Mhasham Polycarp Pengo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

MAKONDA AKIOMBEWA NA MUFTI MKUU WA DAR ...JE HUU NI MFUMO KRISTO???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

Mkuu wa Dar Makonda, akiombewa Duaa na Mufti Mkuu wa Dar!
Wengine hatuoni tofauti ya maana kati ya Ukristo na Uislamu.

Zote ni dini. Dini hazitakiwi kuingilia uongozi wa siasa under the principles of separation of religion and state.

Hatuko Vatican, Zambia au Saudi Arabia hapa.
 
Mimi mahali ninapoona tatizo ni kwenye picha tu, nikiona mtu amefanyiwa maombi huku ameendaa wapiga picha nakuwa naona kama ni show off tu, hakuna jingine.
Kwahiyo alibeba na wandiishi wa habari kwamba twendeni mkanipige picha ninavyoombewa na Pengo.

Haka katoto kanatakiwa kakaendelee kunyonya tu
 
Kuombewa ni jambo zuri ila kuita mpiga picha hizo ni show off tu ndo alipoharibu labda angeiweka kwa matumizi binafsi hata bwana Yesu huwa hapendi show off hupenda moyo mnyoofu, tena hata ukifunga unatakiwa usijionyeshe kwa watu. Makonda apunguze show off huyu sijui ni mtumishi wa ngapi anapiga naye picha ki hivo

Haha hahaaaa. Imenikumbusha kisa cha Gwajima.
 
Kila mahala selfie huwezi kufanya jambo mpaka public awareness!!uzuri wa mkakasi huu
 
Hii ndiyo inaitwa kuchanganya dini na siasa! Hili ni gonjwa sugu kwa nchi yetu sijui litaisha lini? Ingekuwa kubadilishana tu mawazo sawa lakini kuombewa? Ni unafiki! Unaombewaje kwa imani usiyoiamini hata chembe? Hiyo ni kudhihaki imani za watu! Kikwete amekuwa akizungumza mara kadhaa na Pengo ila sijawahi kuona akiombewa!
 
Nashangaa watu waliokosa busara wala staha wanakurupuka kuweka topic za kulazimisha kuwa kuna udini nchini kwetu.... Yaani wanatafuta viupenyo vidogo vidogo ili wapenyeze propaganda zao na kuvuruga uhusiano mwema uliopo kati yetu. Mimi binafsi ni mkristo mwenye asili ya uislamu, zaidi ya nusu ya ndugu zangu upande wa baba ni waislamu. Mbona tunaishi kwa raha bila kubaguana ? Haya endeleeni kuizungungumzia na hii
ImageUploadedByJamiiForums1458922808.638251.jpg
 
2016%2B-%2B1


....................Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mhashama Polycarp Pengo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ............
Polycarp Pengo siyo Mhasham, wala siyo mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania.
Anaitwa Muadhama Polycarp Kardinali Pengo. Ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Nje ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam, hana mamlaka. Wahashamu ni Maaskofu na Maaskofu Wakuu ambao hawajafikia hadhi ya Ukardinali.
Nina imani Mohamedi Saidi unalijua hili ila unaandika hivyo kwa makusudi.
Wewe ni mmoja wa waandishi hodari na unayeaminiwa sana na Watanzania, tena wa dini zote.
Tafadhali endelea kulinda heshima yako.
Jitahidi kupunguza udini ndani ya nafsi yako.
 
Vipi kuhusu hili Sheikh Wangu?
 

Attachments

  • 2.JPG.jpeg
    2.JPG.jpeg
    40 KB · Views: 34
Chuki dhidi ya wakristo ndiyo inayokusumbua.

Kuna shida gani kama Raid au mkuu wa nkoa au kiongozi yeyote wa serikali kwenda kufanyiwa maombi kwenye ofisi au jengo la kiongozi wa kidini? Maana hapo hakufanyiwa maombi ofisini kwake. Na isitoshe kaombewa dua pia na watu wa dini yako- japo hilo hukutaka kuonesha ili malengo yako ya chuki yatimie.
 
Watu ni wajinga sana. Hivi Makonda kutembelea viongozi wa dini kwa ajili ya kujitambulisha ili wafahamiane, kuna tatizo gani?

Mnajua kama Meck Sadick alianzisha kamati ya aman dsm?

Wacheni udini wenu. Halafu kuombewa na viongozi wa dini haina maana sara hizo zimepokelewa. Ni maombi tu
 
2016%2B-%2B1


Kwa kiasi cha juma zima hivi mitandao ya kijamii imeweka picha hiyo hapo juu ya Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mhashama Polycarp Pengo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha imamuonyesha Kadinali Pengo akimfanyia maombi Bwana Makonda bila shaka akimuombea Mungu amuimarishe katika kazi yake mpya ili aifanye kwa ufanisi zaidi.
Paul Makonda amependa cheo kutoka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni hadi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya Waislam wameonyesha hofu kubwa katika tukio hili na nadhani hofu hii imetokana na dhana ya Mfumokristo katika serikali ya nchi yetu.

Binafsi nimeliangalia hili kwa jicho jingine kabisa nalo ni kuwa Mufti wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zubeir keshafunguliwa njia na kiongozi mwenzake wa kiroho.

Kadinali Pengo kadhihirisha kuwa vitu kama hivi vya kuwaita watendaji wa serikali ofisini na kuwaombea Mungu vinaruhusiwa.

Mwito wangu kwa wale wenye hofu kuwa labda wataambiwa ''wanachanganya dini na siasa,'' ni kuwa waondokane na hofu hiyo na wasaidie kuwaondoa hofu viongozi wa Waislam ili na wao waige mfano wa Kanisa Katoliki.

Itapendeza siku moja kuona picha ya mtendaji Muislam yuko ofisini kwa Mufti wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zubeir anasomewa Surat Yasin.

2016%2B-%2B1

Posted 1 hour ago by Mohamed Said
Don't panic my bro! Makonda ni binadamu na anahitaji kula kunywa kusali, nk. Kardinali hakwenda ofisini kwa Makonda kufanya hayo, bali Makonda alikwenda kwa Kardinali. Sasa ulitaka afanye nini na kazi yake yeye kama Kardinali ni kutoa the invisible? Kwa Maelezo yako ni kama untaka kusema basi kwa kuwa ni mkuu wa mkoa aache kwenda kanisani, which is nonsense!

Jambo baya ambalo limekuwa likifanyika ktk dini ya kiislamu ni kuwinda kiongozi wa juu kitaifa na kumfanya mgeni rasmi ktk sherehe ya kidini, hilo hutaliona ktk ukristu maana mwanasiasa hawezi kujigeuza kuwa bingwa wa biblia. Mgeni rasmi sherehe za Idd! Lakini kama Rais Muislamu anakwenda musikitini na kuombewa na Sheikh kuna kosa gani? Hapo ni himaya ya Sheikh, siyo Ikulu
 
Hivi umemsoma sawa Alama Mohamed Said? Au u punguani tu unakufanya utokwe na povu lisilo na mpango?
Sikiliza ewe punguani, kama angekuwa na nia ya kuonesha hakuna ubaya kwa makonda kuombewa na pengo(askofu) angeweka pia na picha ya makonda akiombewa na masheikh.

Hapo angebalance, na kusingekuwa na ligi
 
Back
Top Bottom