sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,488
- 4,619
Membe atulie majipu yakamuliwe kwanza.
Membe katumwa na watu au mtu sio yeye labda kuna jambo limeingia anga zake kana kwamba ana PANIC Tusubiri
Membe atulie majipu yakamuliwe kwanza.
Arudishe zile za libya kwanza maana nayeye ni jipu
Nafikiri Membe sasa ameamua kuwa "sauti iliayo nyikani" akiwakilisha msimamo wa serikali ya awamu ya nne chini ya JK. Waliokuwa wakiitetea kwa nguvu kwa kila kitu waache unafiki na kuungana na Membe.
HALAFU huenda amepata jeuri baada ya kuona spidi imepungua. Mwanzoni kwa jazba iliyokuwepo tuliaminishwa kuwa kufikia leo wakwepaji wakubwa wa kodi watakuwa angalau wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuhujumu uchumi. Lakini yaelekea "busara" imetumika na makubaliano muafaka (amicable) yamefikiwa kuwaacha walipe taratibu ili uchumi usitikisike!
Kwa mwenendo huu nina mashaka kama tutasikia mchakato wa kuunda mahakama ya mafisadi ukianzishwa. Kama Pinda naye alivyosema, inabidi mafisadi waendewe taratibu ama sivyo nchi itatikisika.
Basi tusishangae Membe kapata wapi jeuri ya kuongea kinyume na mtazamo wa wananchi kuhusu kasi ya awamu ya tano. Magufuli ajue tu kuwa ana kazi ngumu sana ambayo watangulizi wake hawakuwa nayo. Ajiandae vyema. Mapambano yake na upinzani yatakuwa haba kulinganisha na atakavyokwaruzana na "wasaliti" ndani ya chama.
kama ccmmm ni moja mbona Karume anazomewa kwa kuwa mkweli, yeye na membe nani anastahili heshima!!!!!Mkuu unaongea CCM ipi? Kumbuka CCM si moja na Membe ni mwanachama halisi wa CCM. Bona fide genuine kama anavyosema mkuu Pasco.
Kampuni zake zinatumia majina gani mkuu?Ukanda wote wa kusini kafungua vituo vya kuuza mafuta
Utanilaum bure aliyesema ni membe,soma uelewe ndo ukomenti..sio kukurupuka tu.Wewe ni lofa kabisa! Unataka wafanyabiashara wasilipe kodi? Huyu Bw Membe si vema akakaa kimya tu. Yeye anafurahia mabilioni kutapanywa kwenye mahoteli kwa shughuli zisizo na tija??
Hakuna anayeweza kuanzisha vita dhidi Raisi wa JMTZ ndani ya TanZania na akashinda labda iwe vita kutoka nje ya mipaka ya TanZania na siyo ndani, sababu ni kwamba kutangaza Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ ina maana unatangaza Vita na Nchi ya TanZania, hivyo nchi ya TanZania itatumia arsenal yake yote dhidi yako na hakuna mwenye huwo ubavu, subiri utaona kama ni kweli ametangaza Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ atanywea TU!
Katiba yetu inampa Raisi nguvu nyingi sana na kamwe hauwezi kupingana naye na ndio maana Mlm.Nyerere aliweza kuchukuwa Shule, Hospitali nyumba ktk kwa Makanisa, Misikiti na Wafanyabiashara wakubwa wa Kizungu, Wakihindi na Wakiarabu!
Hivyo kuanzisha vita dhidi Raisi wa JMTZ ndani ya TZ ni kutokuwa na akil na wenye akil wamekaa kimya Kuanzisha vita na rais aliyechaguliwa na majority ni ngumu sana kushnda lakini kwa huyu wetu aliyepatika kwa minority people ni mwepesi sana,mbaya hata waliomchagua wameanza kumgeuka.
