ndugu zangu wana jf. Nashukuru kwa mawazo yenu. Ila tunahitaji kuona mbali je mwaka 2015 tunataka tuishinde ccm au tunataka tupate viti kwa kuokoteza kama hivi vya sasa. Kama tunataka kushinda wapinzani wote washirikiana (chadema, nccr, cuf, udp na tlp), wagawane majukumu kama bunge lilopita. Huo ushirikiano ukuzwa kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Mfano chadema, udp, na nccr tlp, wanaweza kuungani tanzania bara ili kuwa na nguvu mwaka 2015. Nimeisema chadema na nccr, tlp udp kwa sababu maalumu. Sababu ni kwamba cuf haitaingia kwanye muungano wa kuunganisha nguvu za wapinzani mwaka 2015 maana yenye tayari ina mkataba na ccm wa serikali ya umoja kitaifa.ccm imetumia ila falasafa ya kikoloni ya divide and rule. Tukiruhusu ubinafsi yatatokea yale ya 1995, ugomvi kwenye kambi ya vyama vya upinzani ni mzigo katika demokrasia kwa nchi kama ya kwetu ambapo wananchi wataambiwa "wenyewe tu wameshindwa kushirikiana je tukiwapa nchi wataweza". Na ccm sasa hivi imejipanga/itajipanga kuhakikisha upinzani hautatulia, kutakuwa na mgogoro n.k. Naomba mungu usiwepo maana leo nchi yetu ingekuwa imekombolewa kama sio mgogoro wa nccr 1995-2000. Nashauri kwamba chadema au cuf wasing'aganie nani awe kiongozi wa upinzani, ila taratibu zinasemaje? Kama idadi ya wabunge inaruhusu yenyewe kiongozi wa kambi ya upinzani kama ilivyokuwa kwa cuf bunge lilopita, na cuf itoe naibu kiongozi wa upinzani bungeni. Pia tunahitaji kiongozi makini wa kambi ya upinzani si wa kupiga tu makelele awe na uwezo wa kujenga hoja na ana haiba ya kuwa raisi wa baadaye.
Pia nasashauri kila bunge linapo maliza vikao vyake wabunge wa upinzani muwe mnatembelea majimbo mbalimbali , hasa yale maeneo ambayo hamkupata kura za kutosha kupeleka matumaini mapya. Mfano "operesheni chakaza/sangara". Mkibaki tu mnapiga makelel bungeni, 2015 mtapigwa mwereka mpaka mtashangaa.
Na watanzania waliowapa matumaini watawalaani na mtakuwa mmewarudisha nyuma katika ndoto zao.
Naomba mpiganie tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.
Mungu awabariki
mawazo makomavu, point kubwa asante sana