Mfanyakazi aliyepo masomoni Japan kwa miaka 13 kuchunguzwa/kushitakiwa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,997
SUALA la kusaka watumishi hewa limeendelea kushika kasi nchini baada ya mikoa kadhaa kutangaza kuikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza kwa kina huku watendaji waliohusika wakisimamishwa kazi.

Mkoani Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa huo, Said Mecky Sadiki, ameagiza kusimamishwa kazi Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, William Msapali na kutaka Takukuru imchunguze mtumishi Agapit Chuwa aliyepo masomoni nchini Japan kwa miaka 13.

Sadiki, ameagiza Halmashauri ya wilaya ya Mwanga kumsimamisha kazi Msapali kwa madai ya kushindwa kutoa ushirikiano wakati wilaya hiyo ikihakiki watumishi hewa na kuwabaini 21 ambao wameisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 199. Alisema tuhuma nyingine kwa Msapali ni kushindwa kubainisha taratibu zilizomruhusu mtumishi wa sekta ya afya, Chuwa ambaye mwaka 2004 aliomba kibali kwenda masomoni nchini Urusi ambapo alijiongezea muda na sasa yupo nchini Japan huku akilipwa mshahara.

Sadiki aliitaka Takukuru pia kumchunguza mtumishi huyo aliyepo masomoni kwa zaidi ya miaka 13 kwani ameisababishia serikali hasara ya Sh milioni 54. Kutokana hilo, Sadiki alitaka taratibu kufanyika ili kusitisha mshahara kwa mtumishi huyo na kuitaka Takukuru kufanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na baadaye kumfikisha mahakamani mtumishi huyo aliyepo masomoni na wengine wote walioisababishia serikali hasara.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jamhuri William alisema hakuna kumbukumbu za kutosha za taarifa za Chuwa ingawa alipewa ruhusa ya miaka mitatu kuanzia mwaka 2004.

Alisema mtumishi huyo alikuwa akijiongezea ruhusa kwa kushirikiana na maofisa Utumishi waliokuwapo ingawa baadaye tena alipewa ruhusa nyingine mwaka 2014 hadi 2016 kuendelea na masomo katika mazingira ya kutatanisha.

Alisema barua ya kuomba ruhusa ya mtumishi huyo iliandikwa lugha ya Kijapan lakini pia kwa Kiingereza ambacho hakikuwa kinasomeka vizuri jambo lililosababisha badala ya kupewa ruhusa ya miaka miwili, akapewa ya miaka mitatu.

Awali katika taarifa yake kwa mkuu huyo wa mkoa, Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaibu Ndemanga alisema wilaya hiyo yenye jumla ya watumishi 2,048 ilitambua watumishi hewa 21 walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 199.

Alisema walitumia hati ya malipo ya Septemba mwaka jana na kwenda katika kila ofisi kujua kama wahusika wapo ofisini ambapo 17 walikuwa wagonjwa, 14 waliomba ruhusa, 20 walikuwa likizo, 26 watoro, 26 walihama lakini bado walisomeka kwenye hati ya malipo.


CHANZO: Habarileo
 
Hili zoezi la wafanyakazi hewa tutaona na kusikia mengi!

Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela ambaye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa karibu sana na Rais Magufuli kumewaibua Wakuu wa Mikoa na taasisi mbali mbali ambapo wamefahamu kwa sasa dhana ya business as usual ni historia katika serikali ya Rais Magufuli. You reap what you sow!

Kadri zoezi linavyofanyiwa uchunguzi zaidi ndivyo wafanyakazi hewa wanazidi kuongezeka.

Wafanyakazi hewa kwa sasa ni kaa la moto kwa viongozi wakuu.
 
Duh milioni 54 mtu anavuta kiulainiii. Anyway, ni kama kiasi cha mboga ya siku nne huku kwetu Muleba.
 
Du!
Jamaa anasoma miaka 13!
Akirudi si atafanya kazi kwa miaka 3-5 halafu anastaafu!
Kweli suala la watumishi hewa lina mambo.
 
Anaenda Bachelor 3yrs, anaextend for masters 2 years, then PhD 5 years halafu anafanya internship 2 years. Mshahara unaingia. Akimaliza anaajiriwa huko huko

Itakua alikua anaSUP kila mwaka.
 
Kuna taasisi zimefanya Utumishi wao chuo kikuu. Anasjirwa Mtumishi f6, Anapelekwa chuo kwa fedha ya serikali 1year bure hailipi. Anafanya kazi analipwa mshahara. Baadaye let say after 5 years anapelekwa university 3 au 4years. Mshahara unaingia na stahili nyingine, analipiwa gharama zote n za kusoma na serikali mpaka ana graduate. Halipi chochote kugharamia elimu yake. Waliopewa mikopo Na HELSB wanadaiwa ajira hawana. Watumishi wanaolipwa mshahara na kulipiwa masomo bure imekaaje?
 
Miaka 13 masomoni wakati tuofanya kazi kwa kina Patel tunanyinywa siku moja ya kwenda masibani hii ni aibu kwa utumishi bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…