Savimbi Jr
JF-Expert Member
- Sep 23, 2011
- 6,818
- 9,181
Funguka Funguka mzee wa Libya.
Ndio maana anabwabwaja kumbe keshàanza kubinywa k*nde kwa kuwa alizoea kukwepa kodi!!!Ukanda wote wa kusini kafungua vituo vya kuuza mafuta
Hapana...kwa maana nyingine ni....Magufuli apunguze kuwabana wakepa ushuru na wahujumu uchumi.....silly boyYaani kwanamna nyingine tunaweza kusema,kuwa Dr.Magufuli apunguze kukurupuka.
Membe sijui kapanic nini aisee!! Hawaoni watu wenye pesa kama mmiliki wa Bayern Munchen yuko jela kwa kosa la kukwepa kodi!! Yaani bongo eti mfanyabiashara asiguswe kisa nchi itayumba!!! Upuuzi gani huu!! Tena kwa mtu aliyekuwa anautaka urais wa nchi!Members atulie watu wafanye kazi,anataka Tanzania iendelee kua ombaomba kwa sababu gani?hao wafanya biashara wameona Tanzania panalipa na kuna faida kuna ubaya gani wao kulipa kodi?mbona wafanyakazi wa kipato cha chini wanakatwa kodi?.Yesu mwenyewe alilipa kodi...hapa ni kodi tu hawawezi waache biashara. Ulaya kodi ni muhimu ndio maana anayekwepa anashitakiwa na kwenda jela maana ni jipu la umaskini.hamna namna walipe kodi tu.
Ndugu UMENENA. Hilo ndio suluhisho. Kwa kweli hizi kodi, ushuru nk si realistic hata kidogo kwa sababu ulizosema za mtu moja akishakadiria basi tena na mara nyingi viwango wanavyokadiria ni vya kukutisha ili utoe rushwa.Suluhisho ni kubadilisha sheria za kodi kila mtu alipe kodi inayostahili na inayolipika, sheria ya kuruhusu afisa wa kodi akadirie anayoona inafaa ndio inawalazimisha wafanyabiashara watoe rushwa kwa hawa maafisa wanakupiga kodi ya juu makusudi, ijulikane kama in kontena la matairi na limenunuliwa kwa sh.100 kodo ni asilimia ngapi na kama ni gari imenunuliwa kwa sh50 kodi ni asilimia ngapi kwa sasa unaagiza gari wanakupigia hesabu ya kodi,ukileta bandarini kodi inapanda hii si sawa, Apeleke mswaada wa sheria ya kodi bungeni ibadilishwe, hii iliwekwa ili watu wapige pesa na kuwapendelea watu wachache, na wafanya biashara waache kujipendekeza kwa cccmmm, wasimamie na sheria zitakazowezesha kufanya biashara kwa uhuru sio kutegemea kubebwa na wanasiasa.
CCM watamtukana membe kila aina ya tusi.
Wafanyabiashara wanatakiwa waliope kodi tu sio wanaagiza kontena 70 wanalipia 20 zingine nyinyi watetezi wao mnakula mgaoAliyekuwa waziri wa Mambo ya nje Mh.Membe ameonya kuwa wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa.Ametanguliza kuwa anaunga mkono mikakati ya ukusanyaji kodi lakini isiwe katika hali ya kukatisha tamaa na kudidimiza uchumi.Membe ameonya hayo kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara kulalamika kuwa baadhi ya mikakati inaelekea kuwadidimiza.Haya yameandikwa katika magazeti ya leo
Msukuma kwani ni mtu au Msukule?Kwa sasa washauri wa nje ni muhimu,wale waliopewa vyeo hawana jeuri ya kumkosoa Magufuli.nilimsikia mbunge Msukuma akisema watafata yote atakayoagiza Magufuli
Katumwa na Baba MirajiHuyu membe vp katumwa.
1.baraza kubwa
2.kusfir nje ni lazma
3. Asiwabane wafanyabiashara...
Nan anampa hyo airtime kila siku
Aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje Mh. Membe ameonya kuwa wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa.
Ametanguliza kuwa anaunga mkono mikakati ya ukusanyaji kodi lakini isiwe katika hali ya kukatisha tamaa na kudidimiza uchumi.
Membe ameonya hayo kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara kulalamika kuwa baadhi ya mikakati inaelekea kuwadidimiza.
Haya yameandikwa katika magazeti ya leo
Huu ndio utamaduni wetu wa siasa za kijima. Hata Mhe JPM asingethubutu kumshauri JK wakati alipokuwa waziri wake (miaka 10) kwenye yale aliyokuwa akiona hayendi sawa. Ushahidi ni misimamo ambayo anaoinesha katika siku zake za mwanzo wa utawala wake. Ndiyo maana wapenda mabadiliko ya kweli, tunalilia Katiba ya Wananchi ambayo itapungunza umungu mtu wa Rais wa JMT. Hawa wanakuwa miungu watu kiasi cha washauri wao, hususan washauri wakuu ambao ni mawaziri, kuogopa kuwaambia ukweli. Wakiwa uchi wanashangiliwa kuwa wamevaa! Si jambo la siha kwa maendeleo ya nchi.Kwa sasa washauri wa nje ni muhimu,wale waliopewa vyeo hawana jeuri ya kumkosoa Magufuli.nilimsikia mbunge Msukuma akisema watafata yote atakayoagiza Magufuli