SoC04 Mfumo wa wazi wa Kidijitali kufatilia utekelezaji wa miradi ya Serikali

Tanzania Tuitakayo competition threads

salve_claudio

New Member
Apr 21, 2024
4
1
Mfumo wa kidijitali wa ufuatiliaji wa Miradi ya Serikali Ili kuongeza uwazi. (Government Projects Tracking System).
Maendeleo ya Sayansi na teknolojia yamerahisisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi wake, huduma mbalimbi kama Elimu, Afya, Nishati ya umeme, Mawasili na usafirishaji n.k. katika kutoa huduma hizi miundombinu mbalimbali hujengwa. Miundimbinu hiyo ni kama shule, Hospitai, zahanati, Vituo vya Afya, Barabara, Miundombinu ya umeme, Kilimo, Ufugaji, Masoko n.k
Serikali kama chombo mojawapo kinachotoa huduma mbali mbali za kijamii kwa wananchi wake imekua ikitumia mifumo mbalimbali ya kidijitali katika kutoa huduma zake kwa wananchi, Mfamo kama FFARS inayosimamia matumizi ya fedha za serkikali, TAUSI inayosaidia kutoa leseni mbali mbabli za biashara. Hata hivyo kumekua na changamoto katika utekelezaji wa miradi mingi ya serikali
Changamoto
Katika vyombo vingi vya habari kumekua na kuripotiwa taarifa mbalimbali kuhusu kukwama kwa miradi mingi ya serikali kunakotokana na sabababu kadaha wa kadha. Matatizo mengi yanayoripotiwa ni kama yafuatayo;

Miradi kuchelewa kukamilika,
kumekua na kuripotiwa kuchelewa kwa utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya serikali, mfano unakuta kuna mradi wa ujenzi wa kituo cha afya uliotakiwa uwe umekamilika katika kipindi cha mwaka mmoja lakini unajikuta unakaa hata kipindi cha miaka mitano bila kukamilika, na inakuja kujulikana pale tu kiongozi mkubwa wa kitaifa anavotembelea miradi husika.

Miradi kutekelezwa chini ya kiwango.
Miradi mingine inatekelezwa chini ya kiwango kwa sababu ya ufatiliaji duni wa wasimamizi wa ngazi mbali mbali za halmashauri au hata usimamizi mbovu wa rasilimali fedha, Unakutana na Taarifa ya Daraja la miti liligharimu karibu milioni 150 , thamani ya pesa haionekani katika moradi iliyokua mingi, watu wasiokua na taaluma kusimamia miradi inayouhusu utaalamu.

Gharama za miradi zisizokua na uhalisia.
Miradi mingine kujulikana kutumia gharama kubwa kuliko uhalisia, Mfano ujenzi wa kibanda cha mlinzi katika ofisi moja ya serikali uligharimu kiasi kikubwa (milioni 20) kuliko uhalisia. Na hii ilikuja kugundulika pale Mheshimiwa waziri mkuu kasimu majaliwa alivofika katika ofisi husika.

Wakaguzi / Wasimamizi kushindwa kutembelea kila hatua miradi inavyotekelezwa
Hii inatokana na ukweli kwamba vyombo vya usafiri katika halmashauri zetu hazitoshelezi , hata pale usafiri unavopatikana kumekua na ukosefi wa pesa ya kujaza mafuta. hivo kuwapa ugumu wasimamizi na wafuatiliaji wa miradi mingi kutofikiwa kwa wakati katika mchakato mzima wa utekelezaji wa miradi husika, kwani ndani ya halmashauri moja kunaweklza kuwa na miradi mingi inayotekelezwa kwa wakati mmoja.

Changamoto kama hizo na nyingine niyingi zimekua zikigundulika pale viongozi wakubwa wa kitaifa mfano Raisi, mawaziri, wanavotembelea katika miradi husika au wananchi wanaozunguka miradi husika wanapoamua kushirikisha umma kupitia mitandao ya kijamii.

