Mh. Freeman Mbowe awe Kiongozi Mkuu wa upinzani bungeni

Tuache ushabiki Mbowe ndiye kaifikisha Chadema hapa ilipo angekuwa hafai wakati huu ungekuwa unaongelea APPT na si Chadema. CCM inataka watu kama kina Odinga Oginga na Morgan Tsvangirai, ukiwa mtu wa Yes bwana kama kina Cheyo watakutia vidole vya macho.
Kweli mkuu
 
Prof Mlambiti, Mwita Mwikwabe na Regia Mtema wameshafungua kesi mahakamani ya kupinga matokeo, hivyo idadi itaongezeka kwa kuwa ushahidi wao upo makini watashinda.
 
Hivi unavyosema kuwa Chadema imepata wabunge 22 una uhakika???

  1. Halima James Mdee -Kawe/Chadema
  2. Tundu Lissu - Singida Mashariki/Chadema
  3. Mustapha Quorro Akonaay- Mbulu/Chadema
  4. Israel Yohana -Karatu/Chadema
  5. John Mnyika -Ubungo/Chadema
  6. Silinde David -Mbozi Magharibi/Chadema
  7. Salvatory Naluyaga Machemuli-Ukerewe/Chadema
  8. Ole Sambu -Arumeru Magharibi/Chadema
  9. Joseph Mbilinyi -Mbeya Mjini/Chadema
  10. Philemon Ndesamburo Kiwelu-Moshi Mjini/Chadema
  11. Dk Antony Mbasa -Biharamulo Magharibi/Chadema
  12. Joseph Selasini -Rombo/Chadema
  13. Hezekiah Wenje -Nyamagana/Chadema
  14. Peter Msigwa -Iringa Mjini/Chadema
  15. Freeman Mbowe -Hai/Chadema
  16. Vincent Nyerere -Musoma Mjini/Chadema
  17. Godbless Lema -Arusha Mjini/Chadema
  18. Zitto Kabwe/C -Kigoma Kaskazini/Chadema
  19. Hayness Samson -Ilemela/Chadema
  20. John Shibuda -Maswa Magharibi/Chadema
  21. Meshack Opulukwa -Meatu/Chadema
  22. Sylvester Kasulimbayi Mhoja-Maswa Mashariki/Chadema

    [*]Regia Mtema / Chadema
    [*]Prof Mlambiti /Chadema

Hawa watoe, majimbo yao yalichakachuliwa na hivyo kutangazwa washindi wabunge wa ccm. Chadema ina wabunge wa majimbo 22 kwa mujibu wa tovuti ya bunge.
 
Ondoa Ole Sambu wa Aru Meru Magharibi (hakushinda). Weka Professa Kalikoyela Kahigi wa Bukombe/Chadema. Mwaka huu backbone ya CCM ilikukwa threatened. Hata kwangu Shinyanga was a surprise package (Majimbo 4). Umuhimu wa mikoa kwa wingi wa wapiga kura (top 10) ni;
  1. Mwanza (3)
  2. Dar es Salaam (2)
  3. Shinyanga (4)
  4. Mbeya (2)
  5. Morogoro (0)
  6. Kagera (1)
  7. Mara (1)
  8. Tanga (0)
  9. Iringa (1)
  10. Kilimanjaro (3)
In order of size (the largest 1st). Viti vya upinzani viko kwenye Mabano. Kilimanjaro, kiti cha TLP, kinaweza kuhesabika ni cha CCM tu.
 
By calculation, kwa kuwa chadema wana wabunge wa kuchaguliwa 22, na kuongoza Halmashauri zaidi ya 13, vilevile kwakuwa wamevuka lengo la kura za urais kwa kupata 26.1%, (Halali ni 49%) CHADEMA watakuwa na wabunge wa viti maalum zaidi ya 32.

Hivyo 22 + 32 = 54

Ndivyo itakavyo kuwa.
 
Nimekupata mkuu, nilipiga kwa idadi ya kura za rais lakini najua kura za ubunge zitazidi sana na zitaongeza viti maalum maana CCM waliwaza kupunguza kura za urais wakasahau kupunguza kura za ubunge sasa impact yake ndiyo wanaanza kui feel.
 
Prof Mlambiti, Mwita Mwikwabe na Regia Mtema wameshafungua kesi mahakamani ya kupinga matokeo, hivyo idadi itaongezeka kwa kuwa ushahidi wao upo makini watashinda.
Fred Mpendazoe vipi? hajafungua kesi?
 
Luteni,

Angalizo, CUF watadai wao ndio waunde serikali ya upinzani bungeni kwasababu wana viti 24 dhidi ya 22 vya CHADEMA. Pia CUF wanaweza kuungana kirahisi na NCCR, TLP na UDP.

