Mganga Mkuu wa wilaya ya Singida, Dr. Erick Bakuza aachia ngazi

Mkuu wa wilaya ya Uyui alipoachia ngazi,watu mlidakia tu,mlipokuja kugundua aliwahi kuuwa mke,mkanywea na kukimbia humu.
Haya mpongezeni huyo dokta,kesho mtaambiwa alipaswa kuwa Rural medical officer ndipo mtashikwa na homa ya matumbo.
Kwa serikali hii,kama hupo fiti kimwil,kimaadili,kiakili na kieleimu kulingana na kulingana na cheo chako,utakimbia tu kazi
Haha ha! Au utaishia kusoma speech kama kasuku anayefugwa na mwarabu! Acha kudhihaki watu na taaluma zao kuntetea mwanasiasa wa hovyo anayetaka watu wave kwa kipindupindu
 
kama amesimama kwenye misingi ya taaluma yake inabidi tumpongeze wanasiasa wa sasa wanakurupuka inawezekana mkuu wa mkoa na phd anadhani anaweza kuwa na ujuzi sawa na dr aliyesomea miaka saba kutibu watu
 
Haha ha! Au utaishia kusoma speech kama kasuku anayefugwa na mwarabu! Acha kudhihaki watu na taaluma zao kuntetea mwanasiasa wa hovyo anayetaka watu wave kwa kipindupindu
Taratibu kamanda,wenye taaluma ndio hao kila siku mnawakandia humu na thread zako zipo.Lazima ifike wakati tuchukue maamuzi magumu,wakati wa maofisa waandamizi kama huyo kukaa ofisini na kupigwa kiyoyozi huku watu wanakufa kwa pindupindu umekwisha
 
Wewe una mahaba ya ajabu kweli, unajua hiyo hadithi ya kipindu pindu ilikuwaje? Subiri kidogo utaona yatakayo fuatia baada ya DMO kuacha kazi. Kuwa na subira utaelewa tuu
 
Hiyo Advanced Diploma ya Medicine ilikuwa inatolewa na chuo kipi na hiyo zamani ni zamani ipi?!
Wilaya nyingi zimeongozwa na AMOs kwa miaka mingi sana hata zingine na ma COs kama Acting DMOs kabla ya kuanza kuajiriwa MDs kipindi cha Rais Kikwete kushika hizo nafasi na sasa wengi wa DMOs wana MPH.
 
Wewe una mahaba ya ajabu kweli, unajua hiyo hadithi ya kipindu pindu ilikuwaje? Subiri kidogo utaona yatakayo fuatia baada ya DMO kuacha kazi. Kuwa na subira utaelewa tuu
DMO aliwekwa ndani kwa saa 3 kwa uzembe,na yeye kaona akatafute malisho sehemu nyingine,sawa ndio dunia
 
Kwa habari kama ilivyo na kama ndivyo ilivyotokea , kuna mambo mawili

1. Nafasi ya mganga mkuu ni wadhifa tu katika utendaji katika eneo lake la kazi
Si nafasi ya kusomea bali ya kuteuliwa na wahusika.

2. Kuna Udaktari ambao ni sifa ya kitaaluma,inasomewa, si kuteuliwa au kuchaguliwa

Kama habari ilivyo na kama ni kweli, kipindu pindu ni suala la utaalam.

Anayeweza kusema ndicho au sicho ni mtaalam ambaye hapa pia ni mganga mkuu

Kama Dr angefuja pesa za Hospitali au kughushi jambo lolote angekuwa na makosa ya kihalifu, angeshughulikiwa kama mhalifu mwingine. Mkuu wa mkoa ana haki

Kama Dr ameficha kipindu pindu na ikathibitika kitaalam alificha kutoka kwa wataalam hilo ni kosa la kimaadili na kitaalam.

Mwenye dhamana ya kulishughulikia ni mganga mkuu wa wizara na baraza la madaktari
Baraza linaweza kumwadhibu kwa mujibu wa taratibu zake za kitaaluma.

Ni kosa ka mkuu wa mkoa kumwadhibu mtaalam kwa kosa ambalo hajui kitaalam kama ni kosa au la. Mkuu wa mkoa alijuaje kuna kipindupindu?

