Mhe. Rais Magufuli, Anza na Kusaini Hati za Wote Waliohukumiwa Kifo, Wanyongwe Haraka Haraka Mpaka..

hivi, ungekuwa na mtoto wako amehukumiwa kunyongwa, au hata amekamatwa china alafu unamsikia kiongozi wako uliyempigia kura anasema wanyongwe haraka, utajisikiaje? uchungu wa mwana anaujua mzazi. wakati mwingine mtu akiwa madarakani watoto wake wanasoma ulaya, wanakula vizuri, wanalindwa na mabodigadi hawapati shida yeyote anasahau kuwa kuna watu wameugua hadi bp kwasababu ya watoto.alafu leo unatangaza kwamba wanyongwe, si ndo wazazi wao bp zitapanda zaidi? tuwe wakweli tusipepese macho.

yatupasa kupigana vita hii kwa kukata mzizi. hao mapunda sio target kubwa sana na walitakiwa hata adhabu wapunguziwe, ila hao matajiri ndio wabaya. hata hivyo, hata kama angekuwa tajiri, kuamuru mtu anyongwe ni ukatili wa hali ya juu sana and i hope legal and human rights centre wanaopambana kupinga adhabu ya kifo kwamba ni ya kikatili watalisemea hili. badala ya kuokoa maisha ya mtu unaamuru anyongwe, halafu akinyongwa yule aliyedhurika atarudi kwenye hali yake?
 
Magufuli anataka waliohukumiwa kifo China wanyongwe naye tunamuomba amnyonge ACP Bargeni aliyewaua wafanyabiashara wa madini wa morogoro tuone ujasiri wake
 
ha! we inakufaidisha nini..?
halafu mbona umekomalia au una lako jambo..
ingelikuwa mmoja wa ndugu yako yuko kwenye hilo kundi ungejisikiaje.. haya mambo hayahitaji haraka wengine humo usikute wamebambikiwa na wewe unasapoti tu.

kwa maamuzi ya mkulu jinsi yalivyo mi naomba apunguziwe baadhi ya madaraka maana tutaisoma kwelikweli
Huyu nadhani kati ya hao kuna mmoja anamdai
 
Hata kama ni ndugu yako kahukumiwa kunyongwa WACHA maneno WEKA kamba kwa shingo
 
Wanabodi,


Kikwete kiukweli kwa jinsi alivyokuwa dhaifu kwenye mambo makubwa, sidhani kama angeweza kusaini, hata angetaka kusaini, mkono ungetetemeka.

Udhaifu wa Kikwete ulianzia alipo wasamehe wale watuhumiwa wa EPA.

Kuonyesha alivyo dhaifu rais Kikwete aliwaombea msamaha Watanzania waliohukumiwa kifo nchini China kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

Mpaka sasa Kuna mamia ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa tangu enzi za Nyerere ambao hukumu zao hazitatekelezwa zikisubiri saini ya Magufuli.

Marais tangu Nyerere, Mkapa na Kikwete (Mwinyi alisaini), walishindwa kusaini kutokana na udhaifu wa mioyo yao, walikuwa na roho yepesi zenye huruma hivyo kulitia taifa hasara kubwa kutokana na udhaifu wao.

W
Kwangu mimi hili limekaa poa, waliohukumiwa kunyongwa mpaka wafe, wanyongwe tuu wafe, jee wenzangu hili mnalionaje? .

Paskali
Rejea

Idadi ya walionyongwa tokea uhuru Tanzania ni 232

Idadi ya wanaosubiria kunyongwa yafikia 465

Mamia wanasubiri kunyongwa nchini


Yaani wewe tangu ulipomwuliza rais swali na akakujibu kwa utani basi umekuwa ukiandika vitu vya hovyo na vyenye mwelekeo wa kujipendekeza kwenye huu utawala,sio kwamba marais ambao hawakusaini utekelezaji wa adhabu hyo walikuwa dhaifu,hapana ,bali wanajaribu kwendana na dunia ya leo na hasa shirika la haki za binadamu ambalo kwa mda mrefu lipo kwenye kampeni ulimwenguni kote kuzitaka nchi wanachama na wale ambao sio wanachama kufuta adhabu ya kifo,na pia hao walikamatwa China na nchi mbali mbali how sure kama wanamakosa tajwa kweli,je kama wamebambikiwa ama kusafirisha bila kujua?
Mungu anasamehe na kutoa nafasi ya pili iweje binadamu tushindwe hata kuwafunga maisha na kazi ngumu?
yote haya unayafahamu ila kwa makusudi unayaacha na kuandika yale yanayowapendeza wakubwa,si bure huenda kuna kitu unakitafta
 
Wenzetu ulaya na marekani waliokubuhu kwenye sayansi,hasa ya upelelezi,matumizi ya DNA wameanza kuwaachia baadhi ya waliohukumiwa kunyongwa,

Uchunguzi wa DNA ukifanyika upya,wanakuta aliyehukumiwa kunyongwa si muhusika taking accounpt uwezo mkubwa wa polisi kupika kesi.

Kama yeye anasahau idadi ya sheria(ile ya madawa)sembuse hii human justice inayofanywa na majaji
Demokrasia iko kwa wenzetu huko ambako mahakama inaweza kutengua agizo la raisi bila kujali kama yeye ndio anawapa pesa ama vp. Mr Trump chalii.
 
ha! we inakufaidisha nini..?
halafu mbona umekomalia au una lako jambo..
ingelikuwa mmoja wa ndugu yako yuko kwenye hilo kundi ungejisikiaje.. haya mambo hayahitaji haraka wengine humo usikute wamebambikiwa na wewe unasapoti tu.

kwa maamuzi ya mkulu jinsi yalivyo mi naomba apunguziwe baadhi ya madaraka maana tutaisoma kwelikweli
rudia kusoma kwa makini hili umuelewe mwandishi
 
Pasco mbona hii inshu ya kunyonga umeikomalia sana?
Huu ni uzi wa pili ama wa tatu kama sikosei
 
Wakati anaambiwa mayalla maana yake ni "njaa"nadhani ulikuwa ujumbe mzito.


:D:D:D:D:D:D

Hilo Siwezi Kulisemea Ni Wa Kwetu Huyo, Ni Upepo Mbaya Tu Umempitia Ila Akipata Hewa Safi Atarudi Kwenye Hali Yake Ya Kawaida Shaka Ondoa​
 
@Pasco tufautisha kati ya ujasiri na ukatili please,mfano Mkwawa alikua ni jasiri na fulani utawala wake ulikua wa kikatili na kupandikiza chuki
Bye bye
 
Back
Top Bottom