maana mada yangu kuu hapa ni jinsi kiti cha Zanzibar kilivyopotea kule UNO hadi sasa Zanzibar kubaki jina tuu ikiitwa nchi ili hali kiuhalisia sio nchi bali ni sehemu tuu ya JMT yenye mamlaka yake kamili kushughulikia mambo yake ndani. Ingekuwa ni Nyumba, ni yale madogo madogo ya jikoni, chumbani na maliwato,yale makubwa ya kibarazani na sebuleni ni wenyewe!.
Pasco.

Pasco,
Unataka nikueleweshe kuhusu makomredi?

Matusi ushaacha sasa unataka kusoma?
Nakushauri ubaki katika hayo unayoyajua vyema.

Hayo ya ushemeji na ukwe.
Haya ya usomi mazito kwa kichwa chako.
 
Hili kila mtu analijua, ila tulifungulie thread yake ili pia tueleze jinsi Waarabu walivyokuwa kuwa wakaribu kwa watumwa!, waliwauza wapi?, huko walikouzwa ni kwa kina nani?, hao walionanunua hao watumwa babu zetu, walifanya nini watumwa wote wanaume?, na wanawake walitumikaje!. Fungueni tuu thread kuhusu ya Wema na Ukarinu wa Waarabu kwa Watumwa ili tuichangie!. Hii ni ya Maswali yasiyo na majibu kuhusu Ule uhuru bandia wa Zanzibar na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Pasco.

Pasco,
Historia ya utumwa huwezi kuieleza kabla hujaisoma historia ya Across Atlantic Slave Trade.

Anza na hiyo kwanza kabla hujaingia katika ''matukufu.''
 
Zanzibar nimekuwa nakuja tangu mtoto nikisoma primary tukiwa na marafiki wa kizenji shuleni kwetu tukisoma nao bara, wakati wa likizo tukija kwao Zenzi wana hoteli kubwa enzi hizo!.

Nipongia uandishi tukaja ziara rasmi Zenzi tukapokelewa kwa kelele za kuitwa machogo!, tango hapo nimefanya zaidi ya sarri 100 Zanzibar!, nimeishalala Mwembe Madema!, nimeishaondolewa Zenj under escort na kupigwa marufuku nisikanyage tena!. Baadaye ban ikaondolewa!. Enzi za ujana pia nilishiriki sana na ndugu zetu sisi si ni dugu moja!.
Wiki ijayo nakuja kukaa siku 10 Zanzibar kushherekea Mapinduzi Matukufu na mimi ni wale Chapa Ng'ombe wa Kanda ya Ziwa, ugonjwa wetu unajulikana!. Wengi wa wabara sasa wakija Zenji ni kuja kuponda maraha, huu uzi unakoelekea siko, nikona vipi, nitaumalizia baada ya kutoka huko, sije endelea sana nikajikuta vile vichupa vya tindikali ndivyo vinanisubiri!. Hapo Zenj mpaka nina nyumba ya kufikia, anytime, nikiamua kulala hoteli ni kwa raha zangu tuu!. Zanzibar kwangu, Waarabu wangu, Wahadimu wangu, Watumbatu pia wangu!, na nyinyi bara yenu!.
Tunajenga nyumba moja Tanzania, kwa nini mnataka tugombee fito?. Kiukweli tukiona vipi, tunaamua tuu Nchi Moja, Serikali Moja!.
Pasco.

Intellect yako kweli ni ndogo kama alivyosema Maalim Mohamed Said. Mimi nimekuuliza "Mara yako ya kwanza kwenda Zanzibar ilikuwa lini na kwa sababu zipi?" wewe unabwabwaja mambo ambayo hayana kichwa wla miguu, mantiki yangu ya kukuuliza hujaielewa kabisaaaa unaleta mambo ya "Zanzibar nakuja", nililala, nikarudishwa, sijui kubwabwaja kote kunattokea wapi? by the way mimi nnaekuuliza nipo hapa bara au wewe upo Zanzibar kwa sasa hivi?

Hebu jibu swali kwa ufupi tu, mara yako ya kwanza kwenda Zanzibar lini? kwa sababu zipi?
 