Pia viti maalum vinategemea kura za ubunge kwahiyo CHADEM kitakuwa na viti karibu 20 kati ya 72 na sio 32 kama anavyodai huyo mdau mwingine, hapo nimechukulia CHADEMA watakuwa wamepata asilimia kama 30 ya kura za ubunge nchi nzima.

Itakuwa vizuri vyama vyote vya upinzani vikiungana ili kuunda serikali ya upinzani bungeni. Huenda Hamad akaendelea kuwa kiongozi wa hivyo vyama bungeni.
 
Kwa hilo kaka umenena,but am not sure kama CCM inaweza kutoa special seat 22 kwa chadema but Let us wait and see!Mapendekezo yako ya Mbowe awe Kiongozi mkuu wa upinzani bungeni naliunga mkono 100%:israel:
 
Luteni,

Angalizo, CUF watadai wao ndio waunde serikali ya upinzani bungeni kwasababu wana viti 24 dhidi ya 22 vya CHADEMA. Pia CUF wanaweza kuungana kirahisi na NCCR, TLP na UDP.

Pia viti maalum vinategemea kura za ubunge kwahiyo CHADEM kitakuwa na viti karibu 20 kati ya 72 na sio 32 kama anavyodai huyo mdau mwingine, hapo nimechukulia CHADEMA watakuwa wamepata asilimia kama 30 ya kura za ubunge nchi nzima.

Itakuwa vizuri vyama vyote vya upinzani vikiungana ili kuunda serikali ya upinzani bungeni. Huenda Hamad akaendelea kuwa kiongozi wa hivyo vyama bungeni.
Mkulima

Hapa si CUF wanadai ni kanuni zinasemaje na kuongoza kwa viti si vya majimboni tu bali ni total seats including viti maalum.

Chadema Viti majimboni 22 maalum approx 20 = 42
CUF viti majimboni 24 maalum approx 6 = 30

Hii inatokana na idadi za kura za wabunge walizopata kila chama ukizingatia CUF majimbo yake mengi yako Pemba ambako kura hazizidi laki 2 in total.

Hata kama wakiungana CUF NCCR TLP na UDP hawawezi kuifikia Chadema zitakuwa kama 30 CUF + 4 NCCR + 1 TLP + 1 UDP = 36 kwa vile vyama vingine havija- qualify kupata viti maalum. Na elewa hesabu ya viti vya Chadema ni minimum kwa vile kura za ubunge ni nyingi kuliko za urais.
 
Wana jf,tuche juu ya kulumbana nani awe nani juu ya kuanzisha serikali kivuli na mambo mengine kama hayo.
Binafsi naamini katika umoja ni nguvu,haijalishi kama unashirikiana na ni ila kama lengo lenu ni moja basi kuungana huleta nguvu.
Ni kweli viongozi wetu wengi ni wabinafsi (pengine hata wanamageuzi/wanamabadiriko),lakini ni muhimu sana kuonyesha picha sahihi ya wanamabadiliko kwa wananchi waliowachagua. Tuseme nini basi???chadema pamoja na cuf na vyama vingine vya upinzani(excluding mrema,simwamini hata kidogo) washirikiane kwa pamoja kuweza kuleta msukumo wa mabadiliko ya maisha na mifumo ya uendeshaji wa serikali kwa wananchi.nafahamu fika kuna wabunge wa ccm ambao hawako tayari kutekeleza matakwa ya chama na ku compromise misingi ya haki na utawala wa sheria. Hao nahesabu wana mchango mkubwa sana maana kukulacho kinapokuwa nguoni mwako cha moto utakiona.
Natazamia mabadiliko kwa kuweka viongozi wenye ushawishi zaidi,haijalishi kama ni wa cuf au chadema. Kumbuka kigezo kingine wanachokitumia wananchi kupima upinzani ni uwezo wao wa kuungana na kutenda kazi kwa kushirikiana.last parliament iliongozwa vizuri sana na kiongozi wa upinzani kutoka cuf,kwa hiyo natarajia the same hata kama chadema watashika uskani kwa kuongoza shughuli za upinzani bungeni.
Sitarajii kuona wapinzani wanaanza kuleta utengano.makubaliano ya january makamba na jussa hayana influence kabisa kwa system ya bunge maana jussa si mtu wa ushawishi kiasi hicho ndani ya cuf.
Mbowe ana uwezo wa kuongoza kwa sababu hatasimama kuto mawazo yake binafsi,atakuwa akisimama kuto msimamo wa vyama vya upinzani.
 