Kwanini hakuwasiliana na wataalam wa wizara kufikisha malalamiko yake?

Kuwaacha hawa Ma RC na DC ambao kazi zao ni za kisiasa kuingilia kazi za kitaalam ni kosa kubwa na tunapaswa kulilaani.

Ipo siku RC ataamuru mgonjwa afanyiwe operesheni la sivyo Dr anakwenda ndani.

Ipo siku DC ataamua dozi ya mgonjwa kinyume chake Dr anakwenda ndani.

Naungana na Dr kama kweli ameachia ngazi.
Ni mtaaalam anayeweza kufanya kazi popote pale na maisha yake yakaendelea.

Angeweza kubaki alipo bila uganga mkuu na hakuna wa kuondoa utaalam wake.

Dr hakuteuliwa au kuchaguliwa, alisomea!

Hatumbuliwi degree yake isipokuwa tu na chombo kinachosimamia taaluma.
 
Hiyo Advanced Diploma ya Medicine ilikuwa inatolewa na chuo kipi na hiyo zamani ni zamani ipi?!
Level hiyo ya Advanced Diploma ya Medicine ilianza kutolewa miaka mingi sana nyuma Muhimbili kabla ya kuhamishia kada hiyo KCMC mwaka 1976 na mpaka sasa kuna vyuo kama 5 hivi vinatoa wahitimu 40 kila mwaka kwa chuo wa AMO.
 
Mimi naendelea kuhesabu. Washakua wawili.
Duh, unahesabu? Halafu unaona ni wawili, nakuambia ni wengi sana. Tena wabaya ni wale wanaosusa huku wanaendelea na kazi, juzi waziri Mkuu alitoa tamko na kuwapiga marufuku, lakini wanatia kiburi tu. Subili picha iendelee ni utawala huu tu, wakuu wa mikoa wanaweka watendaji ndani, tena huyu si ndio alikuwa mtangazaji au!!
 
Kwa nini baadhi ya watu wanadhani ni kitu cha ajabu kwa mtu kujiudhuru wadhifa wake?

Mtu ambaye hakulazimisha kuajiriwa kwa nini iwe ni ajabu anapoamua kwa hiari yake kuondoka?

Kuna sheria za kazi nchini ambazo zimewekewa mahakama maalum na kwa maana hiyo alikuwa na haki ya kwenda mahakamani kama anadhani kuna kosa ametendewa lakini hakufanya hivyo bali ameamua kwa hiari yake kuondoka katika nafasi yake.

Nashangaa baadhi ya wanasiasa wanataka kulifanya kama ni jambo la ajabu. Au ndio aina ya siasa nyepesi nchini baada ya kukosa siasa zenye nguvu za hoja.

Hao hao wanaompa pongezi kwa kujiudhuru ndio hao hao wanapiga kelele kuiomba serikali itoe ajira.

Hizo nafasi zikitangazwa ninaamini kuna mamia au maelfu ya watanzania wenye uwezo wataomba ili kuzijaza.

Ukitoka wewe kuna wengine mamia au maelfu wanaitaka nafasi yako.

Kufa kufaana!
Mbona povu linakutoka, unaacha kuongelea kiini cha tatizo unaongelea matokeo duh pole sana.
 
Wilaya nyingi zimeongozwa na AMOs kwa miaka mingi sana hata zingine na ma COs kama Acting DMOs kabla ya kuanza kuajiriwa MDs kipindi cha Rais Kikwete kushika hizo nafasi na sasa wengi wa DMOs wana MPH.
Hoja yako hasa ni ipi?!
 
Mkuu Nguruvi3,

Uliyosema ni ukweli mtupu! Jambo ambalo sijathibitisha ni kwamba, kiprotokali ni RMO ndie alikuwa na mamlaka ya kutangaza mlipuko wa kipindupindu!!!

Tusisahau, ni majuzi tu hapa Dr. Mwele Malecela ametumbuliwa kwa madai ya kutangaza Zika wakati huo sio wajibu wake!!!