Mkuu Ritz, unamjua Shamte au unamsikia tuu?!.

Jee unajuwa kuwa Shamte alikuwa ASP!, unazijua sababu zilizomfanya kujiengua ASP na kuunda ZPPP?!.

Baada ya ASP kushinda uchaguzi wa mwanzo, Shante aliutamani Uwaziri Mkuu, kwa vile Karume ndio alikuwa Kinara wa ASP, Mohamed Shante akijiengua kutoka ASP na kuunda chama cha ZPPP ili kujiunga na wabaya wa ASP kuunda serikali ya mseto

Katika uchaguzi wa Julai 1961, ASP kilipata asilimia 49.9 ya kura zote, ZNP kilipata asilimia 35 na ZPPP asilimia 13.7. Hata hivyo, pamoja na ushindi wa kura ASP, kilishindwa kutamba katika viti vya bunge (LEGCO) kilipopata viti 10, ZNP 10 na ZPPP vitatu.

Uchaguzi huo ambao haukupata mshindi na ilibidi urudiwe Julai, 1963, matokeo ni muungano wa ZNP/ZPPP viti 18 na ASP viti 13. Shamte alishauriwa aunde Serikali ya mseto kati ya ZNP/ZPPP na ASP ili kulinda umoja wa kitaifa, lakini aligoma kata kata kwa kiburi na jeuri ya kuogopa ASP isije kumoutshine!. Kitendo cha Shamte aliyekuwa ASP na kujitoa kwa tamaa ya uiongozi, kisha kukataa kata kata kushirikiana na ASP ambao ndio Waswahili wenzake na badala yake kujiunga na ZNP ambacho ni cha Waarabu, hapa ndipo ukibaraka wake ulipolalia!.

Pasco.

Pasco,
Nenda kasome ''Conflict and Harmony in Zanzibar'' cha Ali Muhsin.

Katika kitabu kile Sheikh Ali Muhsin kaeleza msimamo wa Zanzibar Nationalist
Party (ZNP) kuhusu huo wewe unaouita ''Uarabu.''

Angalia idadi ya ya hao wewe unaowaona kuwa ni Waarabu kisha fananisha
na idadi ya Waafrika.

Kisha jiulize vipi ZNP itatetea mtu mmoja kura moja katika hali kama hiyo?
Vipi wangeweza kushinda?

Kama una akili ya uchambuzi utakuwa umenielewa.

Angali hapa chini hali ya Zanibar na uongozi wake na kama una akili chambua
uwapate Waafrika na Waarabu hapo.

Hapo yuko Maulid Mshangama, Dk Baalawy, Ali Muhsin, Juma Aley, Ibun Saleh,
Mohamed Shamte.

Hebu nichambulie nani Muarab hapo nani Mwafrika.

z13%255B1%255D-1.jpg
 
Komredi Ali Sultan Issa

Komredi Sharifu Ahmed Baddawiy Qullatein (Jina lake limechukuliwa kwa Ahmed Baddawiy wa Riyadhwa Lamu)

Kanali Ali Mahfoudh

Komredi Amour Dugeish

Salim Rashid

Nk

Zanzibar ina mambo Sheikh Pasco, ni vema ukaendelea na yale ya kuichachafya Chadema na kumsifu Alhabib Edward Lowassa hasa msimu huu wa "Nyama Choma Festival" kule Monduli.
 
La ushemeji, si nimesema ninge!, au hasira na kumbadili dini mtu?!. Mbona wabara wengi wamesilimishwa kwa ajili hiyo!. Bara Zanzibar dugu moja!. Hata mitaa yako hapo Gerezani, tumepita sana tuu, wakati huo nikiwa RTD, walikuwa wanakuja wenyewe!. Ujana nao una ushetani wake, basi tuu saa hizi ungekuta labda niliishasilimishwa zamani nikiitwa Mkwe!. Basi tuu!.
Pasco.

