Mganga Mkuu wa wilaya ya Singida, Dr. Erick Bakuza aachia ngazi

Acha mbwembwe wewe. Hao wabobezi wametufikisha wapi?
To support your argument, lete hapa ushahidi WA tija iliyoletwa na huyo unayemuita mbombezi
Naamini utakuta kesi za rushwa, kuuza madawa kutohudumia wagonjwa na madhaifu kadhaa kwenye hiyo Hospitali aliyokuwa anaongoza.
Binafsi nimepoteza imani watumishi wa Umma na wasomi wa Nchi hii. Ingewezekana tungefuta ajira zote tukaanza upya, kwa sasa ni mabingwa wa kulalamika bila kutimiza wajibu wao. Wao hawaangalii tija Bali Mahudhurio kazini
Wewe hapa umefanyaje kama sio kulalamika?
Hata matumizi ya jf ni matokeo ya wabobezi.
Lete ushahidi kujustfy unachokisema. Vinginevyo umeweka mbwembwe tu.
Kama umekosa imani nao achana nao.
 
watumwa huamini kuwa ni serikari tu zaweza kukidhi haja zao/mahitaji hivyo hubaki kuwa watumwa serikali daima hadi uzee wao!!!! hongera doctor
 
Nami nampongeza sana sana kwa kutokubali upuuzi wa wanasiasa acha waendelee na sifa za kijinga watajielewa wakitolewa......kuna mwingine w Kilwa kwenye mazingira magumu pia ameulizwa maswali ya kitoto na kipuuzi na RC wa Lindi (watoto wa kulipana fadhila)....yale maswali ni ya kitoto na kwa taalamuma yake hakutakiwa kuulizwa mbele ya umati vile......na kwa vile sio yeye alietuhumiwa anamnyanyasa namna ile kwa nini amepokea simu akiwa theatre jibu.....ni rahisi la common sense akiwa mule anazunguka na manesi na wasaidizi kibao tu wakiona simu inapigwa mara kwa mara na yeye kutambua unyeti wake na muda ataokaa mule ndani manesi huwa wanapokea na kumuwekea sikioni.....anaongea na kutoa maelekezo sahihi wajua DMO anafanya kazi za utawala nyingi za hospitali na anafanya operation......emergencies zote anapigiwa simu usiku wa manane......sio lazima umjue anaekupigia wewe unasikiliza shida na kutoa maamuzi hapo hapo.......RC wa Lindi amechemka sijui kichwani kuna mawashawasha yale au kuna kinyesiii
watumwa huamini kuwa ni serikari tu zaweza kukidhi haja zao/mahitaji hivyo hubaki kuwa watumwa serikali daima hadi uzee wao!!!! hongera doctor
 
Taratibu kamanda,wenye taaluma ndio hao kila siku mnawakandia humu na thread zako zipo.Lazima ifike wakati tuchukue maamuzi magumu,wakati wa maofisa waandamizi kama huyo kukaa ofisini na kupigwa kiyoyozi huku watu wanakufa kwa pindupindu umekwisha
Siyo! Sema kwa wengine siyo huyu! Tumesikia historia yake alikuwa mchapakazi.
 
Daaah yani nilivaa viatu vya huyu jamaa halafu nikamuangalia huyu mama sura yake tu inajieleza hana exposure wala elimu anapenda sana kuropoka
Mungu amlipe huyu jamaa hapa hapa duniani
 
Hakuna jipya hapo ya kulazimisha lionekane ni suala la ajabu.

Kama alidhani wakuu wake wa kazi wanakurupuka kwa nini hakwenda kwenye mahakama ya kazi?

Tanzania kuna sheria za kazi ambazo zinatafsiriwa kwenye mahakama ya kazi nchini.

Ninasema tena, kujiudhuru haijawahi kuwa ni suala la ajabu hasa kazi ambayo kuna mamia au maelfu ya watu wanaita hiyo kazi.

Kinachochekesha zaidi kuna watu wanampa pongezi halafu hao hao unawasikia wanalalamika wakisema kwa nini serikali haijatoa ajira. Tanzania kwa unafiki!
Hata hueleweki nini umeandika......
 
Kwa nini baadhi ya watu wanadhani ni kitu cha ajabu kwa mtu kujiudhuru wadhifa wake?

Mtu ambaye hakulazimisha kuajiriwa kwa nini iwe ni ajabu anapoamua kwa hiari yake kuondoka?

