Mfahamu Zodiac Killer, muuaji aliyeitikisa Marekani

kuna crime moja nimeisahau jina huyo jamaa alikuwa anaua watoto tu.ilisababisha huo wa marekani uingie hofu ya kutisha ya kupotea watoto.jamaa katika interogation anasema aliamua kuua watoto sababu wakikua watakutana na changamoto kubwa za kimaisha kama zake hivyo akaona bora awasend afterlife
mkuu huyo jamaa akili zimefyatuka
 
Mtu huyu alikuwa akijitambulisha kwa jina la Charles Range Kichune, Josephat Chacha, Charles Joseph Msong’o (38) mkazi wa Kijiji cha Kenyamanyori Kata ya Turwa wilayani Tarime.
Mkuu kama unaifahamu ilivyokuwa itupie
 
Mkuu kama unaifahamu ilivyokuwa itupie
MTU anayedaiwa kuwa ni jambazi anayeua raia wasiokuwa na hatia katika vijiji mbalimbali Wilaya ya Tarime mkoani Mara, amekamatwa. Muuaji huyo anayetembea na bunduki ya SMG, alikamatwa juzi katika Mkoa wa Tanga, wakati akitoroka baada ya kuua watu 10 wasiokuwa na hatia mwishoni mwa mwezi Januari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya, Justus Kamugisha alisema mtu huyo alikuwa akitumia majina mengi kwa ajili ya kumfanya asitambulike haraka na kwa urahisi.

Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, mtu huyo amekuwa akijitambulisha kwa jina la Charles Range Kichune, Josephat Chacha, Charles Joseph Msong’o (38) mkazi wa Kijiji cha Kenyamanyori Kata ya Turwa wilayani Tarime.

“Mtu huyu amekamatwa mkoani Tanga Februari 6 majira ya saa 1:30 jioni. Hata hivyo hakuwa na silaha yoyote ndani ya begi lake la nguo. Takribani raia 10 wameaga dunia kwa kuuawa na mtu huyu, ambaye amekiri kuhusika na matukio hayo yote.

“Baada ya kumweka chini ya ulinzi na kuanza kumhoji, ndipo tukagundua kuwa si yeye peke yake anayefanya matukio haya bali wako wengi japokuwa aliyekuwa akifahamika ni yeye tu,” alisema.

Kamanda Kamugisha alisema, alipohojiwa zaidi mtu huyo alieleza ilipo silaha anayoitumia na kuwaomba askari kuwapeleka alikokuwa ameificha.

“Polisi mkoani Tanga waliondoka hadi mkoani Mara, ambapo aliwafikisha kwa jambazi mwenzake aliyemwachia baada ya kuona kuwa Jeshi la Polisi limeanza kumtafuta.

“Aliwapeleka maofisa wa Jeshi la Polisi hadi Kijiji cha Bweri Musoma mjini, kwa mwenzake aliyemtaja kwa jina la Marwa Keryoba au Alex anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 38, ambaye ni mkazi wa Sirari akiishi Musoma.

“Wakati polisi wanaingia kwa Keryoba, aliwasikia na kutoka nje akiwa amevaa koti refu jeusi kisha kulitupa chini kwa lengo la kupoteza mwonekano wake.

“Hata hivyo polisi walipiga risasi juu kumtaka ajisalimishe, japo alianza mashambulizi kuwashambulia maaskari hao.

“Askari walimuua Keryoba kwa kumpiga risasi baada ya kukaidi amri ya Jeshi la Polisi, lililomtaka ajisalimishe, kwa vile alikuwa amebeba silaha ya SMG iliyokatwa kitako na mtutu huku imefutika namba,” alisema Kamugisha na kuongeza:

“Baada ya kumpekua walimkuta akiwa na vitu vifuatavyo, SMG iliyofungwa tochi kwenye mtutu, magazine moja yenye risasi kumi na kwenye nyumba aliyokuwa anaishi marehemu zilipatikana simu mbili za mkononi.

“Vitu vingine ni CD 21 za picha mbalimbali, deki moja, viatu pea mbili aina ya buti, tochi mbili na mpira wa baiskeli pamoja na bidhaa mbalimbali za dukani,” alisema.
 
Haya matukio alikuwa akitafanya saa ngapi? Usiku? Mchana? Je hizo risasi alizokuwa akizikifyatua zilikuwa hazitoi sauti? Ilikuwaje watu washindwe kumwona mtuhumiwa na kumwacha atokomee pasipojulikana kirahisi namna hiyo?

Yapo maswali mengi ambayo tanahitaji majibu.
Ahsante kwa story.
 
Big up mkuu Mark @pawelk kwa nyuzi zako murua..naona wadau wamemzoea zaidi The Bold ktk story hizi.
 
Asante mkuu. Uendelee kutujuza zaidi. Naomba utuletee kisa cha J. Edgar Hoover director wa FBI aliyekaa madarakani miaka 40 chini ya marais 6 tofauti
 
Ndo kusema srkl ilishindwa kumvhukulia hatua maana ina mkono mrefu so ushaidi wa kumtia nguvuni ulikosekana au
 
Kuna mwingine aliitwa Papaa Lufungulo kule Kigoma,naye alifanya mauaji ya kinyama na kikatili sana
 
Back
Top Bottom