Siungi mkono Mbowe kuwa kiongozi wa upinzani, nadhani hiyo itaipa nguvu CCm kusema kwamba wapinzani ni wapenda vurugu na hooligans... Kumbukeni mbowe ana rekodi nzuri sana ya violence na short temper... Pia kwa watu wenye busara ndani ya chadema wanaelewa fuse yake fupi na ego imeikost chadema kwa kushindwa kuungana na wapinzani wengine na vilevile kuharibu harmony wakati ule wa uchaguzi wa chadema

I would advice wisdom i-prevail na si ushabiki

Mbowe hafai kuwa kiongozi wa upinzani bungeni...

Nakubaliana na wewe mkuu! Mbowe bado, busara inatakiwa kubwa sana kwa nafasi hii. Sidhani upinzani kwa sasa una nafasi ya kupeana vyeo kwa kuenziana, hili liachiwe CCM ndio zao. Huku ni kazi na kazi mpe mzigo yule anaweza kubeba, very strategic. Chadema tunategemea mengi mno kwenu
 
Wana jf,tuche juu ya kulumbana nani awe nani juu ya kuanzisha serikali kivuli na mambo mengine kama hayo.
Binafsi naamini katika umoja ni nguvu,haijalishi kama unashirikiana na ni ila kama lengo lenu ni moja basi kuungana huleta nguvu.
Ni kweli viongozi wetu wengi ni wabinafsi (pengine hata wanamageuzi/wanamabadiriko),lakini ni muhimu sana kuonyesha picha sahihi ya wanamabadiliko kwa wananchi waliowachagua. Tuseme nini basi???chadema pamoja na cuf na vyama vingine vya upinzani(excluding mrema,simwamini hata kidogo) washirikiane kwa pamoja kuweza kuleta msukumo wa mabadiliko ya maisha na mifumo ya uendeshaji wa serikali kwa wananchi.nafahamu fika kuna wabunge wa ccm ambao hawako tayari kutekeleza matakwa ya chama na ku compromise misingi ya haki na utawala wa sheria. Hao nahesabu wana mchango mkubwa sana maana kukulacho kinapokuwa nguoni mwako cha moto utakiona.
Natazamia mabadiliko kwa kuweka viongozi wenye ushawishi zaidi,haijalishi kama ni wa cuf au chadema. Kumbuka kigezo kingine wanachokitumia wananchi kupima upinzani ni uwezo wao wa kuungana na kutenda kazi kwa kushirikiana.last parliament iliongozwa vizuri sana na kiongozi wa upinzani kutoka cuf,kwa hiyo natarajia the same hata kama chadema watashika uskani kwa kuongoza shughuli za upinzani bungeni.
Sitarajii kuona wapinzani wanaanza kuleta utengano.makubaliano ya january makamba na jussa hayana influence kabisa kwa system ya bunge maana jussa si mtu wa ushawishi kiasi hicho ndani ya cuf.
Mbowe ana uwezo wa kuongoza kwa sababu hatasimama kuto mawazo yake binafsi,atakuwa akisimama kuto msimamo wa vyama vya upinzani.
Cuf ya leo si Cuf ya juzi wamebadilika sana wameonyesha hawako serious na ukombozi wa watanzania wako pale kwa maslahi binafsi kiasi kwamba tamaa inawatesa, si wa kuaminiwa kwa sasa. Muungano ni mzuri lakini si lazima uungane ilikufanikisha jambo. Ngoja nitumie maneno ya Mwanakijiji waungane ili wafanye nini.
 
Nakubaliana na wewe mkuu! Mbowe bado, busara inatakiwa kubwa sana kwa nafasi hii. Sidhani upinzani kwa sasa una nafasi ya kupeana vyeo kwa kuenziana, hili liachiwe CCM ndio zao. Huku ni kazi na kazi mpe mzigo yule anaweza kubeba, very strategic. Chadema tunategemea mengi mno kwenu
Hivi nyie mnatafuta busara ipi mtu kakitoa chama from no where hadi kinatikisa chama chenye miaka 50 bado mnasema hawezi. Kutoka wabunge watano hadi zaidi ya 40 hamuoni kitu, kumbuka hao wabunge wamepokonywa toka CCM. Hamuoni kaishusha CCM toka ushindi wa kishindo wa 80% hadi 60%. If you cant appreciate this little change hata akiletwa malaika aongoze huta appreciate.
 
Pia kuna majimbo bado hayajachagua wabunge, yakiwa ni:

Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa anzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)

Nafikiri hapo CHADEMA watapata jimbo moja huko Mpanda na CUF pia wataongeza majimbo yao Zanzibar.
 
Sema Cuf wataongeza jimbo lao la Wete Pemba.
 
Back
Top Bottom