Kuna sheria za kazi nchini ambazo zimewekewa mahakama maalum na kwa maana hiyo alikuwa na haki ya kwenda mahakamani kama anadhani kuna kosa ametendewa lakini hakufanya hivyo bali ameamua kwa hiari yake kuondoka katika nafasi yake.

Nashangaa baadhi ya wanasiasa wanataka kulifanya kama ni jambo la ajabu. Au ndio aina ya siasa nyepesi nchini baada ya kukosa siasa zenye nguvu za hoja.

Hao hao wanaompa pongezi kwa kujiudhuru ndio hao hao wanapiga kelele kuiomba serikali itoe ajira.

Hizo nafasi zikitangazwa ninaamini kuna mamia au maelfu ya watanzania wenye uwezo wataomba ili kuzijaza.

Ukitoka wewe kuna wengine mamia au maelfu wanaitaka nafasi yako.

Kufa kufaana!
Mkuu pamoja na yote kitendo cha RC kumuweka lockup DMO ni vurugu na matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi. Ni kudhalilisha taaluma za watu na kukiuka taratibu za utumishi wa umma. DMO hajafanya kosa la uhalifu labda amefanya kosa la kiutendaji ambalo kuna taratibu zake za kuwajibishwa kupitia sheria za utumishi wa umma. Tusilee mambo kama haya yakizoeleka kutakuwa na vurugu sana na watu watakimbia kuitumikia nchi yao kupitia taasisi za umma.
 
Kwa habari kama ilivyo na kama ndivyo ilivyotokea , kuna mambo mawili

1. Nafasi ya mganga mkuu ni wadhifa tu katika utendaji katika eneo lake la kazi
Si nafasi ya kusomea bali ya kuteuliwa na wahusika.

2. Kuna Udaktari ambao ni sifa ya kitaaluma,inasomewa, si kuteuliwa au kuchaguliwa

Kama habari ilivyo na kama ni kweli, kipindu pindu ni suala la utaalam.

Anayeweza kusema ndicho au sicho ni mtaalam ambaye hapa pia ni mganga mkuu

Kama Dr angefuja pesa za Hospitali au kughushi jambo lolote angekuwa na makosa ya kihalifu, angeshughulikiwa kama mhalifu mwingine. Mkuu wa mkoa ana haki

Kama Dr ameficha kipindu pindu na ikathibitika kitaalam alificha kutoka kwa wataalam hilo ni kosa la kimaadili na kitaalam.

Mwenye dhamana ya kulishughulikia ni mganga mkuu wa wizara na baraza la madaktari
Baraza linaweza kumwadhibu kwa mujibu wa taratibu zake za kitaaluma.

Ni kosa ka mkuu wa mkoa kumwadhibu mtaalam kwa kosa ambalo hajui kitaalam kama ni kosa au la. Mkuu wa mkoa alijuaje kuna kipindupindu?

Kwanini hakuwasiliana na wataalam wa wizara kufikisha malalamiko yake?

Kuwaacha hawa Ma RC na DC ambao kazi zao ni za kisiasa kuingilia kazi za kitaalam ni kosa kubwa na tunapaswa kulilaani.

Ipo siku RC ataamuru mgonjwa afanyiwe operesheni la sivyo Dr anakwenda ndani.

Ipo siku DC ataamua dozi ya mgonjwa kinyume chake Dr anakwenda ndani.

Naungana na Dr kama kweli ameachia ngazi.
Ni mtaaalam anayeweza kufanya kazi popote pale na maisha yake yakaendelea.

Angeweza kubaki alipo bila uganga mkuu na hakuna wa kuondoa utaalam wake.

Dr hakuteuliwa au kuchaguliwa, alisomea!

Hatumbuliwi degree yake isipokuwa tu na chombo kinachosimamia taaluma.
Na kwa aliyeangalia leo Bunge, Wabunge wamekemea sana mienendo ya wakuu wa Mikoa kutumia vibaya KISIASA madaraka ya kuwaweka watu ndani. Tena mmoja wa Wabunge niliyemuona akichangia ni mtu mzito mstaafu wa Jeshi la Polisi kama sikosei ambaye ni Mbunge wa CCM kutoka katika jimbo moja la Mkoa wa Tanga. Ukiona hivyo amegundua kuna dosari.
 
Tatizo kubwa wengi wa watawala ni failures darasani hivyo wana inferiority complex wanayotembea nayo na kuziba gape hiyo ndio twaona madudu haya kwani pia wengi hawakubahatika kuwa na busara na hekima ya kuzaliwa nayo
 
Back
Top Bottom