Wewe kama u Msukuma kweli nna uhakika hukosi Mjomba au Shemeji wa Kiarabu, Wamanga wamezagaa usukumani toka enzi na enzi au mwenzetu hujabahatika? au u Usukuma wako wa kudandia? maana takwimu za DNA za Mkemia Mkuu zinatisha:

Takwim:Asilimia 48.3 Ya watoto waliozaliwa sio watoto wa baba halisi.wengi wamebambikiwa - Salma Msangi
 
Asome pia "Race, Revolution and Struggle for Human Rights in Zanzibar: Memoirs of Ali Sultan Issa n Maalim Seif Sharif Hamad" cha Thomas Breggs.

Naambiwa pia mwandishi huyu alishakutanisha na Mzee wetu Hassan Nassoro Moyo ili waandike Kitabu kuhusu maisha yake, Mapinduzi na Muungano kwa mapana yake, haya masuala yako "ahly" wa kuyajibu zaidi ni Hassan Nassoro Moyo, aliyekuwa Waziri wa Sharia wa Zanzibar wakati wa Muungano.

Kuhusu hayo ya Sakura mimi niko Tanga Sheikh wangu na nafanya mazungumzo na hao wengi ambao Sheikh Harith Ghassany anadaiwa aliwapitia, kuna utata mkubwa kwenye hilo la Sakura kwa kuwa ni maneno ya upande mmoja, nione kabla ya kuleta huo uzi wako nikupe ya ziada.

Kuhusu Mohammed Said Salim Abdallah Semitungo, kwanza huyu ni Mtani wangu wa Kimanyema, sisi wadigo hufurahia sana mafungamano yetu na hawa ndugu zetu wa azzal na enzi, pili Ndugu yangu huyu alifanya upendeleo mkubwa sana katika kumuandika Sheikh Abdulwahid Kleist Sykes Mbuwane.

Jana nilizungumza na Jamaa wa Mzee Rashid Makoko (Huku kuna kitu inaitwa "Makoko Road"). Zaidi nilijikita kwenye mafungamano ya Ally Kleist Sykes Mbuwane na Mamboleo Rashid Makoko, naamini kwa dhati sasa kuwa Sheikh Mohammed Said anapaswa kutoa "Edition ya Pili" ya Kitabu chake.

Daktari Adolph Mkenda wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Sasa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha) naye alikichambua kiasi kitabu cha Mohammed Said, Hasa kwenye muktadha wa Kitabaka ambao Sheikh Mohammed Said aliukwepa, kaeleza kwa kirefu "Ubwanyenye" uliotumika kumfanya "mtu asiye Kuli" kuwa "Kiongozi wa Makuli" nk.

Mimi nawapongeza pia Mohammed Said na Mwanapopatlal Harith Ghassany kwa kuleta hayo ya upande mwengine, Kina Pasco nanyi changamkeni mje na yenu na sio kulalama kuwa wenzenu warongo tu wakati hamji na huo ukweli.

Ila kuhusu la "Uarabu" la Zanzibar, umetokota sheikh wangu. Zanzibar ni "Rainbow Nation", Kipo kiminyano cha Kitabaka na ndio usuli wa hayo Mapinduzi, na kuyaeleza Mapinduzi hakuwezi kunoga mpaka ujikite kwenye kuwachambua hao "Third Party" kina Umma Party.
 
Mkuu Ritz, unamjua Shamte au unamsikia tuu?!.

Jee unajuwa kuwa Shamte alikuwa ASP!, unazijua sababu zilizomfanya kujiengua ASP na kuunda ZPPP?!.

Baada ya ASP kushinda uchaguzi wa mwanzo, Shante aliutamani Uwaziri Mkuu, kwa vile Karume ndio alikuwa Kinara wa ASP, Mohamed Shante akijiengua kutoka ASP na kuunda chama cha ZPPP ili kujiunga na wabaya wa ASP kuunda serikali ya mseto

Katika uchaguzi wa Julai 1961, ASP kilipata asilimia 49.9 ya kura zote, ZNP kilipata asilimia 35 na ZPPP asilimia 13.7. Hata hivyo, pamoja na ushindi wa kura ASP, kilishindwa kutamba katika viti vya bunge (LEGCO) kilipopata viti 10, ZNP 10 na ZPPP vitatu.

