Mfanyakazi aliyepo masomoni Japan kwa miaka 13 kuchunguzwa/kushitakiwa

UCHUNGUZI UKIKAMILIKA SIO TU WAFUNGWE AU KUFUTWA KAZI BALI WARUDISHE HELA ZETU HATA KAMA KWA KUFILISI MAKABURI YA WAZAZI WAO.
 
Anaenda Bachelor 3yrs, anaextend for masters 2 years, then PhD 5 years halafu anafanya internship 2 years. Mshahara unaingia. Akimaliza anaajiriwa huko huko
Kwa mtindo huo Serikali isimlipe
 
Duh milioni 54 mtu anavuta kiulainiii. Anyway, ni kama kiasi cha mboga ya siku nne huku kwetu Muleba.
Duh!
Huko Muleba mna maisha bora kwa kila mkaaji wa Muleba!

Kwenu bilioni moja ni pesa ya mboga kama alivyotueleza Mama yetu, Tibaijuka
 
Nikweli kaanzia huko dalasa la kwanza mpaka fm 4 ukijumlisha miaka 7 +4=13 hiyo ujue kaanza kuajiriwa ana miaka 7 hii nchi sijui ingefika wapi!!+
Mkuu acha tu,hapa Tanzania kuna mambo ya kijinga sana yanafanyika ukiyaona utashangaa mwenyewe...
 
Hili zoezi lingefanyika kwa kuangalia wanao sign daftari la mahudhurio kazini na wale wasiokuwepo bila ruhusa maalum wachukuliwe hatua. Hii njia iliyotumiwa kwenye zoezi lililopita na halmashauri nyingi lina udanganyifu mwingi sana. Kuna wafanyakazi waliondoka vituoni kiujanjaujanja na kwenye uhakiki walirudi wakaonyesha barua za ajira na kuthibitishwa kazini halafu wakaondoka zao. Walio futwa kwenye malipo ya mishahara ni wale tu ambao siku zile za uhakiki hawakujitokeza
 
Naisi jamaaa alikua anaimanasha ya kuwa mabaya ni mengi kuliko mazuri. 89% kwa 11%

Pamoja na hayo, mimi binafsi kwa kuzingatia uzoefu wangu katika nchi hii na ule wa kitaaluma, siamini kuwa mabaya ya CCM ni mengi kuliko mazuri. Ni kweli CCM imefanya mabaya lakini nakuthibitishia mazuri ni mengi kuliko mabaya. Ila ni kawaida kwa binadamu kuangalia mabaya tu ya wengine... Mjadala wa mazuri na mabaya ya CCM ni mpana, kwa leo tuishie hapo.
 
Hebu tutajie Mazuri ya CCM kama yapo!

Hii hoja inahitaji mjadala mpana kwa leo nimebanwa kidogo, ila zuri mojawapo la CCM kwa maana la serikali ya CCM ni ule uhuru wa kutoa mawazo na ambao unawafanya wengi ukiwemo wewe kutoa maoni yao kwa uhuru bila kuingiliwa kwenye mitandao kama humu JF. Baya mojawapo la serikali ya CCM ni kushindwa kudhibiti rushwa na matumizi ya raslimali za nchi hii...
 
unamtumbua mtu hewa,.unamwacha lugumi na 37.763trillions
serikali ya vichekesho........
time will tell
 
Duu huyo atakuwa had I huko japani hayupo huko na waananga wa USA beby mwezin wakifanya utafit mwezin
 
NYIE AMJUI HUYO CHA MTOTO SUBIRINI YA MTWARA HIO N MICHONGO ATI WAKIRUDI NA WALE WA BOT AMTAGUSA TENA JF LOH
NCHI IMEOZA
 
Halafu RC Mecky Sadick anasema amesababisha hasara kwa serikali shilingi milioni 54 tu kwa muda wotw huo! Labda hesabu hazijakaa sawa.
Kumbuka miaka ndani ya ruhusa halali ya masomo haiwezi kuhesabika kama ni hasara hivyo hasara itakuwa kwa miaka nje ya ruhusa.
 
Du!
Jamaa anasoma miaka 13!
Akirudi si atafanya kazi kwa miaka 3-5 halafu anastaafu!
Kweli suala la watumishi hewa lina mambo.
Huyo kasoma hadi nyuma ya Ubao ni zaidi ya kusoma hapo na Sasa pengine ni raia wa Japan .
 
Back
Top Bottom