unachokiongea ni kizuri kabisa, tatizo la Tanzania wanaofanya Maamuzi hawajui hata wanachokiamua. Ni ngumu sana mtu kasomea Afya, halafu leo anapitisha kodi, hajui lolote. Kuna umhimu wa kuwa na jopo la wataalamu wa kuwaelimisha watu kuhusu mambo ya kodi, ushuru wa manispaa, na gharama zingine zote.Suluhisho ni kubadilisha sheria za kodi kila mtu alipe kodi inayostahili na inayolipika, sheria ya kuruhusu afisa wa kodi akadirie anayoona inafaa ndio inawalazimisha wafanyabiashara watoe rushwa kwa hawa maafisa wanakupiga kodi ya juu makusudi, ijulikane kama in kontena la matairi na limenunuliwa kwa sh.100 kodo ni asilimia ngapi na kama ni gari imenunuliwa kwa sh50 kodi ni asilimia ngapi kwa sasa unaagiza gari wanakupigia hesabu ya kodi,ukileta bandarini kodi inapanda hii si sawa, Apeleke mswaada wa sheria ya kodi bungeni ibadilishwe, hii iliwekwa ili watu wapige pesa na kuwapendelea watu wachache, na wafanya biashara waache kujipendekeza kwa cccmmm, wasimamie na sheria zitakazowezesha kufanya biashara kwa uhuru sio kutegemea kubebwa na wanasiasa.
mkuu hiyo avatar yako!Naona Membe anataka kuwachezesha ngoma yake yeye UKAWA.
Ha ha anahamu ya kuondoka bungeni huyuKwa sasa washauri wa nje ni muhimu,wale waliopewa vyeo hawana jeuri ya kumkosoa Magufuli.nilimsikia mbunge Msukuma akisema watafata yote atakayoagiza Magufuli
Huu sio muda wa kuangalia nani mfadhili. Kwahiyo sisi watu wachini tuendelee kunufaika kisa wafadhiri wa ccm kwenye kampeni. Sasa wakiendelea tutaitoa hiyo ccm na upinzani kuingia ili waishie kula hasara tu. Kwanza hakuna urafiki kati ya serikali na mfanyabiashara. Kama utakuwepo kuna watu watakuwa na persenal interest si bureMembe anamtahadharisha kuwa:
1. Atambue Wafanyabishara ndio Wafadhili wakuu wa CCM.... Hivyo lazima walindwe kwa maslahi ya Chama Chao.
2. Akumbuke Mchango wa Wafanyabiashara ktk Harakati zake za Uraisi.......
Hongera Membe kwa angalizo.
Mkuu.Hakuna anayeweza kuanzisha vita dhidi Raisi wa JMTZ ndani ya TanZania na akashinda labda iwe vita kutoka nje ya mipaka ya TanZania na siyo ndani, sababu ni kwamba kutangaza Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ ina maana unatangaza Vita na Nchi ya TanZania, hivyo nchi ya TanZania itatumia arsenal yake yote dhidi yako na hakuna mwenye huwo ubavu, subiri utaona kama ni kweli ametangaza Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ atanywea TU!
Katiba yetu inampa Raisi nguvu nyingi sana na kamwe hauwezi kupingana naye na ndio maana Mlm.Nyerere aliweza kuchukuwa Shule, Hospitali nyumba ktk kwa Makanisa, Misikiti na Wafanyabiashara wakubwa wa Kizungu, Wakihindi na Wakiarabu!
Hivyo kuanzisha vita dhidi Raisi wa JMTZ ndani ya TZ ni kutokuwa na akili na wenye akili wamekaa kimya kama akina Mengi, Manji n.k kwa maana wanajua hauwezi kushinda hata akina Kingunge, Mwapachu & Co. wako kimya na hawafungui mdomo dhidi ya Raisi wa JMTZ na sababu wanajua kwamba hawawezi kushinda!
Kwabwana membe hapa lazima kutakuwa na "conflict of interest si bure". Ila siungi mkono kabisa swala wafanyabiashara kutofuatiliwa. Haiwezekani waokutaka kutawala nchi huku walalahoi machache wakiumia1 serikali ya Magufuli kimsingi sio ndogo
Nje Magufuli ataenda atake asitake
2 uchaguzi Zanzibar haukapaswa kufutwa wote
3 wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa ...............
Vipi Membe ulikua wapi ?? Au ndio fitina za Manguli ccm zimeanza ,naona kama safari yako ya urais 2020 umeianza rasmi ,vipi Magufuli mnataka kumpiga chini ???
Sina maana ya kua napinga anachosema Membe kimsingi inahitaji tafakuri ya kutosha