Uchaguzi huo ambao haukupata mshindi na ilibidi urudiwe Julai, 1963, matokeo ni muungano wa ZNP/ZPPP viti 18 na ASP viti 13. Shamte alishauriwa aunde Serikali ya mseto kati ya ZNP/ZPPP na ASP ili kulinda umoja wa kitaifa, lakini aligoma kata kata kwa kiburi na jeuri ya kuogopa ASP isije kumoutshine!. Kitendo cha Shamte aliyekuwa ASP na kujitoa kwa tamaa ya uiongozi, kisha kukataa kata kata kushirikiana na ASP ambao ndio Waswahili wenzake na badala yake kujiunga na ZNP ambacho ni cha Waarabu, hapa ndipo ukibaraka wake ulipolalia!.

Pasco.

Natamani uuone u punguani wako kwenye hii post yako ili uurekebishe lakini nnajuwa huna upeo huo kwani "you are too shallow". Sitokupa ilmu hiyo, nawaachia wengine nao wakusome ulivyo punguani.

Hint; "Waswahili", "Waarabu", ASP.
 
Asome pia "Race, Revolution and Struggle for Human Rights in Zanzibar: Memoirs of Ali Sultan Issa n Maalim Seif Sharif Hamad" cha Thomas Breggs.

Naambiwa pia mwandishi huyu alishakutanisha na Mzee wetu Hassan Nassoro Moyo ili waandike Kitabu kuhusu maisha yake, Mapinduzi na Muungano kwa mapana yake, haya masuala yako "ahly" wa kuyajibu zaidi ni Hassan Nassoro Moyo, aliyekuwa Waziri wa Sharia wa Zanzibar wakati wa Muungano.

Kuhusu hayo ya Sakura mimi niko Tanga Sheikh wangu na nafanya mazungumzo na hao wengi ambao Sheikh Harith Ghassany anadaiwa aliwapitia, kuna utata mkubwa kwenye hilo la Sakura kwa kuwa ni maneno ya upande mmoja, nione kabla ya kuleta huo uzi wako nikupe ya ziada.

Kuhusu Mohammed Said Salim Abdallah Semitungo, kwanza huyu ni Mtani wangu wa Kimanyema, sisi wadigo hufurahia sana mafungamano yetu na hawa ndugu zetu wa azzal na enzi, pili Ndugu yangu huyu alifanya upendeleo mkubwa sana katika kumuandika Sheikh Abdulwahid Kleist Sykes Mbuwane.

Jana nilizungumza na Jamaa wa Mzee Rashid Makoko (Huku kuna kitu inaitwa "Makoko Road"). Zaidi nilijikita kwenye mafungamano ya Ally Kleist Sykes Mbuwane na Mamboleo Rashid Makoko, naamini kwa dhati sasa kuwa Sheikh Mohammed Said anapaswa kutoa "Edition ya Pili" ya Kitabu chake.

Daktari Adolph Mkenda wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Sasa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha) naye alikichambua kiasi kitabu cha Mohammed Said, Hasa kwenye muktadha wa Kitabaka ambao Sheikh Mohammed Said aliukwepa, kaeleza kwa kirefu "Ubwanyenye" uliotumika kumfanya "mtu asiye Kuli" kuwa "Kiongozi wa Makuli" nk.

Mimi nawapongeza pia Mohammed Said na Mwanapopatlal Harith Ghassany kwa kuleta hayo ya upande mwengine, Kina Pasco nanyi changamkeni mje na yenu na sio kulalama kuwa wenzenu warongo tu wakati hamji na huo ukweli.

Ila kuhusu la "Uarabu" la Zanzibar, umetokota sheikh wangu. Zanzibar ni "Rainbow Nation", Kipo kiminyano cha Kitabaka na ndio usuli wa hayo Mapinduzi, na kuyaeleza Mapinduzi hakuwezi kunoga mpaka ujikite kwenye kuwachambua hao "Third Party" kina Umma Party.

Huyo kutokota atakuelewa kweli, ungemwambia "kachemsha" tu. Na u "sheikh" autoe wapi huyu? angeuweza u shemeji kwanza labda saa hizi tungempiga na kanzu la darzi na makubadhi, ingawa japo "kiduchu" akaukaribia u sheikh.
 
Pasco,
Nenda kasome ''Conflict and Harmony in Zanzibar'' cha Ali Muhsin.