Nini kifanyike ?
Serikali kupitia Tamisemi ije na mfumo wa kidijitali utakaosaidia katika kufatilia utekelezaji wa miradi yake. Mfumo huu utakua na moduli mbalimbali ambazo zitahakikisha:

kila msimamizi wa mradi anasajili mradi anaousimamia katika eneo lake. Miradi itasajiliwa na wasimamizi ikieleza kwa kina Jina la mradi, mfadhili, gharama za mradi, mategemeo ya kukamilika kwa mradi na hatua mbali mbali zitakazopitiwa katika kutekeleza mradi husika. Na taarifa hizi ziwe wazi kwa mtu yeyote anaetaka kujua taarifa hizi azione katika mfumo utakaokua umetengenezwa. Pia
Msimamizi abainishe pesa aliyopokea kwa ajili ya utekelezaji mradi husika,

Msimamizi atahuisha matumizi ya pesa husika kwa kila hatua anayosimamia. Ndani ya mfumo kuwe na moduli inayoruhusu msimamizi kujaza taarifa za hatu ya mradi ulipofikia ukiambatana na Picha za mradi, paoja na gharama za pesa zilizotumika mpaka mradi ukipofikia.

anahuisha taarifa za hali ya mradi anaosimamia kwa kila hatua, hapa msimamizi aweze kusema kama mradi imekwisha, umesimama, au unaendelea, kama umesimama atoe na sababu za kusima aunkukwama kwa mradi husika, ili mamalaka zichukue hatua mapema.

Kuwe na Dashboard inayoonesha maendeleo ya Utekelezaji wa miradi husika katika ngazi zote za juu, waziri na viongozi wengine wa wizara husika wakitaka kuona miradi mbalimbali katika halmashauri zote nchini waweze kuiona hata wakiwa ofisini, wanaweza kuchuja kuona miradi iliyosimama tu na kujua shida zake au ile inayoendelea kwa kujiridhisha na picha zilizopandishwa na wasimamizi waliopo eneo la mradi, pamoja na matumizi ya fedha kwa kika hatua
Nini faida za mfumo huu.
Urahisi wa ufatiliaji, sio lazima viongozi wasafiri kilomita nyingi kwenda kujua maendeleo ya miradi inayotekelezwa.

Nini faida za mfumo huu?

Kuokoa gharama
, ile pesa ambayo ingehitajika kwa viongozi wengi kutembelea miradi husika kwa inaweza kutumiaka mahala pengine.

Kuweka Uwazi wa miradi inayotekelezwa, hii itaweka uwazi kwani Umma wote utakua na uwezi wa kujua namna miradi mbalimbali inavotekelezwa na kukemea pale inapotokea mradi husika hautekelezwi kwa ufanisi.

Kuhamasisha uwajibikaji kwa wasimamizii wa miradi mbalimbali, wasimamizi wa miradi watajitahidi kusimamia miradi kwa ufanisi kwani wanajua taarifa za miradi hiyo zinaonekana kote duniani.

Kurahisha na kuharakisha ufikiwaji wa huduma kwa wakati kwa wananchi, miradi ikikamilika kwa wakati , maana yake hudumq kwa jamii zinafika kwa wakati
Mfumo wa kidijitali wa Kufatilia utekelezaji wa miradi ya serikali (Project Tracking System) utawezesha wadau mbalimbali kuweza kufatilia na kujionea maendeleo ya Miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia vifaa janja kama simu, kompyuta na vishikwambi.

Hapa chini ni baadhi ya changamoto zilizogundulika mpaka pale viongozi walivo tembelea miradi hiyo, kitu ambavho kingeweza kuonekana hata kabla ya viongozi husika hawajafanya ziara hizo
images (13).jpeg

Chanzo: msasaonline.co.tz

images (12).jpeg

Chanzo: madumah online media

Hivyo nashauri mfumo huu wa kidijitali utadaidia katika kupunguza changamoto kama hizo na nyingine nyinginzinazoikumba miradi yetu na pia kuweka uwazi wa taarifa kwa Umma.
 
ila msimamizi wa mradi anasajili mradi anaousimamia katika eneo lake. Miradi itasajiliwa na wasimamizi ikieleza kwa kina Jina la mradi, mfadhili, gharama za mradi, mategemeo ya kukamilika kwa mradi na hatua mbali mbali zitakazopitiwa katika kutekeleza mradi husika. Na taarifa hizi ziwe wazi kwa mtu yeyote anaetaka kujua taarifa hizi azione katika mfumo utakaokua umetengenezwa. Pia
Msimamizi abainishe pesa aliyopokea kwa ajili ya utekelezaji mradi husika,
Naona itasaidia sana katika ufuatiliaji.

Naona wewe umeweka wazi kwamba kila mwananchi atakuwa na uwezo wa kifuatiloa na kuhoji maendeleo ya miradi inayomuhusu. Nzuri.

Hivyo nashauri mfumo huu wa kidijitali utadaidia katika kupunguza changamoto kama hizo na nyingine nyinginzinazoikumba miradi yetu na pia kuweka uwazi wa taarifa kwa Umma.
Wazo zuri tu mi nnaona
 
Back
Top Bottom