Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,471
- 11,454
Sayyed Hassan Nasrala katika hotuba yake wiki iliyopita aliionya Marekani kutokana na uungaji wake mkono maafa kwa wapalestina akiiambia kuwa tayari wana kitu mkononi kwa meli zake za kivita zilizotia nanga karibu na nchi hiyo.
Kitu hicho kizito inaaminika ni aina ya makombora mazito ya kuzamisha meli ambayo imeshayapokea kutoka Urusi kupitia Syria.
Makombora hayo inasemekana ni Yakhont missile yenye uwezo wa kupiga mpaka kilomita 300. Pamoja na makombora hayo Hizbollah tayari ina droni nyingi na ambazo wameshaanza kuzitumia kulenga maeneo ya kaskazini ya Israel na kusababisha hasara kwa vikosi vya IDF.
Hapo jana jeshi la Marekani limeomboleza vifo vya askari wake 5 katika eneo la Magharibi ya Lebanon ndani ya bahari ya Mediterraneo.
Katika taarifa ya jeshi hilo imeelezwa kuwa maafa hayo yaliyokea baada ya helkopta iliyokuwa kwenye mazoezi kudondoka baharini.
Akitoa pole kwa familia za askari hao Rais Biden amesema askari hao wamekufa kishujaa wakitetea nchi yao. Akasema wanawaombea mashujaa hao na watafanya hivyo kila siku.