Katika kitabu kile Sheikh Ali Muhsin kaeleza msimamo wa Zanzibar Nationalist
Party (ZNP) kuhusu huo wewe unaouita ''Uarabu.''

Angalia idadi ya ya hao wewe unaowaona kuwa ni Waarabu kisha fananisha
na idadi ya Waafrika.

Kisha jiulize vipi ZNP itatetea mtu mmoja kura moja katika hali kama hiyo?
Vipi wangeweza kushinda?

Kama una akili ya uchambuzi utakuwa umenielewa.

Angali hapa chini hali ya Zanibar na uongozi wake na kama una akili chambua
uwapate Waafrika na Waarabu hapo.

Hapo yuko Maulid Mshangama, Dk Baalawy, Ali Muhsin, Juma Aley, Ibun Saleh,
Mohamed Shamte.

Hebu nichambulie nani Muarab hapo nani Mwafrika.

z13%255B1%255D-1.jpg
Pasco hayawezi hayo si kimo chake wala hathubutu.
Pasco nakushauri uombe radhi ukae kimya uwaache hawa magwiji wa historia watutumbuize humu, huna ubavu wa kusimama mbele yao hata "kiduchu".

Natamani kuona jibu lako katika hii, lakini nasikitika kusema naona nzi haooo wamemtangulia muuza utumbo.
 
Pasco vipi, jana usiku uliahidi "kesho sina kazi, nitazipangua hoja moja baada ya nyingine!, hakibaki kitu hapa!."

Ukatutia hamu, leo baada ya swalat' fajr tukakukalia hapa na uji wetu wa kunde tunakusubiri ujitutumuwe japo "kiduchu" lakini
naona upo kimya, umepatwa na kazi ya ghafla? au maji yamekuzidi kimo?
 
La ushemeji, si nimesema ninge!, au hasira na kumbadili dini mtu?!. Mbona wabara wengi wamesilimishwa kwa ajili hiyo!. Bara Zanzibar dugu moja!. Hata mitaa yako hapo Gerezani, tumepita sana tuu, wakati huo nikiwa RTD, walikuwa wanakuja wenyewe!. Ujana nao una ushetani wake, basi tuu saa hizi ungekuta labda niliishasilimishwa zamani nikiitwa Mkwe!. Basi tuu!.
Pasco.

Wewe ni kama.alivyosema Maalim Mohammed Said, huna adabu tena huna adabu sana tu. Remember you are a public figure as a news man unapaswa kuwa na adabu ata the same time unaweka maadili ya kuheshimu the public itself. Ukossefu wako wa adabu unwezaje kujisifu in public domain kuhusu uhusiano wako na wasichana na even huyu mmoja kumtaja kwa jina.
Wewe huoni kama umdhalilisha huyu msichana na hao wasichana wengine unaojisifia wanakujia mwenyewe?

Sasa hizi ziko in public domain usije ukakataa mbele ya sheria za udhalilishaji na itakapotokea hili hata huoneleki huruma wewe bcz hukukosea umeandika kwa makusudi na umeliandika three times.

Wewe kama huna ndugu wanawake basi at least una jamaa na marafiki wenye ndugu zao wa kike just ponder of what you have just done!!

Hufai hata hapo TBC kuachiwa kufanya kazi.

Kumbe ulifikiria utatupandisha mori upate kucheka umechemsha hapo.

You just took a wrong turn!
 
Asome pia "Race, Revolution and Struggle for Human Rights in Zanzibar: Memoirs of Ali Sultan Issa n Maalim Seif Sharif Hamad" cha Thomas Breggs.
Mkuu Sinapandu, kwa vile nitakuwa Zanzibar kwa siku 10, nitakitafuta kitabu hicho ili kupata ilmu.