Na kama ulivyosema, daktari hawezi kukosa kazi hata siku moja! Kwanza, ikumbukwe kwamba, alianza kupiga chini Ukuu wa Idara ambao ndio ulikuwa unampa nafasi ya u-DMO! Baada ya kupiga chini ukuu wa idara, akabaki kama daktari wa kawaida... bila shaka, alikuwa anaweka mambo sawa kabla hajaachana nao rasmi!

Nadhani baada ya kuweka michakato sawa, ndipo akaachia ngazi jumla!!!!
 
Level hiyo ya Advanced Diploma ya Medicine ilianza kutolewa miaka mingi sana nyuma Muhimbili kabla ya kuhamishia kada hiyo KCMC mwaka 1976 na mpaka sasa kuna vyuo kama 5 hivi vinatoa wahitimu 40 kila mwaka kwa chuo wa AMO.
Duh! Sasa unatuletea habari za enzi za Mwalimu....!!!! Hivi hiyo 1976 si ndo kwanza bado TANU anamlia mingo ASP kabla hajamtundika ujauzito uliomleta toto tundu duniani....!!!
 
Kwa nini baadhi ya watu wanadhani ni kitu cha ajabu kwa mtu kujiudhuru wadhifa wake?

Mtu ambaye hakulazimisha kuajiriwa kwa nini iwe ni ajabu anapoamua kwa hiari yake kuondoka?

Kuna sheria za kazi nchini ambazo zimewekewa mahakama maalum na kwa maana hiyo alikuwa na haki ya kwenda mahakamani kama anadhani kuna kosa ametendewa lakini hakufanya hivyo bali ameamua kwa hiari yake kuondoka katika nafasi yake.

Nashangaa baadhi ya wanasiasa wanataka kulifanya kama ni jambo la ajabu. Au ndio aina ya siasa nyepesi nchini baada ya kukosa siasa zenye nguvu za hoja.

Hao hao wanaompa pongezi kwa kujiudhuru ndio hao hao wanapiga kelele kuiomba serikali itoe ajira.

Hizo nafasi zikitangazwa ninaamini kuna mamia au maelfu ya watanzania wenye uwezo wataomba ili kuzijaza.

Ukitoka wewe kuna wengine mamia au maelfu wanaitaka nafasi yako.

Kufa kufaana!

"Kujiuzuru" siyo "kujiudhuru"
Na taifa haliwezi kufika popote kama hoja za wataalamu zitaendelea kupuuzwa ovyo.
 
Wenyewe watakwambia ukisusa sisi twala ..,.............

Lakini Kuna haja ya wajuaji kuwaachia waendeshe wanavyotaka........

Watu wabunifu hawawezi kufanya Kazi na wakurupukaji..........

Wacha wakurupukaji wafanye kazi na wakurupaji wenzao................
Ila kweli. Hii ndo serikali ya (..)..ovyo sana.mnaingilia sector zisizo za kwenu...tenaa?? Kuna hatari ya madaktari kugoma..maana mwakajana na hata mwaka huu..sector ya afya imeingiliwa kiasi kikubwa.mwisho wa siku hawa viongoz wa siasa nyingi tutawaachia wakatibu wao.tuone ...wamezidi sana.wanapoenda ni pabaya mno.sasa waendelee majuzi wameleta suggestion s za kuwapindua madaktari wasaidizi kua watumishi wa kawaida sasa hii ni hatari iko siku watagoma completely... Hii selikal ya saiv siipendi haina maadili.
 
Kuna hatari kubwa sector ya afya kua mbovu kihuduma kama siasa inaingilia taaluma zisizowahusu mnaaharibu systems za utoaji huduma kiujumla.na pia huduma ya afya haitatolewa kama selikali zilizopita.mnaleta siasa kazini mnatarajia huduma zitakua bora? Sasa mnawaletea hofu na kupungua kwa nguvu kazi za watumishi.mbona kipind cha nyuma hakukuepo muingiliano kama huu wa saiv...hii ni too much. Sasa mnaweza mkadhan kua mnaboresha kumbe MNA borosha...sasa iv hakuna mtumish wa selikali anaefanya kazi kwa amani na kujitolea. Zilikua ni enzi za nyerere,mkapa na angalau jakaya. But..nowadays take a look. Watu wanafanya kazi recklessly. Kwa sababu ya interruptions zisizokua na lazima.
 
Back
Top Bottom