Naambiwa pia mwandishi huyu alishakutanisha na Mzee wetu Hassan Nassoro Moyo ili waandike Kitabu kuhusu maisha yake, Mapinduzi na Muungano kwa mapana yake, haya masuala yako "ahly" wa kuyajibu zaidi ni Hassan Nassoro Moyo, aliyekuwa Waziri wa Sharia wa Zanzibar wakati wa Muungano.
Mpaka sasa kati ya Mashujaa wa Mapinduzi Matukufu na Muungano Adhimu aliyepo hai ni Mzee wetu Hassan Nassor Moyo, jana nimeelezwa na Mzanzibar mmoja kuwa yeye ndiye pekee mwenye zile original signed Articles of Union. Ikulu Zanzibar hazipo!, Ikulu bara hazipo!, kwenye Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa hazipo!. Mhifadhi Mkuu amesema kila rais anapomaliza muda wake, huondoka na baadhi ya kumbukumbu na personal copies zake za nyaraka kwa ajili ya kutunzwa kwenye personal presidential achieves hivyo nipatapo fursa ya kwenda Butiama, nitaziulizia, ila nafanya juhudi kumpata Mzee Hassan Nassor Moyo!.

Kuhusu hayo ya Sakura mimi niko Tanga Sheikh wangu na nafanya mazungumzo na hao wengi ambao Sheikh Harith Ghassany anadaiwa aliwapitia, kuna utata mkubwa kwenye hilo la Sakura kwa kuwa ni maneno ya upande mmoja, nione kabla ya kuleta huo uzi wako nikupe ya ziada.
Asante Mkuu Sinapindu, kwa hili nitakutafuta, ila alichofanya ni kujaribu kubadili mind set ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa hakukufanywa na Wanzibari bali wabara!, tangu day one nikauliza kwa nini ajikite kwa wanaodai ndio washiriki wa mapinduzi hayo wa upande mmoja ili hali mashushajaa wa Mapinduzi yale wakingapo hai?!. Na Mwenyeezi Mungu atakapoamua hatma ya hawa wachache waliobakia, naamini wataibuka mashujaa wapya wengi zaidi kussuport hilo ili kujifariji ASP walimpenda Sultani na ndio maana waiahidi kumlinda!, aliyempindua Sultani ndio yule yule aliyempokea, kumhifadhi na kumpatia safe passage to UK!.

Kuhusu Mohammed Said Salim Abdallah Semitungo, kwanza huyu ni Mtani wangu wa Kimanyema, sisi wadigo hufurahia sana mafungamano yetu na hawa ndugu zetu wa azzal na enzi, pili Ndugu yangu huyu alifanya upendeleo mkubwa sana katika kumuandika Sheikh Abdulwahid Kleist Sykes Mbuwane.
hili la upendeleo, tumemsema sana humu, kakubali kuwa yeye ni muwamba ngoma, lazima avutie kwake na kuwa lengo ni ajili ya Wazee wake wa Gerezani tuu, wengine nao wakaandike na kuwapendelea wa kwao!.[/QUOTE]

Jana nilizungumza na Jamaa wa Mzee Rashid Makoko (Huku kuna kitu inaitwa "Makoko Road"). Zaidi nilijikita kwenye mafungamano ya Ally Kleist Sykes Mbuwane na Mamboleo Rashid Makoko, naamini kwa dhati sasa kuwa Sheikh Mohammed Said anapaswa kutoa "Edition ya Pili" ya Kitabu chake.
Hili tumemlilia sana kuwa inawezekana alivyoambiwa sivyo, humu ameambiwa jinsi haswa ilivyo, tukamuomba basi angalau arekebisha makosa!, kagoma kata kata akiwataka walioona makosa nao watoe machapisho yao kulirekebisha andiko lake!.

Daktari Adolph Mkenda wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Sasa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha) naye alikichambua kiasi kitabu cha Mohammed Said, Hasa kwenye muktadha wa Kitabaka ambao Sheikh Mohammed Said aliukwepa, kaeleza kwa kirefu "Ubwanyenye" uliotumika kumfanya "mtu asiye Kuli" kuwa "Kiongozi wa Makuli" nk.
hili ni andiko la kutafutwa na ikibidi mwenye nalo alimwage humu!.

Mimi nawapongeza pia Mohammed Said na Mwanapopatlal Harith Ghassany kwa kuleta hayo ya upande mwengine, Kina Pasco nanyi changamkeni mje na yenu na sio kulalama kuwa wenzenu warongo tu wakati hamji na huo ukweli.
Hiki ndicho kitakachofuatia baada ya uzi huu, uandishi wa kitabu ni kipaji, sisi wengine tumejaaliwa critique tuu na sio kuandika.

Ila kuhusu la "Uarabu" la Zanzibar, umetokota sheikh wangu. Zanzibar ni "Rainbow Nation", Kipo kiminyano cha Kitabaka na ndio usuli wa hayo Mapinduzi, na kuyaeleza Mapinduzi hakuwezi kunoga mpaka ujikite kwenye kuwachambua hao "Third Party" kina Umma Party.
Hili nimekubali siku nyingi ila Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni class strungle kati ya wenyenacho na wasionacho, kisha wasionacho sio tuu kukalia makazi ya wenyenacho bali pia kuwabaka binti za wenyenacho na kuwafanya wake zao kwa nguvu matokeo yake ni vizalia wenye hasira machungu na visasi!, michango ya vizalia hivyo humu naibaini wazi, kuambiwa ukweli hawataki, undeni tume ya mapatano na maridhiano muambiane mlivyo fanziana kwenye mapinguzi yale, mshikane mikono, msameheane, msonge mbele!, ndio kwanza wengine wanatafuta scapegoat ya hasira zao kuwasingizia wengine kuwa ndio waliopindua ili kujifariji!, tena Waushukuru sana huu Muungano Adhimu, vinginevyo sijui wengine wangekuwa wapi hii leo!.
Pasco.
 
Zomba huyu Pasco hana cha kupangua wala cha kupanda.
Umemsikia lakini Mkuu Sinapindu?!, baada ya kuupata ukweli zaidi ya ule uujuaa, jee utakuwa tayari kutoa edittion nyingine!. Subiria mnakasha huu sehemu ya pili, ngoja nimalizie kuzijibu hoja kisha nipandishe sehemu ya pili humo ndimo kutakuwa kwako!.
Pasco
 
Dah nimeingia kwenye hii thread kwa minajili ya kuongeza knowldge matokeo yake nakuta majibizano,dah im disappointed
 
Kama umekuja as a reinforcement kumsaidia Pasco basi msaidie kutuza heshima ya kazi yake halafu umnasihi afanye uchambuzi yakinifu kabla hajaleta hoja zake.

Pasco kama haja yake ni kuitoa na kisafishia doa Tanganyika katika kile anachokiita scape goat yaani role ya Tanganyika katika mapinduzi na yaMuungano katika kuyalinda na kutetea mapinduzi anayoyaita matukufu basi anayo kazi kubwa kwanza ya kujifunza kuhusu Zanzibar.

Ikiwa Mwalimu alitamani kuikokota Zanzibar to the middle of the Indian Ocean mwaka mmoja tu baada ya Muungano basi Pasco ajitayarishe na kuelemewa na hisyoria halisi ya Zanzibar asiyoijuwa.
 
Hili nimekubali siku nyingi ila Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni class strungle kati ya wenyenacho na wasionacho, kisha wasionacho sio tuu kukalia makazi ya wenyenacho bali pia kuwabaka binti za wenyenacho na kuwafanya wake zao kwa nguvu matokeo yake ni vizalia wenye hasira machungu na visasi!, michango ya vizalia hivyo humu naibaini wazi, kuambiwa ukweli hawataki, undeni tume ya mapatano na maridhiano muambiane mlivyo fanziana kwenye mapinguzi yale, mshikane mikono, msameheane, msonge mbele!, ndio kwanza wengine wanatafuta scapegoat ya hasira zao kuwasingizia wengine kuwa ndio waliopindua ili kujifariji!, tena Waushukuru sana huu Muungano Adhimu, vinginevyo sijui wengine wangekuwa wapi hii leo!.
Pasco.

Nimekuuliza hivi; Abeid Amani Karume "mtwana" alimuoa lini Fatma "muungwana"? bado hujajibu.
 
Kenya Weekly News Dec 1963

It must be realized that for at least130 years Zanzibar has had a civilized and peaceful existence under an organized Goverment where racial and religious harmony has been the keynote and that ideas being tried out in neighbouring territories have been established practise in Zanzibar for many years.
End of qoute

What happened that Zanzibar backslided?
 
Back
Top Bottom